Halimashauri ya jiji la Mbeya kupitia
wakala wa ukusanyaji wa ushuru wa
mabango SIMAMIA imeyashusha mabango ya kampuni ya Vinywaji baridi ya Cocacola tawi la Mbeya kutokana na
kudaiwa zaidi ya shilingi milioni 102.
Hata hivyo kampuni hiyo iko hatiani kuburutwa mahakami kwa kushindwa kulipia gharama za
mabango ya matangazo yaliyowekwa
maeneo mbali mbali ya Jiji hilo .
Kampuni hiyo imeshindwa kulipia gharama za kuweka matangazo hayo kwa
kipindi cha mwaka wa fedha 2012 – 2013 ambapo deni limefikia Shilingi Milioni
102 ambazo walitakiwa kuzilipa kutokana na wingi wa mabango hayo.
Akithibitisha kudaiwa kwa kampuni
hiyoMkurugenzi wa Wakala wa
kukusanya ushuru wa mabango ya biashara na Hoteli Jiji la Mbeya Simamia Company Limited, Ndugu Aloyce Mrema amesema kampuni yake
inatekeleza sheria ya jiji ambayo inataka kila bango la tangazo linatakiwa
kulipiwa.
Amesema kutokana na Kampuni ya Cocacola
kushindwa kulipia mabango hayo kampuni ya Simamia imeamua kutoa mabango yote
yaliyondani ya Jiji la Mbeya ambapo alisema hatua itakayofuata ni kuifikisha
mahakamani kampuni hiyo kwa kushindwa kutekeleza agizo la Halmashauri ya Jiji.
Amesema kabla ya kuanza kutoa mabango
hayo wameshapeleka barua za kuwakumbusha
zaidi tatu lakini bado hawakuitikia wito wa kulipa mapema gharama hizo
zilizowataka hadi ifikapo Machi 18, Mwaka huu kutoa majibu au kulipia mabango
hayo.
Mrema amesema utaratibu wa kampuni hiyo
ni kuhakikisha kuwa kila kampuni iliyoweka bango la biashara katikati ya Jiji
la Mbeya inalipa gharama kwa mujibu wa Sheria za Jiji ambapo kwa takayeshindwa
kufanya hivyo atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Aidha ametoa wito kwa makampuni makubwa
kuheshimu sheria za nchi na siyo kukiuka kutokana na kuwa na fedha nyingi
ambapo aliongeza kuwa kwa sasa zaidi ya makampuni sita makubwa ya Jiji la Mbeya
yameshapewa barua za kuwakumbusha kulipia mabango hayo.
Hata hivyo ameyataja makampuni hayo kuwa
ni pamoja na makampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Vodacom, Airtel,Zantel, Tbl
na Pepsi ambayo yameshapewa barua za kuwakumbusha kulipia mabango hayo yakiwemo
makampuni ya watu binafsi.
Akizungumzia hatua hiyo Ofisa wa Cocacola
aliyejitambulisha kwa jina moja la Zekaria amesema hajui lolote kuhusu
kuondolewa kwa mabango ya kampuni yake na wakala wa Jiji Simamia ambapo amesema
atalifuatilia na kulipeleka kitengo kinachohusika kwa ajili ya kulitolea
taarifa.
Hata hivyo Ofisa huyo alionekana kukwepa
kutokuwa na taarifa juu ya kampuni hiyo kung’oa mabango ili hali baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo walionekana wakipiga picha na kufuatilia hatua zote
zilizokuwa zikifanyika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Haslmashauri ya Jiji la Mbeya Juma Iddi alipoulizwa juu ya utaratibu wa kampuni
hiyo wa kutoa mabango ya biashara ya kampuni ya Cocacola amesema hajui lolote
kwa sababu kampuni ya Simamia
ilishinda tenda ya kukusanya ushuru wa Hoteli na mabango ya biashara
hivyo yeye hana uwezo wa kuingilia.
Na Mbeya yetu
WATANZANIA
WENZETU WANAISHI NA KUTESEKA NA UGONJWA WA UKOMA MAKETE WILAYANI RUNGWE
WANAHITAJI MISAADA KWA JINSI MTU ATAKAVYOJISIKIA
| ||||||||||
BAADHI
YA WAGONJWA WA UKOMA WAKIWA WANASUBIRI KUPEWA MISAADA NA WASAMALIA WEMA
JUMUIYA YA AKINA MAMA UMOJA WA MAKANISA WILAYANI RUNGWE CCT
|
Monday, March 18, 2013
KAMPUNI YA SIMAMIA YASHUSHA MABANGO YA MATANGAZO YA KAMPUNI YA COCACOLA TAWI LA MBEYA KUTONANA NA KUDAIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 102
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment