Meya wa Jiji la Mbeya Ndugu Attanus Kapunga akiwaomba watulie ili awasikilize shida yao wamiliki na madereva wa magari ya biashara kuanzia tani moja |
Wamiliki na madereva wao wakiwa makini kumsikiliza meya wa jiji la mbeya |
Emmanuel Mbuza mmilikiwa Mbuzax Auction Mart & Court Brockers akiingia ukumbini hapo huku madereva na wamiliki wa maroli wakimtolea macho |
Moja ya wanasheria wa jiji la Mbeya Kaijage akielezea sheria inayotumika kukusanya ushuru huo wa maroli yanayofanya biashara katika jiji la Mbeya |
Mheshimiwa meya siku ytulipokuja ofisini kwako kukueleza juu ya huyu wakala wenu ukasema humtambui sasa leo nashangaa unasema unamtambua sasa tukueleweje hapo mweshimiwa meya unatuchanganya |
Kwa ujumla huyu wakala hatumwelewi tunamlipa hiyo kodi risiti anatupatia za malipo ya Taxi |
Emmanuel Mbuza akinyoosha mkono ili apatenae kuzungumza kidogo hapo ndipo palikuwa pangumu kelele zilitawala ukumbi mzima kutaka akae la sivyo hali ya hewa humo ukumbini itachafuka |
Naibu meya Fungo akijaribu kuwatuliza wamiliki hao wasiendelee na kelele jamani tumewaelewa Mbuza tunaomba ukae ili kikao kiendelee |
Jamaa wakiondoka kwa furaha kufuatia ushindi wa matatizo waliotoa kwa meya wa jiji la Mbeya |
HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya limelazimika kuifuta Sheria ndogo ya Halmashauri hiyo namba
376 (4)na (1) ya Mwaka 2011 iliyokuwa inataka kusajili magali ya kukodi,
teksi,Bajaji na Pikipiki kwa kulipia ushuru Shilingi 58,000/=kwa Mwaka.
Sheria
hiyo imefutwa baada ya kutokea
ugomvi mkubwa baina ya wamiliki na madereva wa magari kuanzia tani moja hadi
tano nne na wakala aliyepewa zabuni ya kukusanya ushuru huo.
Ushuru
unaolalamikiwa na wamiliki hao wa magari ni ule unaokusanywa na Halmashauri
hiyo kupitia kwa wakala aliyejulikana kwa jina la Mbuzax Auction Mart &
Court Brockers inayomilikiwa na Emmanuel Mbuza.
Wananchi
hao walitoa malalamiko hayo kwenye mkutano wapamoja kati ya wamiliki wa magari,
madereva na viongozi wa Halmashauri ya Jiji chini ya Meya uliofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri uliopo Sokomatola Jijini hapa.
Wakizungumza
kwenye mkutano huo Madereva hao wamesema utaratibu wa ushuru huo unawaumiza
sana kutokana na kuwa na gharama kubwa kama ushuru wa usajili kwa mwaka
Shilingi 58,000/= pamoja na ushuru wa kuegesha magari kila siku shilingi
1000/=.
Paulo
Mwasilelwa Dereva wa Pick up ambaye pia ni katibu wa Chama cha waendesha maroli
Jiji la Mbeya amesema wanapingana na ushuru huo ambao unatozwa unawaumiza kwa
sababu hulazimika kulipia gharama za usajili wa gari linaponunuliwa, bima ya
gari,Tra, maegesho na zimamoto ambavyo lazima vilipiwe.
Amesema
Kodi ya Maegesho ni zaidi ya Shilingi 360000 kwa mwaka hivyo ukiongeza na
ushuru wa usajili gari haliingizi fedha yoyote badala yake linadumaza uchumi wa
mwananchi wa kawaida ambapo aliongeza kuwa biashara ya magari hiyo haina
uhakika kutokana nakutokuwa na wateja wanaoeleweka badala yake wanasuburi
kukodishwa.
Wameongeza
kuwa utaratibu unaofanywa na wakala huyo ni mbovu ambao walidai kuwa wakala
huyo hutumia nguvu nyingi hali inayosababisha kuhatarisha maisha yao kutokana
na watumishi wa wakala huyo kutumia mapanga kuwatishia maderev pamoja na
kuwajeruhi.
Akijibu
tuhuma hizo Meya wa Jiji la Mbeya Ndugu
Attanus Kapunga aliyekuwa amefuatana na Kamati ya Fedha ya baraza la
madiwani wa Halmashauri hiyo alisema kutokana na sheria iliyokuwa imepitishwa
na madiwani hao kutotolewa elimu kwa wananchi wanaotakiwa kulipa kodi
inamakosa.
Kapunga
amesema kama sheria haileti amani baina ya wananchi inatakiwa iangaliwe upya
hivyo wakala anatakiwa kusimama mara moja ili Sheria hiyo iangaliwe upya kwa
maslahi ya maendeleo ya Jiji hilo.
Amesema
kitendo cha wakala huyo kukusanya ushuru kinyume na maeneo aliyoaambiwa ni kosa
kubwa ikiwa ni pamoja na kutumia ubavu kudai kodi ambayo Halmashauri haijamtuma
ni kinyume na taratibu alizopangiwa.
Ameongeza
kuwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye sheria hiyo lazima wakala
asimame asubiri vikao vikae upya na kuitazama upya ili isiwagombanishe na
wananchi hali itakayosababisha uvunjifu wa amani.
kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbuzax Emmanuel Mbuza ambaye awali
hakupewa nafasi ya kujitetea kutokana na madereva kumzomea pindi aliponyoosha
mkono akitaka kujitetea hadi mkutano unafungwa aliwaambia waandishi wa habari
kuwa anaishukuru Halmashauri hiyo kwa kugundua mapungufu ya sheria zao.
Mbuza
amesema kutokana na kuvunjwa na kufutwa kwa sheria hiyo kutampunguzia yeye
kufanya kazi katika mazingira magumu yanayosababisha kuwa na ugomvi na wananchi
wanaotakiwa kulipia ushuru huo.
Amesema
kilichofanyika ni Hlmashauri ya Jiji kugundua kuwa sheria iliyokuwa ikitumika
ilikuwa na mapungufu ambayo wakala asingeweza kuyajibu badala yake walipa kodi
walikuwa wakitoa lawama ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.
BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AWATAKA WAANDISHI WA HABARIWANAWAKE KUHAMASISHA AMANI KWA KALAMU ZAO
Na Mwanishi Wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Balozi Khamis Kagasheki amewataka waandishi wa Habari wa Kike kutumia
kalamu zao katika kuandika mambo yanayohamasisha amani na utulivu
nchini.
Pia aliwataka kutumia kalamu zao
katika kuandika na kuibua vitendo vya unyanyasaji na vya kikatili
wanavyofanyiwa wanawake nchini.
Hayo aliyasema hivi karibuni
jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Lamada , wakati wa uzinduzi wa
kikundi cha Habari Group kinachojumuisha waandishi mbalimbali wa habari
hapa nchini.
Alisema ni vyema wakatumia fursa
zao katika kufichua viashiria mbalimbali vya fujo kwa kuwa endapo
itatokea uvunjifu wa amani wanaoathirika zaidi ni wanawake na watoto.
Kikundi cha habari kinajihusisha
na ununuaji wa hisa, kukopeshana na kufanya miradi mbalimbali ya kikundi
na mmoja mmoja hivyo aliwataka wanakikundi kujibidiisha zaidi na
kuongeza wanachama wake.
“Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi
ni moja ya maadhimio 12 ya ulingo wa Belgin hivyo mnachofanya hapa ni
katika kujikwamua wenyewe kiuchumi na kama mnavyofahamu wanawake
wanamajukumu mengi katika familia na pia kutingwa na mambo mengi katika
tasnia yenu lakini mmethubutu kufanya hivyo hivyo endeleeni,”alisema
Kagasheki
Pia alitoa wito kwa wanawake kuhakikisha kuwa majukumu waliyonayo yasiwe kikwazo kwao kushiriki katika kukuza uchumi.
