Wednesday, January 30, 2019

Kamishna wa kupambana na kuzuia Dawa za Kulevya anena mazito


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kupambana na kuzuia Dawa za Kulevya, James Sianga amesema kazi ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya si ya kukurupuka.

Amebainisha hayo leo kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV ambapo ameeleza kuwa baada ya kuusoma vizuri mtandao wa dawa za kulevya nchi, sasa wameuvuruga mtandao huo.

"Kazi ya kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya sio kazi ya kukurupuka," amesema Kamishna Sianga.

Ameendelea kwa kusema, 'Tulipokamata kg.95 za Heroine kule Kabuku, muuzaji yule ambaye sasa hivi amehukumiwa miaka 25 jela, alisema atatoa dola 300,000, akasema twende Rose Garden atazileta pale. Tulipokamata kg. 210 kule Lindi muuzaji alisema atatoa dola 800,000, tulipokamata kemikali Bashirifu kule Mwanza muuzaji alisema anatoa milioni 800,'.

No comments: