Sunday, October 28, 2012

WABUNGE-KUKATAA POSHO NI UNAFKI

Mhe Peter Serukamba
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia CCM Mhe Peter Serukamba amesema suala la baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga posho lilikuwa ni unafiki. Serukamba aliyasema hayo katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango kupitia Magic FM. Fina aliuliza moja ya swali kutoka kwa wasilizaji ambapo alisema biashara ya kukataa posho ni unafiki tu huku akimwambia Fina ataje mbunge gani karudisha au kukataa posho, alisema "Tumeongezewa mafuta tumechukua, tumeongezewa vingine tumechukua hakuna ambaye amerudisha na next day ilipokuwa confirmed wengine wakaanza kukopa" huku akisema hakuna umuhimu wa kupinga posho za wabunge badala yake wabunge waombe serikali iwaongezee posho na watumishi wengine. Alipoulizwa kwa nini wasiiombe serikali ianze na sehemu nyingine kabla ya kuwaongezea mshahara wabunge akitolea mfano wa shirika la ndege la taifa ATCL Serukamba alijibu kuwa siku zote binadamu anaanza na "mimi" kabla hujawafikiria wengine akikumbushia siku alivyopendekeza kama bunge lifungwe kama watu hawataki wabunge wapokee posho na kuishia kushambuliwa kupitia mitandao ya kijamii. Serukamba aliongezea kusema kuwa bunge la Tanzania ni kati ya mabunge yanayolipa hela ndogo sana watumishi wake ambazo ni milioni mbili tu kwa mwezi bila posho na kusema wanazidiwa na bunge la nchi ya Burundi wanaolipwa dola 4,500 za Marekani. Alimalizia kwa kusema jukumu la wabunge libaki kuwa kutekeleza wajibu wao wa kibunge ambao ni kutunga sheria na kuisimamia serikali itekeleze wajibu wake. Photo Caption 1. Mhe Peter Serukamba akikongea katika kipindi cha Makutano
Post a Comment