Saturday, September 15, 2018

Mama ajifungua mapacha watano kwa mpigo

Bi Honoratha Nakato kutoka Uganda ameandika historia mpya barani Afrika baada ya kujifungua watoto watano kwa mara moja, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza chini ya Jangwa la Sahara kuzaa idadi hiyo kupitia njia ya IVF (kupandikiza mayai).

Kwa mujibu wa  Mama huyo amesema kuwa amehangaika kwa zaidi ya miaka 15 kutafuta mtoto lakini amejikuta juhudi zake zikigonga mwamba mpaka alipopata ushauri wa kutumia mfumo huo wa IVF.

”Nilipofanya uchunguzi na kuambiwa na madaktari kuwa nitajifungua niliona kama ndoto hivi, nilifanya siri kiasi kwamba hata mume wangu hakujua kama nilikuwa natarajia watoto watano, alikuwa anajua angalau wawili,” amesema Honoratha.

Honoratha ameongeza ”Niliangaika miaka mingi kutafuta mtoto, nilitembea huku na kule hadi nilipokuja kwa dokta Sad, ila wengi walinitisha kuwa nisingeweza kulipia gharama yake na hatimaye nilifikia muafaka ila sikutarajia kupata idadi hii ya watoto.”

Daktari aliyemzalisha mama huyo ameelezea namna alivyo weza kufanya uzalishaji huo huku akishindwa kuamini.

”Ilikuwa muujiza, muujiza kabisa na tofauti na tulivyofanya kabla. Tulifanya upasuaji na mtoto wangu mtoto wa kwanza alitoka kichwa chake kikiwa kimefungunguka nikasema huyu msichana tu wapili hivyo hivyo watatu mvulana,” amesema daktari

”IVF imebadilisha maisha kabisa kiasi kwamba kwa sasa hivi hakuna mwanamke asiyeweza kubeba mimba, mtazamo na hisia zawatu zimebadilika kabisa watu hawana haibu tena kwenda kufanya njia hii.”

”Wanne mvulana na watano msichana, sijawahi kumzalisha mwanamke hivi katika miaka yangu 30, yakufanya kazi hii.”

No comments: