Monday, December 17, 2012

ALIYEDHANIWA AMEKUFA KWENYE AJALI ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA JUMAMOSI AFUNGA NDOA HAKIKA MUNGU NI MKUU


Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth  Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya
Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100  Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia jumamosi mida ya saa sita nanusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya mafiati mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo 
Hii ndiyo hali halisi iliyotokea siku hiyo ya ajali mbeya yetu tulifika usiku huo eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ndipo jana tukaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo tukaenda kufuatilia harusi hiyo  katika kanisa la agape 
Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani
Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa
Sasa bwana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa
Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T toka DSM ndiyo aliyofungisha ndoa hiyo
Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete  huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea
Hapa wakipata mibaraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE
Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe
Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota

Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa
Maharusi wakiwa na familia na wazazi wao
Sherehe fupi ya kuwapongeza maharusi ilifanyika katika bustani ya ccm jijini mbeya
Ndugu jamaa na marafiki walihudhuria sherehe hiyo ingawa maharusi hawakuweza fika kwenye sherehe hiyo kutokana hali yake haikuwa nzuri alihitaji kupumzika na kurejea tena hospitali kuendelea na matibabu
Dr Tuntufye na mkwe wakiwa katika chakula baada ya harusi kufungwa na kwa tarifa kutoka  kwa Dr Tuntufye usiku bwana harusi Emmanuel Mwangusi alizidia na kukimbizwa hosptal kwa matibabu zaid na hadi sasa Bibi harusi anaendelea kumuuguza mume wake hospitali ya rufaa

 Chagua Maisha Unayotaka Kuyaishi Na Uyaishi Kweli’

Filikunjombe Anena Mbele Ya Mangula

 Viongozi   wa CCM mkoa  Njombe  wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza  wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo  wa kwanza  kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika  wa bunge Anne Makinda  wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike
Deo Filikunjombe miongoni mwa wananchi


Msafara wa pikipiki kwenye mapokezi ya Mangula Njombe
Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara  Philip Mangula.

Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.


" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama  chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .


Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.Kwa Upande wake  Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa  ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.


" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.


Aidha amehimiza  nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya  Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.


Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa  bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo...
LOWASA NA HARAMBEE MAKANISANI NINI SIRI YAKE? 

Lowassa Ashiriki Harambee Ya Kanisa Akyeri Meru

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo,iliyofanyika leo Mkoani humo.Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
===========     =========   =========
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari. ”tunashuhudia maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu. Huko nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala hilo”alisema Lowassa. Lowassa ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2. Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.

Kwa upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.”Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako”alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada
Post a Comment