Wednesday, October 10, 2012

WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA WAPATA HALMASHAURI MBILI RUNGWE NA BUSOKELO


KABLA BARAZA LA MADIWANI HALIJAVUNJWA

MHE, HILDA NGOYE MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MBEYAAKIFUATILIA MCHAKATO KWA MAKINI

MKUUWA WILAYA RUNGWE CYPLIAN MEELA AKIONGEA NA MADIWANI

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA RUNGWE NOEL MAHYENGA AKISOMA TAARIFA YA KUUNDWA

MKUU WA MKOA WA MBEYA  ABAS KANDORO AKIKABIDHI CHETI CHA KUANZISHWA RASM KWA HALMASHAURI YA BUSOKELO

PICHA YA PAMOJA YA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA BUSOKELO

PICHA YA PAMOJA YA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA RUNGWE

WAANDISHI WA HABARI WAKIONGEA NA MWENYEKITI MPYA WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MHE, MECKSON MWAKIPUNGA

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABAS KANDORO AMEVUNJA BARAZA LA MADIWANI  WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA NA KUTANGANZA RASMI HALMASHAURI YA RUNGWE ITAKAYO KUWA NA KATA 26 NA KUITANGAZA HALMASHAURI YA BUSOKELO ITAKAUO KUWA NA KATA KUMI NA MOJA.

AKIONGEA NA BARAZA LA MADIWANI MKUU WA MKOA WA MBEYA AMSEMA KUWA SERIKALI IMEANZISHA KIFUNGU (sub_vote) Na>7813140 NA KUTENGA FEDHA KWENYE BAJET YA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 KWA AJILI  YA HALMASHAURI  YA BUSOKELO, YENYE JUMLA YA TSH 12,549,250,889/=

HALMASHAURI YA RUNGWE ITAKUWA IKIONGOZWA NA MKURUGENZI NOEL MAHYENGA  PIA HALMASHAURI YA BUSOKELO ITAKUWA INAONGOZWA NA IMELDA ISHUZA ALIYETEULIWA  KUIONGOZA HALMASHAURI YA BUSOKELO INAYOANZA LEO KUWAHUDUMIA WANANCHI WA BUSOKELO.

AKITOA SARAM ZA MKOA MKUU WA MKOA WA MBEYA KANDORO  AMEWATAKA WANANCHI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUCHANGIA SHUGHURI ZA MAENDELEO NA HILI  ITAZIZIFANYA HALMASHAURI KUWA  MAENDELEO ZAIDI.  

PIA  AMESEMA HAITAKUWA NA MAANA KUWA NA HALMASAHAURI  MBILI BILA YA KUJIBIDISHA KUFANYA KAZI ZA MAENDELEO NA KUKUSANYA USHURU ILI KUJIWEZESHA KUJITEGEMEA
ZAIDI AMEWAPONGEZA WANANCHI WA BUSOKELO KUPATA HUDUMA ZA MAENDELEO KARIBU  NA WAO 

 AMEWAHAKIKISHIA KUWA SERIKALI KWA KUZINGATIA AHADI YA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE ALIYOITOA  KATIKA KIPINDI CHA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010 OMBI LILILOTOLEWA NA MBUNGE WA RUNGWE MASHARIKA PROF MARK MWANDOSYA KATIKA KIWANJA CHA TANDALE  NA RAIS  ALIAHIDI KUIFANYA WILAYA YA RUNGWE KUWA NA HALMASHAURI MBILI RUNGWE NA BUSOKELO  NA BAADA YAMCHAKATO WA MUDA MLEFU HATIMAYE LEO AHADI HIYO YA RAIS WA TANZANIA DR JAKAYA M. KIKWETE IMETIMIA KWA WILAYA YA RUNGWE KUPATA HALMASHAURI YA MPYA YA BUSOKELO.

(JE WANANCHI WANATARAJIA NINI BAADA YA KUUNDWA KWA HALMASHAURI MBILI KATIKA WILAYA YA RUNGWE? FUATANA NAMI KWA MATUKIO. )

ALLY KINGO
0752881456
Post a Comment