ELIZABETH MOSHI AKIWASHUKURU WAKINA MAMA WA TUKUYU KWA KUMUAGA KWA SHEREHE ILIYOFANA NA KUFUATA MAADIRI |
ELIZABETH AKIWA NA MPAMBE WAKE WAKIINGIA UKUMBINI |
MWENYEKITI WA KAMATI AKIMSHUKURU BIBI HARUSI MTALAJIWA KWA KUJITUNZA NA KUFIKIA UTU UZIMA WA KWENDA KUOLEWA |
KATI YA ZAWADI NYINGI ALIZOPEWA ELIZABETH MOSHI |
MWL ELIZABETH SEKILE AMBAYE NDIYE MC WA SHEREHE AKIMFURAHISHA JAMBO ELIZABETH HA HA HA HA HA HA MWANAMKE KUTUNZA NDOA ( MIE NILIISIKIA KWENYE MKANDA WA VIDEO MAANA HUMO NDANI SIRUHUSIWI KUINGIA) |
ALIYESHIKA CAMERA KULIA NDIO MKE WA BAROZI WENU KINGO YEYE ALIKUWA NDIYE KATIBU WA SHEREHE YA ELIZABETI AMABAYE NI AFISA UTUMISHI ANAYETARAJIA KUFUNGA NDOA MWANZONI MWA MWEZI WA NNE JIJINI ARUSHA. |
................................................................................................................................................................
JAMBAZI SUGU LAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI KWENYE HARAKATI ZA KUTEKA MAGARI MLIMA NYOKA JIJINI MBEYA
Mwili wa Jambazi sugu Emanuel Blasius Mdendemi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya |
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiangalia mwili jambazi lililouwawa na kikosi cha polisi Mbeya |
Baadhi ya polisi na waandishi wa habari wakiwa nje yajengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa Mbeya |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesha baadhi ya siraha alizokutwanazo jamabazi huyo aliyeuwawa |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesaha hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo kama kinga katika matukio yake |
Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari MTU mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya kurushiana risasi.
Jambazi huyo ni
miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa
akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba G 68 PC Jafari
yaliyotokea Februari 6, Mwaka huu katika eneo la Matundasi Wilayani
Chunya.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano
alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo
lilitokea jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia Machi 27,
Mwaka huu.
Kamanda Diwani alisema
kabla ya tukio majambazi wapatao wanne tayari walikuwa wameweka mawe
barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji katika eneo hilo la
Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya watu kuporwa mali zao.
Alisema Jeshi la
polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika kwa wakati kwa
kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego kwa kuwa majambazi
hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
Aliongeza kuwa baada
ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari kushambulia lakini
kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha kinyume chake wakaanza
kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi yakafanywa.
Diwani alisema katika
mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi kiunoni na ubavuni kulia na
wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo Marehemu alipowahishwa hospitali
kwa matibabu daktari alibaini kuwa amekwisha fariki.
Alisema jambazi
huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba AB huku namba nyingine
zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na mbili (22) pamoja
na mapanga mawili 2.
Aliongeza kuwa baada
ya Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo alikutwa na
kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius
Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa
makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
“Jambazi huyu
amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao wa majambazi
uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya Mikoa mbalimbali
ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika kushiriki katika tukio la
mauaji ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha Mkwajuni – Chunya tarehe
06.02.2013.” Alisema Kamanda Diwani.
Aliongeza kuwa
ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo pia
anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila
kuchelewa kwa jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi.
Pia
amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na
uhalifu kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli halali
kupata maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.
Picha na Mbeya yetu
............................................................................................................................
Greetings from JBG – Kibanda & Wife.
Hope all is well.
Salamu nyingi saaana toka JBG!
I could not resist! Yes I cried! But Absalom is the same person I knew last two months! Amesimama! Mungu ni Mwema!!!
Anaomba watanzania wamwombee na amesema anaendelea vizuri kwa sasa…
Cheers,
Hoyce Temu.
KINGO TANZANIA INAKUTAKIA KILA LA KHERI NA URUDI SALAMA NA KUENDELEA NA MAJUKUMU YAKO YA KILA SIKU YA KUIJENGA NCHI YETU YA TANZANIA BILA KUKATA TAMAA.
|
No comments:
Post a Comment