Wednesday, April 24, 2013

WANANCHI WA RUNGWE MKOANI MBEYA WAJIANDAA KUMPOKEA RAIS DR JAKAYA KIKWETE KWA FURAHA NA AMANI

ZIARA YA MKUU WA WILAYA  YA KUANGALIA NA KUKAGUA MIRADI ITAKAYOZINDULIWA NA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO DR JAKAYA KIKWETE ATAKAPO TEMBELEA WILAYA YA RUNGWE TAREHE 30.04. 2013 NA KUKAGUA SHUGHURI ZA MAENDELEO NA KUZINDUA MIRADI
UJENZI WA SIKIMU YA KAMBASEGELA UKIENDELEA

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIPATA MAELEKEZO UA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA KAMBASEHERA ULIOPO HALMASHAURI YA BUSOKELO

KIONGOZI WA KUSIMAMIA MRADI WA UJENZI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI KULIA AKIONGEA NA DAS MOSES MWIDETE AKIFUATIA NA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE WAKIPATA MAELEKEZO YA MWISHO KABLA ZIARA YA RAIS KIKWETE KUJA  KUZINDUA MRADI HUO UTAKAO KUWA NA MANUFAA KWA WAKULIMA WA RUNGWE

MKUU WA WILAYA  CHRISPIN MEELA ALIPATA WASAA WA KUONGEA NA KAMATI YA KATA YA KAMBASEGELA WAKIWA KATIKA MAANDALIZI YA KUMPOKEA RAIS DR JAKAYA KIKWETE ATAKAYE KUWA NA ZIARA WILAYANI RUNGWE NA KUZINDUA MRADI MKUBWA WA UMWAGILIAJI WA KAMBASEGELA NA KUONGEA NA WANANCHI WA RUNGWE KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA KKT KAMBASEGELA

MAANDALIZI YA KUPOKEA UGENI WA ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE HAPA NI KIKAO CHA KAMAKA KATA YA KAMBASEGELA WILAYANI RUNGWE

HAPA KATIKA UWANJA WA KANISA LA KKT USHARIKA WA  KAMBASEGELA NDIPO RAIS DR JAKAYA KIKWETE ATAPATA NAFASI YA KUONGEA NA WANANCHI WA WILAYA YA RUNGWE  . (NA HAPO MBELE YA KANISA UNAONA MAKABURI MAWILI YA MKE NA MUME MCHUNGAJI MWAIKENDA WALIOKUFA KWA AJALI YA PIKIPIKI NA KUGONGWA NA GALI TUKUYU MJINI WAKITOKEA KANISANI HAPA KIFO KILICHOWASIKITISHA WATU WENGI )

NIMEPITA LWANGWA AMBAPO NDIKO MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA BUSOKELO NA NI SIKU YA JUMATANO NI SIKU YA GULIO NIMEKUTA WATU WAKIENDELEA KUUZA NA KUNUNUA

KULIA NI JENGO LA KITUO CHA POLISI AMBACHO KINATARAJIWA KUBOMOLEWA NA KUJENGWA KITUO CHA POLISI CHENYE HADI YA WILAYA KUANZIA MWAKA HUU WA FEDHA 2013/2014
  

NIMEONANA NA RAFIKI YANGU SANA MR GABI MWASYEBULE SIKU HIZI ET ANAITWA DANDO WA BUSOKELO

HAPA NDIPO MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA BUSOKELO NA HII NDIYO ILIKUWA OFISI YA MBUNGE WA RUNGWE MASHARIKI PROF MARK MWANDOSYA NA SASA NIDIPO OFISI YA MKURUGENZI IMEANZIA KUFANYA KAZI NA KAZI ZINAKWENDA

OFISI ZA HALMASHAURI YA  BUSOKELO
.........................................................................................................
WANANCHI WA MWAKALELI WAPATA HOFU BAADA YA KUACHIWA WATU WAWILI WALIPIGIWA KULA YA KUHUSIKA NA MAUAJI WA WATOTO WALIOKUFA KWA KUKATWA VICHWA AMBAVYO MPAKA SASA HAVIJAPATIKANA
MKUU WA WILAYA AKIONGEA NA WANANCHI WA BONDE LA MWAKALELI KATA YA BUSOKELO
BAADHI YA WAZEE WA KIJIJI CHA ISANGE MWAKALELI WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA



WANANCHI WAKISIKILIZA KWA MAKINI

MKOA WA MBEYA KWA MAKANISA NDIO WENYEWE UNAOONGOZA LAKINI PIA NI HATARI KWA KUWA NA WAHARIFU WENGI LAKINI KABLA YA MKUTANO MKUU WA WILAYA ALITOA MWONGOZO KUWA TUOMBE AMANI YA MKUTANO KWA MUNGU WETU ALIYE HAI ILI MKUTANO UPATE UWEPO WA MUNGU NA MAJIBU YA KWELI YAPATIKANE ILI KUKOMESHA ROHO MBAYA ILIYOJITOKEZA YA MAUAJI

MKURUGENZI WA BUSOKELO IMELDA ISHUZA AKIONGEA NA WANANCHIPIA AMEWATAKA WANANCHI KUONYESHA USHIRIKIANO WA DHATI KWA VYOMBO VYA USALAMA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKEKWA WALIO HUSIKA

DAS WA WILAYA YA RUNGWE MOSES MWIDETE NAYE AKIONGEA NA WANANCHI WA MWAKALELI NAYE AMEWATAKA VIJANA KUTOLUBUNIWA NA WATU KUWA KUNA MAISHA YA MKATO YA KUJIPATIA KIPATO ZAIDI YA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA HARALI

AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA ISANGE BYASON NGULO AKITOA TAARIFA KWA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA ILI KUJUA NI HATHARI GANI ZIMETOKANA NA ROHO CHAFU ILIYOJITOKEZA YA MAUAJI KWA WATOTO WATATU NA WATU WAZIMA WAWILI
MTOTO AYUBU ALIYEUWAWA KWA KUKATWA KICHWA  HADI SASA KICHWA CHAKE HAKIJAPATIKANA
MTOTO LISTA ALIYE KATWA KICHWA NA HIVYO NI BAADHI YA VIUNGO VILIVYOPATIKANA BAADA YA SIKU 8 BAADA YA KUPOTEA KWA MUDA WOTE HUO SIKU YA 8 MBWA ALILEJEA NA MGUU MMOJA KIJIJINI NDIPO VIKAPATIKANA BAADHI YA VIUNGO
Photo: MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .
MTOTO DEBORA RIZIKI ALIYE ZIKWA NA BABA YAKE AKIWA HAI SEBURENI MWAO HUKU JUU YA KABURI AKIIWEKA MEZA NA KUIPAMBA VIRUZI
 NA TAREHE USIKU WA TAREHE 21 MTU MZIMA ALIUWAWA KWA KUPIGWA NA VITU VYENYE NCHA KALI NA WATU WASIOFAAMIKA KIJIJI CHA NDALA NA MWILI WAKE KUTUPWA SIKU HIYOHIYO MCHANA KIJANA WA MIAKA 27 ZUBERI KITENE ALIMUUA MAMA YAKE MZAZI GRESTA MWAKIGOMBE  KWA KUMPIGA NA MCHI WA SHOKA HADI KIFO KIKAMKUTA NYUMBANI KWAKE NA MTUHUMIWA AKIWA ANAKIMBIA ALIKAMATWA NA WANANCHI NA KUFIKISHWA KITUO CHA POLISI TUKUYU AKISUBIRI SHERIA KUCHUKUA MKONDOWAKE
MAMA ALIYE UWA WA NA MWANAE WA KUMZAA TUKIO LILILOTOKEA JANA TUKIO AMBALO SASA LINAWAFANYA WANANCHI WA MWAKALELI WAISHI KWA HOFU SANA WAKIHOFIA UZIMA WA MAISHA YAO

