NA BASHIR NKOROMO, DOGGUAN, CHINA
WATANZANIA wanaoshi nchini China wametakiwa kukiwa na mshikamano mkubwa na kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha tabia njema katika matendo kwa wenyeji wao.
Akizungumza na Wanajumuia ya
Watanzania wanaoishi China, baada ya kukutana nao katika mji wa
Dongguan, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema, wasipokuwa na
mshikamano na kuwaonyesha tabia njema wenyeji wao, Wataharibu sifa ya
Tanzania Kimataifa ambayo inafahamika kwamba ni nzuri kwa miaka mingi.
Kinana ambaye hupo nchini China na
ujumbe wa watu 14 kwa ajili ya ziara ya mafunzo katika nyanja
mbalimbali, alikutana na Watanzania hao, baada ya kuamua kumtembelea
katika hoteli ya Exhibition International hoteli, jana, Machi 12, 2013,
ili kumsalimia na kubalishana naye mawazo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
Watanzania hao walisema, wamekuwa wakiishi nchini China kwa mahusiano
mazuri kutokana na maadili waliyolelewa nayo ya Kitanzania, lakini hali
hiyo huenda ikaingia dosari kutokana na kuwepo Watanzania ‘feki’ ambao
wamekuwa wakiingia China kwa pasi za Tanzania na kufanya maovu.
“Hawa Watanazania bandia
wakiishaingia hapa hujitambulisha kuwa ni Watanzania, hata wakiulizwa
pasipoti ya Tanzania wanayo, lakini cha ajabu ukiwauliza wanakotoka
Tanzania wanababaika na hata lugha ya Kiswahili hawajui sawasawa.
Utamkuta mtu anajua kusalimia tu, anasema ‘mambo’ basi, sasa jamani kuna
Mtanzania ambaye hawezi kuzungumza kiswahili, lakini akawa na uwezo wa
kuja ugenini kama huku?” alisema Katibu wa Jumuia wa Watanzania hao
waishio China, David Chgamla.
Alisema, kutokana na hali hiyo,
Wachina sasa wameanza kupunguza imani yao kwa Watanzania kiasi kwamba
mtu anapojitambulisha kuwa ni mtanzania wakati akiihitaji huduma
anatazamwa mara mbili mbili kuthibitisha uaminifu wake.
Akizungumzia baadhi ya
Watanyabiashara kutapeliwa au kuziwa bidhaa zisizo na ubora au kwa bei
isiyo halali, Katibu huyo alisema, wengi wanakutana na mikasa hiyo kwa
sababu wanakifika China wanakwenda mahali ambapo siyo sahihi kwa
mahitaji yao na hivyo kutahamaki wakiingia hasara.
“Lakini Ndugu Kinana, Jumuia hii
tuliyounda hivi karibuni na kuwa na uongozi huu mpya, nina imani
itawasaaidia Watanzania wengi kutopoteza fedha au mali zao wanapokuwa
wamekuja hapa kibiashara, kwa sababu tunajipanga vema kuhakikisha kila
atakayekuwa anakuja akipenda anakutana na sisi kwa ajili ya msaada”,
alisema.
Uongozi wa Wanajumuia hiyo ya
Watanzania unaundwa na John Luhumbiza (Mwenyekiti), Abraham Merishani
(Makamu Mwenyekiti), David Chamla (Katibu Mkuu) na Msaidizi wake ni
Aboubakari Mwinyi.
WAKATI HUOHUO
CHINA YAITABIRIA TANZANIA KUPIGA HATUA
Mtumishi
katika mnara wa Canton, mrefu kuliko yote nchini China na watatu
duniani kwa urefu, Sarah Xie, akimuonyesha mandhari ya jiji la
Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na
ujumbe wake walipopanda hadi mwisho mnara huo wenye urefu wa zaidi ya
futi 100, Machi 13, 2013. Wengine Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya
Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine shigella. Kinana na
ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko
wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakitazama maumbo ya
mandhari ya mji wa Guanzhou, China, yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton
wenye urefu wa zaidi ya mita 100, walipotembelea mnara huo, Machi 13,
2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya
kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha
na Bashir Nkoromo).
Katibu
wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitazama
bidhaa zinazouzwa kwenye kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko
yote nchini China ukiwa na urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou,
China. Dk. Asha-Rose Migiro na Yusuf ni miongoni mwa viongozi
walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya
siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China
(CPC). (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi na wanachama wa Jumuia ya watanzania waishio nchini China
NA BASHIR NKOROMO, DONGGUAN,CHINA
CHAMA Cha Kikomunisti cha China
(CPC) kimeeleza matumaini yake kwamba upo uwezekano wa Tanzania kupiga
hatua kubwa kichumi kama inajikita kwa dhati katika kuzitumia rasilimali
ilizonazo ikiwemo ardhi.
Hayo yalisemwa Machi 13, 2013 na
Kamishna wa Maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),
jimbo la Donguan, China, Cuo Jian, wakati akizungumza na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, katika hoteli ya Exhibition
Internation mjini hapa.
Jian ambaye pia ni Meya wa jiji la
Donguan, alisema, Tanzania kama zilivyo nchi kadhaa za Afrika, inaweza
kupiga hatua kiuchumi ikiwekeza juhudi zake katika kuzitumia rasilimali
ilizonazo kwa kuwa rasilimali ndiyo msingi wa kwanza katika kuinua
uchumi wa nchi yoyote.
Alisema, anatambuwa kwamba
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye ardhi kubwa, hivyo haina budi
juhudi zake za kuinua uchumi kuzielekeza katika rasilimali hiyo
ikiitumia kwa kilimo cha kisasa, kujenga viwanda na vitegauchumi
mbalimbali ambavyo vitachochea kukua haraka kwa uchumi.
