Monday, October 8, 2012

AJALI YA MBAYA ILIYO UWA WATU 11 MBALIZI MBEYA , MASHUHUDA WAZUNGUMZIA MAMBO YA AJABU WALIYO YAONA KABLA NA BAADA YA AJALI!

AJALI YA MBALIZI MBEYA ILIYO UA WATU KUMI  NA MOJA

Na: Mwandishi wetu
ILE ajali ya kutisha iliyoshirikisha magari matatu, likiwemo la Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM, Mkoa wa Mbeya, Dk. Marry Mwanjelwa na kuua watu 11, imesimuliwa mambo ya kutisha, Risasi Jumamosi linashuka nayo.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 2, mwaka huu, Mbalizi, Mbeya Vijijini ambapo magari matatu, likiwemo lori lililosababisha ajali yaligongana na kupinduka kisha kuwaka moto na kuteketea na baadhi ya watu.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na Risasi Jumamosi, hakuna shaka eneo hilo limetawaliwa na majini kwa vile haupiti mwezi bila kutokea ajali ya kutisha.
“Sisi tunasema hapa kuna majini jamani, hapapiti mwezi  lazima itokee ajali, serikali ielewe hilo jamani,” alisema Mzee Simon Mwalusale, mkazi wa ene hilo.
Pia yapo maelezo kuwa, mapema siku ya tukio, kulionekana noti za shilingi elfu kumi zikipeperuka eneo hilo na watu waliziokota.
“Kuna jambo lingine la ajabu sana, siku ya tukio, mapema zilionekana noti za elfu kumikumi, watu waliziokota licha ya kwamba hazikujulikana zilikokuwa zikitokea.
“Cha kushangaza, zile noti zilikuwa na damudamu, lakini hilo watu hawakulijali, waliziokota na kuziweka mifukoni mwao,” aliongeza mzee huyo.
Wakati huohuo, umoja wa wachungaji, Mbalizi, wakiongozwa na mchungaji aliyetambulika kwa jina moja la Daudi wanajipanga kufanya maombi eneo hilo ili kama kuna nguvu za giza zinazosababisha ajali mara kwa mara ziondoke.
Oktoba 4, 2012, jijini Dar katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dk. Mwanjelwa ambaye alifikishwa hospitalini hapo kutoka Mbeya kwa matibabu zaidi, alizungumza na mwandishi wetu akiwa katika chumba maalum cha uangalizi. 
“Nilikuwa nikishuhudia ile ajali kwani lori lilikuwa nyuma yetu kwa kasi huku likionekana breki ziligoma na ndipo lilipotuvamia na kutugonga.
“Nilisikia kishindo kikubwa kikitokea, nilijua ndiyo mwisho wa uhai wangu hapa duniani, lakini Mungu mkubwa bado niko hai.
“Nawashukuru wasamaria wema na askari waliokuja kutuokoa, ila nimeumia sana niliposikia kuna watu 11 walikufa na wengine kujeruhiwa vibaya.
“Sasa naendelea vizuri tofauti na nilivyoletwa (Jumatano), nawashukuru madaktari na wauguzi kwa jitihada zao,” alisema Dk. Mwanjelwa.

CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS INFO
DR MARY MWANJELWA MBUNGE VITI MAALUM MBEYA
Akiwa katika matibabu Dar es salam kwa mbeya uchaguzi ulikuwa unaendelea  na Mary Mwanjelwa akiwaMjumbe wa Baraza Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, aliyekuwa akitetea nafasi hiyo Dk.Mary alijikuta akishindwa vibaya na mpinzani wake mkubwa kisiasa, Edina Mwaigomole.
Dk.Mary na Edina ni wanasiasa wanaokubalika ndani ya UWT mkoani hapa na wenye upinzani mkali kisiasa, kwani hata katika kinyang’anyiro cha ubunge viti maalum mkoani hapa walishindana kwa kura chache.
Nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, ambayo ilikuwa na wagombea watatu, Shizya Mwakatundu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mbeya mjini ameibuka kidedea.
Nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa ilichukuliwa na Jane Dussu, wakati nafasi ya Uwakilishi wa Jumuia ya Wazazi ilinyakuliwa na Florence Mwakanyamale huku, Uwakilishi wa Vijana ukichukuliwa na Maryprisca Mahundi.

No comments: