Saturday, November 24, 2012

KATIBU MKUU WA CCM ASEMA SASA NI MUDA WA KAZI KWA VITENDO

KINANA AKIONGEA NA MAELFU YA WAKAZI WA ARUSHA
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahaman Kinana, amewataka mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne kufanya kazi kwa kasi ili kutekeleza ilani ya uchaguzi kwani wakishindwa kufanya hivyo watawajibishwa na chama.Alisema chama hakitawavumilia mawaziri ambao hawatekelezi majukumu yao na kukifanya chama hicho kichukiwe na wananchi.
Alisema kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) mawaziri watakuwa wakitoa taarifa za utendaji kazi na kwamba wajumbe wa Nec watawabana kwa maswali ili kupata ufafanuzi wa kina katika masuala mbalimbali ya wizara zao.Alisema kila waziri, mbunge na Diwani anayetokana na chama hicho atakuwa akipimwa utendaji wake katika kuwahudumia wananchi wa eneo lake na taifa kwa ujumla.
Kinana alisema hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyejuu ya chama hicho bali chama kipo juu yao na ni wajibu wao kuwa watiifu kwa chama na wananchi wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.
“Naomba ieleweke kwamba CCM imejipanga katika kuwaunganisha na kuwahudumia Watanzania, hivi sasa tunaanza utaratibu mpya ambapo mawaziri watakuwa wakitoa maelezo.
Alisema kama kuna kiongozi ambaye ataona kuwa kasi yetu ni kubwa ni bora akaachia ngazi.

Akizungumzia makundi ndani ya chama hicho , Kinana alisema kuwa tangu ulipomalizika uchaguzi wa ndani kuna baadhi ya viongozi walioshindwa wamekuwa wabinafsi kwa kutochaguliwa katika nafasi za uongozi hali inayowafanya kujiona bora kuliko wengine.

Alisema kutokana na hali hiyo kuna baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wabinafsi huku wakiibuka na sababu mbalimbali ikiwamo rushwa.
“Watu wamekuwa wabinafsi kwa kukosa nafasi za kuchaguliwa ndani ya chama. Kama hakupita anaibuka na sababu lukuki na hata kudai aliyechaguliwa hafai bali yeye ndiye anayefaa,” alisema.
Kinana akizungumzia utendaji kazi wa mawaziri alisema kuanzia kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, watakuwa wakitoa taarifa hizo ambapo wajumbe wa NEC watawabana kwa maswali na kuhitaji ufafanuzi wa kina katika masuala mbalimbali ya wizara zao.

Alisema kila Waziri, Mbunge na Diwani anayetokana na chama hicho atakuwa akipimwa utendaji wake katika kuwahudumia wananchi wa eneo lake na Taifa kwa ujumla.

Alisema hakuna kiongozi yoyote wa Serikali aliyekuwa juu ya chama bali chama kipo juu yao na wajibu wao kuwa watiifu kwa chama na wananchi wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.
“Ninapenda ifahamike sasa CCM, imejipanga katika kuwaunganisha na kuwahudumia Watanzania, hivi sasa tunaanza utaratibu mpya ambapo Mawaziri watakuwa wakitoa taarifa zao katika vikao vya NEC na kuhojiwa maswali na wajumbe.

“Kila Waziri atahojiwa utendaji wa shughuli za Serikali katika Wizara yake na utekelezaji wa ilani na ikiwa kuna atakayeonekana kuwa hafai hatua zitachukuliwa stahiki zitachukuliwa.
Post a Comment