Alisema kinachotakiwa ni kuondoa
fikra kuwa haiwezekani na kuhakikisha wanapiga vita mambo
yanayomgandamiza mwanamke kwa kuondoa fikra kwamba haiwezekani
kujikwamua kiuchumi.
Naye mlezi wa kikundi hiko ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angella Kairuki alisema atakuwa
bega kwa bega na wanakikundi hiko katika kuhakikisha kuwa kinasonga
mbele.
“Nimefurahishwa sana na wazo la
wanahabari hawa na nina ahidi nitakuwa nao bega kwa bega katika
kuhakikisha kuwa kikundi kinakua zaidi na kuwatafutia fursa mbalimbali
za kukiendeleza pia,”alisema Kairuki.
UPOTEVU WA DAWA ZA KULEVYA
Sehemu ya mbele ya gari ikiwa imefunguliwa kwa uchunguzi zaidi
Picha chini :Askari polisi akilinda sehemu ya madawa ya kulevya yaliyotolewa kwenye gari hiyo
Baadhi ya maofisa hao ni kamanda wa kikosi cha upelelezi mkoani Mbeya (RCO) Elis Mwita, naibu RCO Jacob Kiangi na mkuu wa kikosi cha FFU Charles Kinyongo. Hii ni baada ya kupeleka sukari na chumvi kwa mkemia mkuu badala ya madawa ya kulevya KILO 1.9. Maafisa hao ni wa jeshi la polisi Mbeya; Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi, alisema katika kikao cha Maofisa na Makamishna wa polisi kilichoketi Dodoma havi karibuni waliazimia kuanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa askari wote watakaokwenda kinyume na kanuni na maadili ya jeshi hilo. Nchimbi aliwataja waliosimamishwa na kufunguliwa makosa ya kijeshi ni pamoja na Elis Mwita, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya, Jacob Kiango, Mrakibu msaidizi wa Polisi, aliyekuwa msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, na Charles Kinyongo mrakibu msaidizi wa Polisi ambaye alikuwa mkuu wa kikosi cha kutuza ghasia Mkoa wa Mbeya. Akizungumzaia mgogoro wa Ardhi kati ya mwekezaji na wanakijiji, Dk Nchimbi alimtaja Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Mtagi, kuwa amesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka ya kijeshi. “Mimi sipendi watu wafanye vurugu lakini napenda haki itendeke sasa katika hili askari hawa hawakufuata taratibu na walikuwa wanajua kuwa wananchi wale walifanyavile baada ya kufanya mkutano wa hadhara na kubaini kuwa mwekezaji yule hakuwa na haki ya kumiliki ardhi kiasi hekari 4000”alisema. Dk Nchimbi alisema wakati wananchi hao wakiwaswaga ng’ombe kuwapeleka kwa Mkuu wa wilaya, lakini wakiwa njiani walikamatwa na polisi, na wengine walikimbilia Dodoma kuonana na waziri mwenyewe. Alisema lakini wakiwa huko, alipigiwa simu na askari polisi kutoka Kagera na kuelezwa kuwa watu hao ni majambazi sugu, hata hivyo, Nchimbi aliomba akutane nao, baini kuwa wananchi hao hawajawahi kuwa majambazi hivyo walisingiziwa tuhuma hizo kwa makusudi. Kwa upande mwingine Dk Nchimbi alisema suala Kamishna Msaidizi Mwandamizi Renatus Chalamila, ambaye alikuwa anasimamia ajira za jeshi la polisi, anatuhumiwa kwa pamoja na maofisa wa polisi kujihusisha na vitendo kupokea rushwa na kuwaingiza vijana wengi katika Chuo cha polisi kilichopo Moshi, kinyume cha utaratibu. Nchimbi alisema kutokana na cheo chaka hicho mwenye madaraka ya kumfukuza kazi ni Rais hvyo taarifa hizo zomefikishwa kwenye mamlaka hiyo ambapo wakati wakisubiri maamuzi mengine wanawajibika kumpa likizo ya mwzi mmoja. |
No comments:
Post a Comment