Thursday, December 20, 2012

Lema Mbunge Arusha Ashinda Rufaa

Lema arudi mjengoni, kwa habari zaidi endelea kusoma mjengwa blog baadae

Daktari Wa Rufaa Mbeya Atiwa Mbaroni Kwa Madai Ya Kupokea Rushwa

DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh 100,000
Hapa daktari huyo akiwa na maafisa wa takukuru wakiingia mahakamani
Hapa Dr huyo akiongea na wakili wake

DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgonjwa aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata ajali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego.Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani  majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi. 

Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod Mafwele.Waendesha mashitaka hao walidai kuwa Disemba 19 majira ya asubuhi akiwa katika sehemu yake ya kazi katika kitengo cha upasuaji, mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la kushawishi rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown, aliyefika hapo kwa lengo la kupatiwa matibabu. 

Walisema katika kosa la pili, siku hiyo majira ya saa nane mchana akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la Victoria iliyopo Jijini hapa, mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo ya shilingi 100,000, huku akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria.Walisema kuwa kwa mujibu wa sheria za taasisi hiyo, makosa yote yaliyotendwa na mshitakiwa yanaangukia kwenye kifungu cha 15 ibara ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo, Wakili wa mshtakiwa huyo, Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama impe dhamana mteja wake akidai kuwa makosa yanayomkabili yanadhaminika. Hakimu Kishenyi alikubaliana na maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote yanayomkabili mshtakiwa yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi.Alimtaka mshtakiwa huyo kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani ya Sh,500,000, na kwamba awe na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa serikali ya mtaa .

Hata hivyo mahakama ililazimika kuahirishwa kwa muda wa dakika 20 ili kutoa nafasi kwa mdhamini wa mshitakiwa kuleta barua hiyo baada ya kudai kuwa alikuwa ameisahau kwenye gari lililokuwa nje ya jingo la mahakama.Baada ya kupokea ombi hilo hakimu Kishenyi aliwahoji waendesha mashitaka kama wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja walikubali kwa maelezo kuwa dhamana ni haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo hawakuwa na pingamizi. 

Mshitakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana hiyo na hivyo kuachiwa huru hadi januari 7 mwaka 20013 ambapo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo.Kwa mujibu wa kumbukumbu za mahama hiyo, mshitakiwa huyo Daktari Kisabi ni mmoja wa mashahidi wa kesi nyingine inayoendelea mahakamani hapo ya mtoto Anethi anayedaiwa kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani na kulazimishwa kula kinyesi chake na Shangaziyake  
 
Habari na moses picha Mbeya yetu
 

Jeshi La Polisi Latoa Siku Saba Kwa Baadhi Ya Askari Wanaodaiwa Kuiba Milioni 150 Zilizo Porwa

JESHI la Polisi limetoa siku saba kwa baadhi ya askari kuzisalimisha  fedha zipatazo sh milioni 150 wanazodaiwa kuiba, ambazo zilizoporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston jijini Dar es Salaam juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo la wapelelezi ili kujua ukweli wa madai hayo.
Alisema Jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo.
Kamanda Kova alisema jeshi hilo lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake.
Alisema tukio hilo halikubaliki hivyo kila aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni lazima ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane haraka kuondoa shaka shaka kwa wanachi.
Kova alimtahadharisha Msangi kuwa, endapo atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi atambue hata yeye itabidi awajibike ambapo alisema vitu kama hivi vikiachwa viendelee vinaliletea jeshi hilo sifa mbaya na kupoteza imani kwa wananchi.
“Pamoja na kumkabidhi kazi hiyo Msangi lakini hata mimi sitakaa kimya bali nitalifuatilia kwa karibu ili mradi tuwapatie wananchi ukweli”alisema Kova.
Alibainisha kuwa hawezi kupinga kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo viovu bali suala hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo, ni vema wananchi wenye ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana fedha hizo.
Aidha, Kova alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi zake kwa nidhamu, uaminifu na ueledi kwani endapo ofisa au askari atakiuka maadili ya kazi yake, basi  hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi yake bila kuchelewa.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe bila kushirikisha wadau wengine kwa madai kuwa, eti lifanya kazi kwa kutii sheria zote bila kwenda kinyume.
 
SERIKALI YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA
 
 

No comments: