Wednesday, October 10, 2012

UBOVU WA MIUNDO MBINU ILEJE WACHANGIA HALI MBAYA YA MAISHA

BARABARA YA ILEJE NA CHANGAMOTO ZAKE KESHO KUTWA NASAFIRI KWENDA HUKO NGOJA TUKAJIONEE KULIVYO TUWE SOTE KATIKA SAFARI
UBOVU wa bara bara katika Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya  umesababisha  hali za maisha za wananchi  wa wilaya hiyo kuendelea  kuwa duni kutokana  na  kushindwa kusafilisha mazao wanayolima kwenda mikoa  mingine.

Akizungumza na mwandishi  Esthar Macha mdau wa mtandao  huu ofisini kwake  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi.Rosemary Senyamule alisema hayo kufuatia ubovu  huo wa bara bara ambao umedumu kwa muda mrefu  bila jitihada zozote za kuhakikisha kuwa zinatengenezwa ili wananchi waweze kuwa na hali nzuri za kimaisha.

Alisema kuwa  ubovu huo  wa bara bara umekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi na hata kushindwa kushindwa kusafilisha mazao  na vitu vingine ambavyo ni mkombozi kwa wananchi  ambavyo vingeweza  kuokoa  hali za maisha.

“Hili suala la miundo mbinu katika wilaya hii ni tatizo kubwa sana ambalo linasababisha uchumi wa wananchi wa wilaya hii kuendelea duni ,ili kuweza kufanikisha hili serikali inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha  kuwa miundo mbinu hii inatengenezwa mapema”alisema.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema hilo likifanikisha  hali ya uchumi kwa wananchi itaweza  kubadilika haraka na wanancghi kuweza kufanya kazi zao kwa mara moja ,hivi sasa safari ya kutoka Mpemba Ileje mwananchi anatumia masaa matatu mpaka manne wakati ni safari ya saa moja tu.

Aidha Bi.Senyamule alisema kama serikali wanaendelea na   na jitihada aza kuhakikisha kuwa bara bara hiyo inatengenezwa  na kupewa kipaumbele kwenye bajeti  ijayo .

Mmoja wa wananchi wa Tarafa ya Kipambawe Wilayani hapa Bw.Sifanuel Luka alisema kuwa tatizo la kutokuwa na bara bara nzuri katika wilaya hiyo limekuwa ni shida kubwa kwao kwa kushindwa kusafirisha vitu muhimu kwao ambavyo vingeweza kuondoa ugumu wa maisha.

“Kwa ujumla hili ni tatizo kubwa sana sehemu ya kwenda na kurudi inakulazimu mpaka ulale  kwa hali hii maisha  lazima yawe magumu  kwa sisi wananchi,wilaya hii ni muda mrefu hebu angalia maisha ya wananchi wa wilaya hii walivyo na maisha magumu serikali ifanye jitihada mapema kuhakikisha kuwa bara bara hii inatengenezwa haraka”alisema.
 
o752-881456
Kingo

No comments: