Sunday, September 30, 2018

Mkuu wa Majeshi amwaga sifa kwa Rais Magufuli, apongeza uongozi wake


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, amesema uongozi mahiri wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli umewezesha kasi ya uokoaji na kuibua kivuko cha MV. Nyerere kufanyika kwa mafanikio makubwa.

Jenerali Mabeyo ameyasema hayo katika misa maalumu ya kuwaombea marehemu waliokufa katika ajali ya ya kivuko cha MV Nyerere, iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yuda Thadei, iliyopo Ilumia, Magu Mkoani Mwanza.

Mabeyo amesema kazi ya kubwa kuokoa kivuko kilichokuwa kimezama imesimamiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania ikishirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa Ukerewe.

"Kama ilivyo Jeshi likipewa maelekezo au amri linatekeleza kwa uweledi, na sisi tunapojipangia kazi huwa tunajiwekea na malengo,baada ya siku tatu hadi nne tukawa tumekitoa kivuko majini na watanzania wameshuhudia,daima tupo tayari kutekeleza majukumu yetu.

"Tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa umahiri wake amekuwa akitusapoti muda wote, alikuwa halali amekuwa akitupigia simu kujua maendeleo ya huku na sisi hatukusita kumpatia yaliyokuwa yanajiri", amesema Jenerali Mabeyo.

No comments: