Tuesday, January 15, 2013

KIWANDA CHA CHAI CHA MWAKALELI KIMEANZA UZARISHAJI WA CHAI BAADA YA MUDA MLEFU KUFUNGWA KUTOKANA NA KUTOKIDHI KWA UPATIKANAJI WA MAJANI MABICHI YA CHAI YANAYOWEZA KUKIDHI UENDESHAJI WA VIWANDA VIWILI KATUMBA NA MWAKALELI.

KIWANDA CHA CHAI CHA MWAKALELI

PETER ROWLAND AKITETA JAMBO NA MENEJA UTAWALA DADA UNJILE

MR LEBI G MWAKATOBE AKIWA NA MR ODEN WAKIONGEA MAMBO MAWILI MATATU


MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSON MWAKIPUNGA AKIWA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE

BAADHI YA WAKULIMA WA CHAI WAKIFUATILIA MATUKIO KWA MAKINI


MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUANZA UZARISHAJI TENA WA CHAI KATIKA KIWANDA CHA MWAKALELI

JONSON MWAKASEGE MWENYEKITI WA BODI YA RSTGA


SEHEM YA KIWANDA JINSI CHAI INAVYOZALISHWA

HAPA CHAI ILIYOZALISHWA HUTENGWA KATIKA MAKUNDI YA TAYARI KWA MATUMIZI




CHRISPIN MEELA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE

PETER ROWLAND MKURUGENZI WA WATCO




MOSES MWIDETE DAS WA RUNGWE AKIWA NA MR KAGIZO


MUONEKANO WA MJI WA TUKUYU WILAYANI RUNGWE UKITOKEA MWAKALELI

KIWANDA CHA CHAI CHA MWAKALELI KIMEANZA UZARISHAJI WA CHAI BAADA YA MUDA MLEFU KUFUNGWA KUTOKANA NA KUTOKIDHI KWA UPATIKANAJI WA MAJANI MABICHI YA CHAI YANAYOWEZA KUKIDHI UENDESHAJI WA VIWANDA VIWILI KATUMBA NA MWAKALELI. 

WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE WANANUFAIKA NA BEI MPYA YA CHAI KWA MSIMU HUU AMBAYO WATAUZA MAJANI MABICHI YA CHAI KWA SHILINGI 231 KWA KILO , HIVYO BEI MPYA INAONGEZA TIJA YA UZALISHAJI WA MAJANI MABICHI YA CHAI  HIVYO KUFANYA VIWANDA VIWILI KATUMBA NA MWAKALELI KUJIENDESHA KWA MWAKA MZIMA .

AKIONGEA KATIKA UFUNGUZI HUO PETER ROWLAND AMABAYE NI MKURUGENZI MTENDAJI WA WATCO AMESEMA KUWA KUPANDA KWA BEI YA MAJANI MABICHI YA CHAI KUTAFANYA WAKULIMA KUNUFAIKA NA ZAO LA CHAI KWA KUWA NA MAISHA BORA NA ZAIDI AMESEMA  MWAKA 2012 MALIPO YA MALA YA PILI YAMEANZISHWA KWA WAKULIMA WADOGO WATAPOKEA ZIADA YA TSH 53/KG YA MAJANI MABICHI YA CHAI WALIYOUZA WATCO
PIA  WATCO INALIPA TSH 187 MILION KWA WAKULIMA WADAOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE KAMA MATOKEO YA UTENDAJI WAO WA KAZI MWAKA 2012  NA MALIPO YALIYOPATIKANA KWA NJIA YA MAUZO KWENYE SOKO NAFUU (Fairtrede) KIASI CHA TSH MILION 650 KIASI HIKI KIMEPATIKANA KUTOKANA NA KUUZA CHAI KATIKA SOKO NAFUU MWAKA 2012.

ZAIDI WAMEWATAKA WAKULIMA KUONGEZA UZALISHAJI WA CHAI HASA WANAOISHI HALMASHAURI YA BUSOKELO KWA KUWA NDIO WENYE KIWANDA SASA MAANA KUFUNGWA TENA KWA KIWANDA ITAKUWA HUZUNI SKWAKUWA  KIWANDA KINAONGEZA UHAKIKA WA MAISHA YA WATU KWA KUPATA AJILA NA KIPATO ZAIDI.

AKIONGEA NA WANANCHI NA WATUMISHI WA WATCO MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AMESEMA KUWA WANAICHI WAONGEZE KUPANUAJI WA  MASHAMBA YA CHAI NA WANANCHI WANAO MILIKI MASHAMBA YA UMAA WASIOTAKA KUENDELEZA AMEAGIZA MASHAMBA HAYO WAPEWE WATU WANAOZALISHA CHAI VIZURI
PIA AMEWATAKA WADAU WOTE WA CHAI KUSHIRIKIANA ILI KUZALISHA CHAI KWA WINGI ISITOKEE TENA KIWANDA KUFUNGWA KUTOKANA NA UPATIKANAJI WA MAJANI MABICHI YA CHAI KUSHUKA, ZAIDI AMEWATAKA WAKULIMA WADOGO KUUZA CHAI KATIKA KIWANDA CHAO CHA WATCO KULIKO WALIVYO SASA WAMEGAWANYIKA WENGINE KUUZA CHAI KWA MTU BINAFSI KITENDO AMBACHO INAPUNGUZA UPATKANAJI WA CHAI MBICHI  KIWANDANI HAPO.

NAYE MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSON MWAKIPUNGA AMESEMA KUWA NIFURAHA YA WANANCHI WA BUSOKELO KUONA KIWANDA KINAAZA KUFANYA KAZI BAADA YA MUDA MLEFU KUFUNGWA TANGU KIZINDULIWE NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE HAPO SEPTEMBER 2008.

CHAI YAKO TUNZA IKUTUNZE HII NIKAULI MBIU YA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE ILIYOTAMKWA NA MWENYEKITI WA BODI WA RSTGA     
  
ALLY KINGO                                                                                                                                                                       TUKUYU-MBEYA 
0752-881456

NA

Unyama mkubwa Mbeya, wawili wazikwa hai


diwani 0e655
                                    Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman
WAKAZI wawili wa Kijiji cha Karungu, Kata ya Ivuna, Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya wamefariki dunia baada ya kufukiwa wakiwa hai katika kaburi moja na marehemu wanaodaiwa kumuua, tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.


Watu hao, Ernest Molela anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 na Bibi Mizinala Nachela ambaye umri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya miaka 50, walizikwa wakiwa hai pamoja na aliyekuwa mkazi wa kijiji hicho, marehemu Nongwa Hussein.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliliambia gazeti hili jana kwa simu kuwa, tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa tano na sita mchana, muda mfupi kabla ya maziko ya Hussein.

Kabla ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, Molela na Nachela kwa nyakati tofauti walipigwa hadi kuzirai na watu wanaodaiwa kushiriki kuchimba kaburi kwa ajili ya kumzika marehemu Hussein.

Silwimba alisema Hussein alifariki dunia Jumamosi saa 10 jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu, lakini inaonekana kuwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walihusisha ugonjwa huo ambao ulisababisha kifo chake na ushirikina.

Jana mchana, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Momba aliyefahamika kwa jina la Wendo aliongoza operesheni ya kufukua kaburi walimozikwa watu hao, ambao walikutwa wakiwa wameshafariki dunia.

Silwimba alisema miili ya Molela na Nachela ilifanyiwa uchunguzi, kisha kukabidhiwa kwa ndugu na jamaa zao ambao waliifanyia mazishi jana mchana.
Mkasa wenyewe
Kundi la vijana tisa ambao wanadaiwa kuwa ndiyo waliokuwa wakichimba kaburi la marehemu Hussein walianza msako katika Kijiji cha Karungu wakiwatafuta wale waliowatuhumu kwamba ni wachawi na kwamba walihusika na kifo chake.

Silwimba alisema katika harakati zao, walikwenda nyumbani kwa George Hussein ambaye ni kaka wa marehemu lakini hawakumkuta, hivyo kuamua kuchoma moto nyumba yake kwa kuwa walikuwa wakimtuhumu kuhusika na kifo hicho.

“Baada ya kufanya uharibifu huo, walikwenda hadi nyumbani kwa Mzee Molela kisha wakamkamata na kumpiga sana hadi hali yake ikawa mbaya kisha wakambeba hadi eneo la maziko,” alisema na kuongeza:

“Waliporejea kwenye msiba walimkuta Mama Nachela naye wakamkamata na kuanza kumpiga hadi akazimia na yeye pamoja na Molela waliwavuta hadi kwenye kaburi ambako mazishi ya Nongwa (Hussein) yalifanyika.”

Alisema baada ya jeneza kushushwa kaburini, vijana hao wanaodaiwa kwamba walikuwa na hasira walimvuta Molela na kumwamuru kuweka udongo kaburini, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na hali yake kuwa mbaya.

“Baada ya kushindwa walimsukumiza kaburini na baadaye walimvuta yule mama (Nachela) ambaye naye alikuwa hajitambui na kumtupa ndani ya kaburi halafu wakawafukia wote, kisha wakaondoka,” alisema Kaimu Ofisa Mtendaji huyo.
                    

No comments: