MUONEKANO WA HARI YA HEWA LEO MJINI TUKUYU |
BAADA YA PILIKA PILIKA YA KILA SIKU LEO NILIKUWA NA MAPUMZIKO YA KUWA SHAMBANI KWANGU |
..............................................................................................................................
MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA KUPANDISHWA KIZIMBANI JUMATATU
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu
mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu kwenye chuo cha uhasibu
mwanzoni mwa wiki hii jijini hapa mbali na lema teyari jeshi la polisi
limewapandisha kizimbani watu 14 kwa kuthuma kama hizo.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi(ACP)
Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema atapandishwa kizimbani kujibu
tuhuma hizo kwenye mahakama ya wilaya siku ya jumatatu mkoani hapa.
Kamanda
Sabas alisema kuwa jeshi hilo lilifanikiwa kumtia nguvuni lema huko
nyumbani kwake Njiro majira ya 9 usiku wa kuamkia jana na anaendelea na
mahojiano na jeshi hilo na kuwa atafikishwa mahakamani siku hiyo.
Vurugu
hizo zilitokea juzi baada ya mwanafunzi mmoja Hendry Kagu 22 kuuwawa
kwa kuchomwa na kisu na watu wasiojulikana na kupoteza maisha ndipo
wanafunzi hao walianza kujikusanya kwa madai ya kujadili kifo cha
mwanzao na ndipo mbunge huyo alifika na kuanza kuwashawishi kwenda
ofisini kwa mkuu wa mkoa kwa maandamano lakini kabla ya kuanza
maandamano hayo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo alifika eneo la chuo cha
uhasibu kusikiliza tatizo hilo.
Hali
ya tafrani na kuzomea ilitawala eneo hilo ndipo baada ya Mulongo kufika
hali iliyoleta sintofahamu hadi rc Mulongo kundoka na ndipo askari wa
kikosi cha kutuliza fujo walipoamua kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na
hali kutulia na kisha mkuu wa mkoa kuamuru chuo hicho kufungwa kwa muda
usiojulikana hali iliyoleta simanzi kwa wanafunzi ambao walikuwa
wakijianda kufanya mitihani yao ya kumaliza chuoni hapo wiki inayokuja.
by John Bukuku
..............................................................................................................................
MTOTO OMBENI MBEULA AKOSA MATIBABU MIEZI MIWILI KWA KUTOKUWA NA PESA UONGOZI WA HOSPITAL WATAKA PESA KWANZA NDIPO APATE MATIBABU BAADA YA KUNGUA NA MOTO
Kiukweli inasikitisha sana kwa Madaktari wa HOSPITALI YA GENERAL iliyoko mjini Dodoma kutomtibu mtoto Ombeni Mbeula kwa takribani miezi miwili kwa ukosefu wa pesa kutoka kwa familia yake. Isitoshe mtoto mwenyewe ana miaka mitano (5) inabidi kiutaratibu apate matibabu bure, hivi kweli uongozi wa hospitali ya General umelisimamiaje jambo hili?. Kiukweli inasikitisha kwa madaktari kutomjali mtoto Ombeni Mbeula mpaka habari iliporushwa kwenye mtandao kupitia BLOG YA PAMOJAPURE na washiriki wake wa blog nyingine ndipo madaktari walipoanza kuitwa lakini hawajaenda kumtibu mtoto huyo.
Kwa moyo wa dhati tunawashukuru wale wote waliotoa michango yao kupitia kupitia kwenye namba ya ndugu yake ambayo ni Ekiria Paskali na namba yake ya simu ni 0757 498336
Hawa ni baadhi ya wale walioguswa na tukio hilo na kutoa mchango wao wa hali na mali
jumla ya michango ni shilingi 421,300 mpaka naondoka hospitalini hapo kuna watu walikuwa bado wanaendelea kuchangia. Kama ulikuwa unataka kumchangia mtoto huyu apate matibabu tuma mchango wako kwa kutumia namba hii 0757 498336 mwenye jina lake ni Ekiria Paskali.
HABARI NA MJENGWABLOG
............................................................................................................................
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi nchini kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika kutekeleza hatua za uhamaji wa urushaji wa matangazo kutoka Analojia kwenda Digitali.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakiwa makini kusikiliza |
Kizazi cha Digitali |
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
imewataka wananchi nchini kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mamlaka hiyo
katika kutekeleza hatua za uhamaji wa urushaji wa matangazo kutoka Analojia
kwenda Digitali.
Mwito huo ulitolewa na Afisa Uhusiano wa Tcra
Innocent Mungi wakati akizungumza na Vyombo vya Habari vya Mkoa wa Mbeya katika
Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mkapa, kuhusu zoezi la uzimaji
wa Mitambo ya Analojia katika Mkoa wa Mbeya.
Mungi alisema zoezi la uzimaji wa mitambo ya
utangazaji wa Televisheni ya mfumo wa Anaolojia ulianza kutekelezwa Disemba 31,
Mwaka jana katika Jiji la Dar Es Salaam kutokana na makubaliano ya nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwao
kutokana maandalizi ya kuzima mitambo hiyo katika Jiji la Mbeya kukamilika kwa
kuwashirikisha wananchi wa Vitongoji vyote ambapo mitambo hiyo itazimwa rasmi
Saa sita Usiku Aprili 30, Mwaka huu.
Afisa huyo alisema Elimu kwa umma kupitia mbinu
mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika Teknolojia ya mfumo wa Utangazaji
wa Digitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha.
Alisema matangazo ya Digitali ni mazuri kwa
sababu huwafikia watazamaji wengi zaidi kuliko Mfumo wa Analijia ambapo kati ya
Watazamaji wanaofikia asilimia 24 ni Asilimia 22 wanaofikiwa na matangazo hayo.
Kwa upande wake Mhandisi wa Maswala ya utangazaji
kutoka Mamlaka ya mawasiliano, Andrew Kisaka alisema katika Awamu ya kwanza ya
uzimaji wa mitambo hiyo itaishia katika Mkoa wa Mbeya.
Alisema hatua ya awamu ya pili itatangazwa
baadaye ambapo aliitaja mikoa ambayo imezimwa katika awamu ya kwanza kuwa ni
Dar Es Salaa (31/12/2012), Dodoma na Tanga(31/1/2013), Mwanza(28/2/2013), Moshi
na Arusha (31/3/2013) na Mbeya ambayo itazimwa mwishoni mwa mwezi huu.
Aliongeza kuwa baadhi ya vigezi ambavyo viliwekwa
na Serikali kabla ya kuanza kutekeleza suala hilo ni pamoja na Kuhakikisha kuwa
eneo linalozimwa lina huduma ya matangazo ya Digitali, Elimu kwa umma itolewe
kuhusu zoezi la uzimaji kabla ya utekelezaji.
Alivitaja vigezo vingine kuwa ni Kuendelea
kuonekana kwa Chaneli tano za Bure ambazo ni Tbc, Star Tv, Itv, Eatv na Capital
Televisheni, Uwepo wa Ving’amuzi vya kutosha katika eneo husika pamoja na
kupunguza makali ya bei
..................................................................................................................
DR.SLAA AWAKWAZA MBEYA, WAONDOKA MKUTANONI BAADA YA KUSEMA KUWA WANATAKIWA KUCHANGIA MSAFARA WAKE
DR.SLAA AKIINGIA JIJINI MBEYA
KUSHOTO NI MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA MBEYA JOHN MWAMBIGIJA AKIKUMBUSHWA JAMBO NA MSAIDIZI WAKE JUKWAANI... MMOJA WA VIONGOZI WA CHADEMA KUTOKA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI AKICHEKA BAADA YA KUONA WANANCHI WANAONDOKA UWANJANI HUKU NAYE AKIAMUA KUONDOKA... WANANCHI WAKIONDOKA UWANJANI BAADA YA KUAMBIWA WACHANGIE FEDHA. SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CAHADEMA) Freeman Mbowe kuwachangisha mamilioni ya fedha wakazi wa Jiji la Mbeya kwa lengo aliloeleza kuwa fedha hizo zingesaidia kununua maji ya kunawa wakiwa wanapambana na polisi ili kushinikiza Waziri wa Elimu ajiuzulu, kisha fedha hizo kutokomea kusikojulikana na maandamano kuyeyuka. Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Wilbroad Slaa katika viwanja vya CCM Ilomba Jijini hapa naye ameibuka na mbinu mpya ya kisayansi iliyoshitukiwa na wanananchi kisha kuamua kuondoka kabla ya mkutano kuisha alipowaambia kuwa wanatakiwa kuchanga fedha zingine kwa lengo la safari za wabunge waliopo kwenye msafara wake. Hali hiyo ikasababisha baadhi ya wananchi wakiwemo baadhi ya viongozi wa chama hicho kuamua kuondoka mkutanoni huku wakisema kuwa wamechoshwa kutapeliwa kisayansi. Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM) atakapowasili Mbeya kwa siku Nne kuanzia April 29- My 3 mwaka huu, bali afanye kazi za kiserikali. “Wakazi wa Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu. Sugu pia alitoa miezi mitatu kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha Soko Jipya la Mwanjelwa linakamilika ifikapo Julai mwaka huu. Alitishia iwapo kufikia muda huo halijakamilika yeye na wananchi wenzake watavamia soko hilo na kufanya kazi za ujenzi wenyewe. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa mjini), Ezekiel Wenje(Mwanza mjini) na Highness Kiwia wa Jimbo la Ilemela. Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Peter Msigwa alisema kuwa wamejipanga kufanya maamuzi magumu kama Spika wa Bunge, Anne Makinda ataendelea kuwapendelea wabunge wa CCM.
..............................................................................................................
|
No comments:
Post a Comment