MAANDAMANO YA WANANCHI ,WAFANYAKAZI NA WANAFUNZI YALIANZIA KATIKA OFISI ZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE NA KUELEKEA KATIKA VIWANJA VYA STANDI KUU YA MABASI TUKUYU MJINI |
KWA MUONEKANO HUU HII NDIO RUNGWE YA KIPINDI HIKI CHA MVUA ,BARIDI NA UKUNGU |
MAANDAMANO |
WIMBO WA TAIFA UKAIMBWA |
PAMOJA NA HARI YA HEWA KUWA MBAYA HASA BARIDI KALI ,UKUNGU NA MVUA LAKINI WANANCHI WA TUKUYU WALIVUMILIA |
KATIKATI RAS WA MKOA WA MBEYA AKISALIMIANA NA WATANZANIA WALIOJITOKEZA KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO WILAYANI RUNGWE |
UMAKINI NA UZALENDO WA WATANZANIA WAKATI WA KUIMBA WIMBO WA TAIFA LETU LA TANZANIA |
UMAKINI NA UZALENDO WA WATANZANIA WAKATI WA KUIMBA WIMBO WA TAIFA LETU LA TANZANIA |
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKITOA TAARIFA YA WILAYA KWA KIFUPI MBELE YA MKUU WA MKOA MBAYE NDIYE MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO HAYA YA MUUNGANO WILAYANI RUNGWE |
WANANCHI PAMOJA NA WANAFUNZI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA KWA MAKINI |
WAENDESHA PIKIPIKI WAKIPITA MBELE YA MGENI RASM NA KUMSINDIKIZA KUONDOKA UWANJANI HAPO KUELEKEA OFISI YA MKUU WA WILAYA BAADA YA KUMALIZA MAADHIMISHO YA MUUNGANO KATIKA VIWANJA VYA STAND TUKUYU |
MKUU WA MKOA AKIONDOKA OFINI KWA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE |
SHEREHE YA MUUNGANO KITAIFA
RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MUUNGANO UWANJA WA UHURU LEO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama
lililoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini
Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama
vya Siasa na Mabalozi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali ili
kushuhudia maadhimisho hayo.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akielekea jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho hayo
Rais
Dk. Jakaya Kikwete akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine kutoka
kulia ni Rais Mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa, Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange na Kutoka kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Wa
Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais
Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kulia akiwa na viongozi wengine
katika jukwaa kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd, Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akiingia uwanjani katika gari maalum huku akisindikizwa na Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo
kwenye uwanja wa Uhuru
Kikosi cha Jeshi la Ulinzi JWTZ wanamaji kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete .
Kikosi chamJeshi la Ulinzi JWTZ nchi kavu kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Watoto
wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya
Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika
maadhimisho hayo
..................................................................................................................................................................
MAHAFARI YA 36 YA STASHAHADA YA UALIMU CHUO CHA UALIMU TUKUYU YAFANA HUKU KATI WAHITIMU 491 MWANAFUNZI MMOJA TU NDIYE ALIYE SOMEA MASOMO YA SAYANSI YA KEMIA NA FIZIKIA HUKU WANNE WAKIOSOMEA HESABU NA FIZIKIA
MAZINGIRA YA CHUO CHA UALIMU TUKUYU |
WALIMU TARAJALI MWAKA 2013 |
WAKUFUNZI WA CHUO CHA UALIMU TUKUYU KILICHOPO MSASANI TUKUYU MJINI |
KUSHOTO MKUU WA CHUO CHA UALIMU MPUGUSO KILICHOPO TUKUYU MJINI |
MRATIBU TAARUMA WA CHUO CHA TUKUYU FRANK MBUNDA AKISOMA MAJINA YA WAHITIMU NA KUPITA KUCHUKUA VYETI HUKU KUSHOTO MAKAMU WA CHUO STEPHANO KILALE AKIWA MAKINI KUSIKILIZA KINACHOENDELEA |
MC WA MAHAFARI YA 36 YA CHUO CHA UALIMU AMBAYE PIA NI MKUFUNZI MWL SANGU |
HONGERENI SANA |
NA HAO WANNE TU WALIO SIMAMA NI KATI YA WAHITIMU 492 NDIO WALIOHITIMU MASOMO YA SAYANSI YA HESABU NA FIZIKIA |
KATI YA WAKUFUNZI WALIOPO CHUONI HAPO MKUFUNZI WALAONZIKU ALITUNUKIWA KUWA MFANYAKAZI BORA NA MCHAPA KAZI MAHIRI |
HAPA NI KUPONGEZANA |
HII NI MAHAFARI YA 36 TANGU CHUO CHA UALIMU KIANZISHWE MWAKA 1979NA KUPITIA KATIKA HATUA MBALIMBALI NA SASA CHUO KINATOA STASHAHADA YA UALIMU |
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana waliumbuana na kushutumiana wazi mbele ya Waziri Mkuu,
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana waliumbuana na kushutumiana wazi mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Hatua hiyo ilifikiwa katika kikao chao katika ukumbi wa Msekwa mjini hapa ambako waliumbuana na kushutumiana waziwazi. Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kilifanyika baada Spika wa Bunge, Anne Makinda kuahirisha mjadala wa makadirio ya mtumizi ya fedha ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2013/14.
Spika aliahirisha mjadala wa makadirio hiyo uliokuwa uhitimishwe jana, baada ya wabunge wengi kuonyesha nia ya kuyakwamisha kutokana na kutoridhishwa na jitihada za Serikali za kukabiliana na kero ya maji nchini.
Chanzo chetu kilichokuwa katika kikao hicho kilisema mjadala ulipoanza, Pinda aliizungumzia kwa kifupi Wizara ya Maji na kuonyesha jinsi Serikali ilivyokubali kwa dhati kurekebisha makadirio ya matumizi ya fedha ya wizara hiyo.
Baada ya hoja hiyo, chanzo hicho kilisema Waziri Mkuu aliwasilisha hoja nyingine iliyowataka wabunge wa CCM kuchangia posho zao za siku moja kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
“Hoja hiyo ilipopita, Nyoka wa Shaba (Kangi Lugora, Mbunge wa Mwibara), alisimama na kuhoji ni kwa nini chama kimekubali kusaidia uchaguzi wa madiwani wakati huwa hakisaidii kesi za uchaguzi za wabunge.
“Si unajua Nyoka wa Shaba naye ana kesi mahakamani, sasa ndiyo maana akaamua kuhoji iweje yeye hasaidiwi na chama wakati huo huo anaambiwa asaidie uchaguzi wa madiwani.
“Alipomaliza kusema hivyo, akasimama Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba. Aliposimama aliwashutumu moja kwa moja Lugora na Filikunjombe (Deo, Mbunge wa Ludewa).
“Akasema wabunge hao badala ya kuisaidia Serikali wanapokuwa bungeni, wao wamekuwa wakiishambulia jambo ambalo halileti picha nzuri kwa wananchi.
“Akasema kitendo cha Filikunjombe kusema bungeni kwamba Serikali ina miwani ya mbao hakikuwa kizuri… akasema ‘hawa wenzetu hatuko nao na kwa kuwa mwezi ujao tutaonana na Mwenyekiti wa Chama (Rais Jakaya Kikwete) nitasema mengi’.
“Alipomaliza kusema hayo akasimama Kibajaji (Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera). Kibajaji akaungana na Nkumba, akawashambulia Lugora na Filikunjombe kwamba wanaiua Serikali kutokana na maneno yao bungeni.
“Akasema kama Lugora ana kesi mahakamani ni bora akakabiliana nayo mwenyewe kwa sababu inaonekana hayuko pamoja na chama,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Baadaye alisimama Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima ambaye alimshutumu Lugora kwamba kitendo chake cha kuliambia Bunge kuwa kuna baadhi ya mawaziri wanajihusisha na dawa za kulevya, kinawaweka njia panda wananchi kwa kuwa wanahisi wabunge wao ambao ni mawaziri, nao wamo kwenye orodha hiyo ikizingatiwa kuwa hakuwataja majina.
“Pia, akahoji kama wabunge wana kero zao ni kwa nini wasiwafuate mawaziri na kuzungumza nao badala ya kuwasema bungeni.
“Kisha, alisimama Mangungu (Mbunge wa Kilwa Kaskazini) ambaye alionyesha wasiwasi juu ya majaji wanaosikiliza kesi za uchaguzi.
“Yeye akasema kesi nyingi za uchaguzi ambazo CCM inashindwa ni kwa sababu majaji wengi wanaichukia CCM na wanaipenda Chadema.
“Baadaye aliungwa mkono na Dk. Chami (Dk. Cyril Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini) ambaye alidiriki kumtaja jaji mmoja kwa jina kwamba ana upendeleo wa wazi wazi kwa Chadema.
“Kisha, alisimama Mbunge wa Karagwe (Gosbert Blandes) na akatoa ushauri kwamba kuna haja chama kusaidia majimbo ya uchaguzi na wakati huo huo, viongozi wakuu wa chama waende kwa wananchi kama wanavyofanya viongozi wa Chadema.”
Mbali na hao, chanzo hicho kilimtaja Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia kwamba alimshutumu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwamba hakusaidia wakati wa vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Mtwara.
“Ghasia alianza kwa kusema kwamba, siku hizi Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, anafanya ziara za mara kwa mara jimboni kwake Mtwara Vijijini lakini CCM haijali.
“Pia akamlalamikia Waziri Nchimbi kwamba wakati wa vurugu za wananchi mkoani Mtwara alimpigia simu lakini hakupokea na hata alipomtumia ujumbe mfupi wa simu hakumjibu.
“Akahoji pia kwamba iweje wakati wa vurugu zote Mtwara, nyumba zinazochomwa ni za wabunge wa CCM wanawake na nyumba za wabunge wanaume hazichomwi, akahoji kuna kitu gani hapo,” kilisema chanzo hicho.
................................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment