Anne Tropeano anapiga pasi nguo zake kujiandaa kwa ajili ya siku inayokuja yenye shughuli nyingi. Anatoa alba yake nyeupe na nguo zake zilizopambwa kwa urembo, zinazovaliwa na makasisi wa Kikatoliki duniani kote.

Kwenye kalenda iliyopo ukutani, kalamu nyekundu iliyokoza inaashiria kwamba kesho ni "Siku ya Kutawazwa".

Pia anazungumza na simu akimkodi mlinzi kwa ajili ya ibada katika kanisa la Albuquerque, New Mexico, ambako anaishi - kwani anatarajia kunaweza kuwa na uhasama.

"Ni suala lenye mvutano, si kila mtu yuko wazi hata kuzingatia uwezekano wa wanawake kuitwa ukuhani," anasema. Si tu unyanyasaji wa kibinafsi ambao Tropeano anajali.

Tangu kushiriki matumaini yake ya kuwa kasisi wa Kikatoliki, anasema amepitia unyanyasaji mtandaoni wa "kuvuta pumzi".

Tropeano ni mmoja wa wanawake zaidi ya 200 duniani kote ambao ni sehemu ya vuguvugu la makasisi wa kike wa kikatoliki, kundi linaloshiriki katika ibada zisizoidhinishwa za kuwekwa wakfu na kuwa mapadre, kwa kitendo cha dharau dhidi ya Kanisa Katoliki.

Kanisa Katoliki haliruhusu wanawake kuwa makuhani. Kwa kweli, Vatican inaiona kuwa uhalifu mkubwa katika sheria ya kanuni ambayo inaadhibiwa kwa kutengwa na kanisa.

Hii ina maana kwamba wanawake, mara tu wanaposhiriki katika 'kuwekwa wakfu', hawawezi kupokea sakramenti, ikiwa ni pamoja na ushirika, au kuzikwa kwa taratibu za ya kanisa.

Kutengwa ilikuwa sababu sikuweza kuwa kasisi kwa muda mrefu," anasema. "Nilikuwa nikienda kwenye ibada ya misa kila siku. Nilifanya kazi parokiani, maisha yangu yote yalikuwa kanisani. Kwa hiyo kufikiria kuacha hilo, sikuweza hata kufikiria kabisa."

Tropeano ni Mkatoliki mwaminifu, ambaye baada ya miaka mingi ya kufanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na kusimamia bendi ya rock, alisikia wito wa ukasisi: "Ningesikia haya.

Wewe ni kasisi wangu, wewe ni kasisi. Nataka uwe kasisi." Chaguo pekee lililokuwa wazi kwake kama mwanamke lilikuwa kutumikia Kanisa katika nafasi nyingine - kama vile mtawa au mchangiaji mlezi katika jimbo lake. Au angeweza kuondoka kabisa kutoka ukatoliki, kwenda dhehebu lingine la Kikristo ambalo lingemkaribisha kama kasisi.

Baada ya miaka ya utambuzi wa kibinafsi, alibaini upungufu wa sheria za Vatican hazingemwacha aishi wito huu: "Mara nilipotambua kwamba hii ilikuwa hatua inayofuata, kutengwa ilikuwa sehemu tu ya safari."

Tropeano, na wanawake wengine kama yeye, pia wanaona chaguo lao 'kuwekwa wakfu' kama njia ya kufanya kampeni dhidi ya kile wanachokiona kuwa utawala wa kijinsia wa Kanisa.

KINGOTANZANIA

0752881456