MAREHEMU MAMA GRESTA MWAKIGOMBE ALIYEUWAWA NA MTOTO WAKE WA KUMZAA
 BAADA YA MAELEZO YA MAJONZI YA MTENDAJI WA KIJIJI CHA ISANGE MWAKALELI LIKAIBUKA KUBWA KWANINI WANANCHI WALIPIGA KULA NA KUPATIKANA WATU WAWILI WANAOHISIWA KUWA NI WAHUSIKA NA KUPELEKWA POLISI LAKINI CHA AJABU WANANONA WATU HAO WAKO HURU WAMEACHIWA SASA HAPO CHINI MZEE AKIAMURU POLISI WAWALEJESHE WAO VIJANA WAWILI HAPO KIJIJINI KWAKUWA WALIWACHUKUA MIKONONI MWAO NA KWAKUWA WAMEONA HAWANA MAKOSA SASA WAWALEJESHE ILI WAO WATAJUA CHA KUFANYA
KATIKA MAADA HII AMANI IKAKOSEKANA KIDOGO MKUTANO KUINGIA KUTOELEWANA NDIPO MKUU WA WILAYA AKAOMBA JESHI LA POLISI KUELEZA KILICHOJILI HADI WATU WAWILI WAACHIWE HURUKUTOKANA NA MAUAJI YA WATOTO MWAKALELI

SSP SILVESTA IBRAHIMU OCD WA RUNGWE AKITOA MAELEZO KWA WANANCHI WA MWAKALELI KWA NINI WAMEACHIWA WATU WAWILI WALIOPIGIWA KULA NA WANANCHI NA OCD AKASEMA USHIRIKIANO WA USHAHIDI WA WANANCHI NI MDOGO AMBAO NDIO UNAFANYA WATU HAO WAKOSE USHAHIDI WA KUWAPELEKA MAHAKAMANI HIVYO HAO WATU HAWAJAACHIWA HURU ILI KWAKUWA KILA MTU ANA HAKI MBELE YA SHERIA BASI WAMEONA WAPEWE DHAMANA HUKU WAKIWA WANALIRIPOTI KITUO CHA POLISI

BAADA YA MAELEZO YA OCD WANANCHI HAWAKURIDHISHWA KABISA NA MVUA IKAANZA KUNYESHA NDIPO MKUTANO UKAHAMIA NDANI NA WANANCHI KWA BUSARA YA MKUU WA WILAYA  CHRISPIN MEELA  WAKAPEWA NAFASI YA KUONGEA WALIYONAYO NA MKUU WA WILAYA KUJIONEA UKUBWA WA TATIZO AMBALO ALILITOLEA MAELEKEZO NA MAAGIZO YA KUFANYA
 

"NAAGIZA KUWA KWAKUWA POLISI MMEWAACHIA WATUHUMIWA BILA YA KUWAHUSISHA WANANCHI SASA NAAGIZA HAO WATU WAWILI WAKAMATWE MALA MOJA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA" MKUU WA WILAYA AMBAYE NI MWENYEKITII WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA AMESEMA

WANANCHI WA MWAKALELI WAMEAMUA KUWEKA ULIZI KATIKA MAENEO YAO HUKU WATU WASIWE WANATEMBEA PEKE YAO NA WATOTO WASINDIKIZWE KILA WAENDAPO SHULE NA WATOTO WASIENDE KUCHUNGA MIFUGO POLINI

NIKASHUHUDIA WATOTO WAKICHEZA MAJUMBANI MWAO HAWATAKIWA KUWA MBALI NA WAZAZI WAO

MKUTANO UKAISHA KWA AMANI HUKU MAAGIZO MENGINE YAKIWA WANANCHI WA MWAKALELI WAJIANDAE KUSHIRIKI MAFUNZO YA MGAMBO YATAKAYOENDESHWA KATIKA KIJIJI CHA ISANGE MWAKALELI
    
RUNGWE
......................................................................................................................................................................