“Hata hivyo nawapongeza Tanzania,
kwa hatua mliyofikia sasa katika kukuza uchumi, asilimia sita ya GDP,
inaridhisha, la msingi serikali kuongeza juhudi na kuwahamasisha
wananchi kushiriki katika juhudi hizo”, alisema, Jian.
JELA MIAKA 35 KWA KUWAUA NDUGU ZAKE KWA KUWACHOMA MOTO
Na Venance Matinya, Mbeya
MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 Samsoni Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma mashtaka mbele ya jaji
wa mahakama hiyo Samwel Karua, Mwendesha mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole
alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha
195 (16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Ngole aliiambia Mahakama hiyo
kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huo majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku
ambapo alifika nyumbani kwa baba yake akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na
baadaye kuidondosha sigala hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
Aliwataja walioathirika na moto
uliokuwa umewashwa kutokana na sigala
aliyokuwa ameidondosha mtuhumiwa kuwa ni
Daniel Mwang’ombe, Anitha Richard, Salome Mwang’ombe,Jane Samson, Diana Samson,
Maria George na Cloud Samson.
Kutokana na kosa hilo mtuhumiwa
huyo alikiri kuhusika na kwamba aliua bila kukusudia ambapo alikiri kuwa akiwa
anavuta sigala alidondosha kipande hicho ambacho kilikuwa bado kinawaka moto.
Aidha Mwendesha huyo aliiambia
mahakama hiyo kuwa pamoja na mtuhumiwa kukiri kusababisha vifo bila kukusudia
mahakama impe adhabu kali kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu
hiyo Wakili wa upande wa utetezi Sambwee
Shitambala alisema Mahakama inatakiwa
kumwonea huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa kutokana nay eye kuwa miongoni mwa wafiwa.
Alisema mshtakiwa ameondokewa
na wazazi, watoto na mke katika ajali hiyo ambapo hakuhudhuria mazishi yao pia
amekaa muda mrefu akiwa mahabusu ambapo
amekaa kwa miaka mitatu na kuongeza kuwa mtuhumiwa ni kijana ambaye ni nguvu
kazi ya taifa hivyo hastahili kufungwa.
Hata hivyo kutokana na utetezi
huo Jaji Karua alisema kutokana na hali iliyojitokeza mtuhumiwa atatumikia
kifungo cha miaka mitano kwa kila tukio ambalo ni kusababisha vifo saba hivyo
jumla atatumikia miaka 35.
Tupige vita rushwa ya mapenzi-jali kile
Mhe. Jaji Engera Mmari Kileo, akizungumzia uzoefu wa Majaji Wanawake wa Tanzania katika kukabiliana na tatizo la matumizi mabaya ya mamlaka kudhalilisha kijinsia na kushawishi rushwa ya mapenzi ( sextortion) wakati Chama cha Majaji Wanawake- Tawi la Tanzania kilipoanda mkutano wa pembezoni ( side-event) sambamba na mkutano unaoendelea wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wanawake ( CSW). aliyekaa kati kati ya Jaji Kileo, na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi Ramadhan Mwinyi ni, Bw. John Hendra aliyewahi kuwa Mratibu wa UNDP nchini Tanzania, Bw. Hendra ndiye aliyekuwa mwendashaji wa mkutano huo, bado anakumbuka vizuri kiswahili, kwa sasa ni Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Sera na Mipango katika Taasisi ya UN- Women
Hatimae wakatoliki wapata papa mpya Francis 1
Kadinali Jorge Mario Bergoglio kutoka
Argentina ametangazwa kuwa Baba Mtakatifu mpya.
Askofu
Mkuu huyo wa Buenos Aires anaitwa Francis wa kwanza.
Miongoni
mwa kauli za kwanza kwa maelfu ya waumini waliokusanyika kwenye uwanja wa
mtakatifu Petro Papa mpya aliwataka waumini waungane naye katika
kumwombea Papa mstaafu Benedikt wa 16.
Hii
ni mara ya kwanza katika kipindi cha takriban karne moja kwa Baba Mtakatifu
kutoka nje ya bara la Ulaya.
Papa
Francis wa kwanza mwenye umri wa miaka 76 anachukua nafasi ya Benedikt wa
16 aliejiuzulu mwishoni uliopita.
Papa
Francis wa kwanza alichaguliwa katika siku ya pili baada ya kura kupigwa kwa mara
ya tano.
Rais
Obama alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza duniani kumpongeza Papa Francis
kwa moyo wa mkunjufu.
Uchaguzi
wa Francis wa kwanza umepongezwa pia na Rais wa Argentina Christina
Kirchner aliewahi kukwaruzana naye katika siku za nyuma juu ya
masuala kama ya mashoga.
Mnamo
mwaka wa 2010, Papa Francis wa kwanza aliziita ndoa za jinsia
sawa kuwa ni jaribio la kuuteketeza mpango wa Mwenyezi Mungu.
Sifa na utukufu tunamwachia mungu nami nimekuwa nafuatilia uchaguzi huu kwa mala ya kwanza nakweli yapaswa kuigwa na wengi mambo kufanyika kwa umakini na zaidi utakatifu wa Mungu maana nimeshuhudia chaguzi kadhaa za makanisa kunakuwa hakuna tofauti na chaguzi za siasa. Hii iwe somo kwa wanadinimbalimbali na wanasiasa.
TUMSIFU YESU KRISTO.......
KINGO 0752881456
WACHEZAJI 23 WAITWA TAIFA STARS KUIKABILI MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16
mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi
ya Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo
kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika
mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim,
wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka
huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa
Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula
(Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki
ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa
Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud
Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam),
Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank
Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco
(Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa
TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la
Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma
Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na
Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
No comments:
Post a Comment