Wednesday, March 13, 2013

UKUMBI WA STAREHE JIJINI MBEYA WATEKETEA KWA MOTO


MMILIKI WA BABZ LOUNGE SHADRACK MAKOMBE 


MNAMO TAREHE 12.03.2013 MAJIRA YA SAA 02:00HRS HUKO ENEO LA UHINDINI JIJI NA MKOA WA MBEYA. SHADRACK S/O MAKOMBE,MIAKA 32,MHEHE,BIASHARA MKAZI WA JACARANDA MBEYA, ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO CLUB YAKE IITWAYO BUBZ LOUNGE NA KUTEKETEZA VITI,LIGHTS,FRIDGE NA VYOMBO MBALIMBALI VYA MUZIKI . THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA NA MALI ILIYOOKOLEWA BADO KUJULIKANA. MOTO HUO ULIDHIBITIWA NA KUZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA IDARA YA ZIMA MOTO NA UOKOAJI, WANANCHI NA ASKARI POLISI. CHANZO KINACHUNGUZWA. HAKUNA MADHARA YA KIBANADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI YA KUJIEPUSHA NA MAJANGA YA MOTO.

Signed By,
[BARAKAEL MASAKI – SSP]
  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
  PICHA KWA HISANI YA C. MWAIPOPO
 
 

Sleiman Seif Omar awataka wanahabari kufanya utafiti wa kina kuhusu habari zao

DSC03417 
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
 Meneja wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar Suleiman Seif Omar ( Bin Seif) amewataka waandishi wa habari kufanya utafiti wa kina katika habari wanazoziandika kama zina ukweli na uhakika.
 Hayo aliyasema jana  wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali katika ukumbi wa Mansoon Hotel Vuga
 Alisema  waandishi wa habari wanapokuwa kazini wawe makini kuandika habari zinazozingatia maadili yote ya habari ikiwemo ukweli na uhakika.
 Alisema kuandika habari kwa kuzingatia vigezo hivyo kunamuwezesha mwandishi kuwa muadilifu na kujiamini katika kazi yake.
 Alisema Baraza la Habari Tanzania kazi yake ni kushajihisha waandishi wa habari na kuiwapa muongozo jinsi wa utafutaji wa habari na kuziandika  vyema ili ziwafikie wananchi wa  taifa hilo .
 “Kila mtu ana haki ya kupata habari ila habari hizo ziwe za ukweli na uhakika hivyo mwandishi nalazimika kuzifanyia utafiti wa kina habari anazozipata kabla ya kuziwasilisha kwa wananchi kupitia chombo cha habari”. Alisisitiza Bin Seif.
 Meneja huyo aliwaambia waandishi wa habari wawe watafiti wa habari na matukio ili kuziwasilisha kwa wananchi kama tukio hilo lilivyotokea.
 Nae mwandishi wa BBC Ali Saleh (Alibato ) alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kujifunza zaidi ili kuepukana na makosa ambayo hayastahiki kujitokeza na kuitia aibu fani hiyo.
 “Habari zipo lakini waandishi wa habari hakuna kutokazana na kutoweza kujifunza kusoma makala, vitabu pamoja kutosikiliza habari mbali mbali za ndani na nje ya nchi”. Alisema Ali Saleh.
 Nao waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walisema hakuna uhuru wa kutosha katika kutoa habari jambo ambalo linawajengea hofu na kutokujiamini katika kazi zao .
 Mkutano huo wa  siku moja kwa  Waandishi wa Habari umeandaliwa na Baraza la Habari Tanzania  (MCT) ambao umebeba mada Haki ya Kupata Habari
 

mkutano kuchagua papa (conclave) waanza vatican

Makadinali 115 leo wanaanza mchakato wa kupiga kura ya kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani katika ukumbi wa ndani  kwenye makao  makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.
Katika kipindi hiki cha sala hakuna Papa aliewahi kuchaguliwa baada ya kura ya kwanza kupigwa.
Makadinali hao watapiga kura za siri hadi mara nne kila siku mpaka Papa mpya atakapochaguliwa.


Post a Comment