Tuesday, December 18, 2012

Madhehebu Ya Dini Yaaswa Kusaidia Wasiojiweza


 Katibu VICOBA kanisa KKKT, Usharika Amani, Singida mjini Mwl Anna Abdalah akikabidhi mafuta ya kula, ikiwa ni sehemu ya msaada
 Mwenyekiti wa VICOBA Kanisa la KKKT Amani, Singida mjini, Happy Francis akikabidhi sehemu ya msaada
Mchungaji Shadrack Langu (katikati), wa kanisa la KKKT Amani akiwa na baadhi ya watoto na kikundi cha VICOBA baada ya kukabidhi
 
Singida
Desemba 17, 2012.
KANISA la KKKT-Dayosisi ya kati Usharika Amani Singida mjini, umetoa wito kwa madhehebu ya dini kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza ikiwemo watoto wanaoishi mazingira hatarishi.
Wito huo umetolewa na Mchungaji wa usharika huo, Shadrack Langu, wakati wa makabidhiano ya msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa kituo cha Malezi, Kititimo mjini Singida.
A u, ili kujemesema utoaji wa misaada hiyo kwa makundi yasiyojiweza, itasaidia kuijenga moyo wa upendo baina yao.
Msaada huo wa kibinadamu uneotolewa na kikundi cha VICOBA, chini ya kanisa hilo, kwa ajili ya kituo hicho, chenye jumla ya watoto 40. 
Mchungaji Langu amesema moja ya majukumu ya kanisa ni kuia jamii, hususani makundi yasiyojiweza ili kuwajenga kimwili na kiroho baadaye wamudu maisha yao.
“Kazi ya kanisa ni kuhakikisha mwanadamu anakombolewa katika maisha yake…ndiyo maana hata wamisionari walipokuja kwetu, walipojenga shule, walijenga pia zahanati na hospitali ili kusaidia jamii kimwili,”alisema mchungaji Langu.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, katibu wa VICOBA –KKKT Amani, Mwalimu Anna Abdalah aliwaasa watoto hao kuondokana na huzuni badala yake wajione wapo sawa na watoto wanaokula, kulala na kuishi na sehemu nzuri wakiwa na wazazi wao.
Kwa upande wake mwangalizi wa kituo hicho anayetumia maisha yake kuishi na kuwahudumia watoto hao, Ali Makala alishukuru msaada huo na kuiomba jamii kuiga mfano wa akina mama wa VICOBA kutoka usharika wa Amani katika kusaidia kituo hicho.
Msaada huo unaojumuisha unga wa sembe kilo 150, mchele kilo 100, mafuta ya kula, sabuni,  maharage, mafuta ya kupaka, dawa ya meno, kalamu, daftari, juisi, biskuti, miswaki na dawa ya kuulia kunguni, una thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.1.

Mkutano Wa Waandishi Wa Habari CHADEMA,Maazimio Ya Kamati Kuu

 Mh.Freeman Mbowe,Mwenyeketi wa CHADEMA Taifa
 Dr.Wilbrod Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA
 Viongozi wa CHADEMA Taifa
 Baadhi ya waandishi
Mkutano na waandishi habari unaendelea.mh.Mbowe anaongea.
1.KIKAO cha kamati kuu kilikuwa cha kawaida ,hakuna jambo la dharula
2.Mchakato wa katiba mpya usiathiri mabadiliko ya sheria nyingine kama mabadiliko ya sheria ya uchaguzi
3.Mwaka 2013,ni mwaka wa nguvu ya umma,hakuna kubembelazana na serikali.rais kikwete hajajibu madai ya CHADEMA kwa hiyo atashinikizwa.
4.sehemu ambazo CCM wanaogopa kuitisha uchaguzi,wanalazimishwa kuitisha uchaguzi.kata za arusha mjini,sengerema,nk.ziko 15
5.Uongozi wa KARATU wa CHADEMA umesimamishwa kwa muda mpaka chama kitakapokamilisha uchunguzi wake huko.wanasheria Marando na Prof Safari watachunguza kashfa za mtu mmojammoja huko karatu.,
Taarifa kamili itawajia

Kada Wa Chadema UK Atimkia CCM!

Leo hii nimeamua rasmi kurudi CCM, chama ambacho nimekifahamu kwa miaka 35 sasa.

  Nilijiunga na Chadema kwa matumaini niliyokuwa nayo kuwa ni chama kitakachomkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini na kumfikisha kwenye level sawa na watu wa mataifa mengine kama Botswana , Namibia au hata baadhi ya nchi za Ulaya.

Niliamua haya baada ya kufuatilia yanayoandikwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu mie binafsi kwa sasa naishi UK hivyo basi mambo mengi yatokeayo nyumbani huwa nayapata kwa kusoma magazeti na blogs mbali mbali.

Nilifanikiwa kukutana na Mheshimiwa Lema hapa London ambapo tukapanga mikakati ya kukijenga chama hapa UK na nikapewa jukumu la kufungua matawi nchi nzima na kuhamasisha Watanzania, kazi ambayo niliifanya kwa moyo mmoja. Pia nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chadema UK.

Nimefanikiwa kuhamasisha watu wengi na baada ya miezi michache niliamua kwenda nyumbani kuona hali ilivyo. Niliyoyakuta ilikuwa tofauti na niliyokuwa nikiyasikia na kusoma.

NIMEKUTA BARABARA NZURI SIJAWAHI KUONA TOKA NIZALIWE NA ZINAENDELA KUJENGWA!

SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA NA VYUO VIKUU VYA KUJICHAGULIA.

MAISHA YA WATANZANIA YAMEBADILIKA SANA - MIDDLE CLASS NI MAISHA YA KAWAIDA TU. VIJANA WENGI WAMEENDELEA TOFAUTI NA ZAMANI MPAKA UWE MCHAWI KIDOGO NDIO UWE TAJIRI. MIJI INAJENGEKA KWA KASI YA AJABU. UKIHARIBU KAZINI UTAWAJIBIKA .

 Na mengine mengi tu niliyaona mpaka nikaanza kujiuliza , hivi najiita mpinzani, NINAPINGA NINI?

 Kama ni maendeleo nayaona tena maendelo original Nikakumbuka msemo mmoja... “KWA NINI UHANGAIKE NA FOTOKOPI WAKATI ORIGINAL IPOO?”

Kwangu mimi CCM ni original na Chadema ni photocopy, tena copy iliyotolewa wakati mashine imekwisha wino . Mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya CCM na si kwingineko!

 Kuna mengi mazito yamenichefua Chadema lakini sitayasema leo. Juzi mwenyekiti wangu wa Taifa Mheshimiwa Mbowe alipita hapa UK, lakini, mpaka ameondoka hakutaka kuwasiliana na kiongozi yoyote wa Chadema hapa UK kitendo ambacho kiliniuma sana, kwani, niliona kama tumedharauliwa;

  BABA HUWEZI KWENDA SEHEMU WALIPO WANAO UKASHINDWA HATA KUWAPIGIA SIMU KUWAJULIA HALI.

Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wangu utaeleweka. Kama tujuavyo, kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, lakini naona kwenye msafara wa Chadema idadi ya kenge inazidi mamba.

Chris Lukosi
Post a Comment