HAKI YA NANI VILE, WANANCHI MBOZI WALIZWA NA MBOLEA FEKI

 Sehemu ya Mifuko ya Mbolea kimeo ikisogezwa pembeni na vijana wa kazi baada ya kufunguliwa kwa dula la Mbolea la STACO LTD na kusafishwa kwamba mbolea nyingine haina matatizo
 Mbolea yenye alama ya kampuni ya YALA aina ya DAP ambayo pia imekutwa ikiwa chini ya kiwango

ofisa wa Upelelezi Mbozi akionyesha sehemu ya Mbolea mbovu ambayo imefumbiwa macho na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania na kuitakatisha kama haina matatizo wala madhara kwa wakulima
Katika hali inayoonyesha kuna mchezo mchafu wa kuendelea kuwamaliza wakulima wilayani Mbozi, shehena ya Mbolea mbovu iliyozuiwa  kuuzwa mwaka jana hatimaye “upepo umepita” na kuruhusu iendelee kuuzwa kwamba ipo juu kiviwango!
Katika hali hiyo wakulima wamekuja juu jana wakati wakishuhudia ufunguzi wa duka la STACCO ambalo miezi kadhaa lilishuhudiwa likiwa limepigwa makufuli na kwa mbwembwe nyingi ikiwemo msururu wa vyombo vya habari, lakini kwa jana ilikuwa kimya kimya kufuli la kwanza likafunguliwa, likafuata la pili na hatimaye la tatu!
Wakati wananchi kwa macho yao meupe wakishuhudia mifuko iliyoganda ya Mbolea za UREA, DAP, CAN na SA taarifa iliyotolewa kuruhusu kufunguliwa kwa duka hilo inatoa maelezo kuwa ni Mbolea ya SA peke yake  ndiyo iliyobainika kuwa na ubora hafifu! ambayo ni mifuko 11 tu.
Hata hivyo afisa anayesimamia ubora wa Mbolea katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi Bi Shonyela amesema licha ya maelekezo kutoka juu mengine hayatatekelezeka kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwamaliza wakuliwa wa wilaya yake kwakuzingatia kuwa Mbolea iliyoganda kuto kufaa tena mashambani.
“nimeandikiwa Mbolea aina ya SA pekee ndiyo isafirishwe chini ya usimamizi wa polisi kwenda Dar es Salaam lakini ni mifuko 11tu! Wakati kuna mbolea aina nyingine ambazo ni zaidi ya mifuko 50 hazina viwango vya ubora na taarifa imekuwa kimya” alifafanua
Uchunguzi wa haraka kwenye duka hilo unaonyesha kuwa mifuko16 ya DAP ilikuwa imeganda wakati wa kufunga duka hilo mwezi September mwaka jana, UREA mifuko 16, CAN 11 na SA 11.
Ingawa katika maelezo ya mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA ilionyesha kuwa wangeshirikiana bega kwa bega na TBS katika kuhakikisha viwango vya bidhaa hiyo vinasimamiwa, maamuzi ya kuruhusu uuzwaji wa mbolea aina ya DAP, CAN na UREA iliyoharibika kwenye ghala la STACO wilayani Mbozi yanajenga mawimbi na mashaka kwa wananchi kuwa mamlaka imelainishwa na ama wamefumbishwa macho!
Tanzania hutegemea maabara yake ya Mbolea iliyopo Mlingano mkoani Tanga kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo hata hivyo kumekuwepo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya maofisa wa serikali na kuwasaliti wakulima kutokana na makampuni yanayofanya shughuli za usambazaji wa pembejeo na hasa Mbolea kushika keki kubwa katika mzunguko wa fedha nchini
Wakati pia chuo cha kilimo SUA kimekuwa kikitumika katika tafiti na uchunguzi wa Mbolea, mwaka jana Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika Dr Adam Malima alikataa matokeo ya uchunguzi wa mbolea yaliyotolewa na SUA na kuahidi sampuli za Mbolea iliyokamatwa RUVUMA kupelekwa nchini Afrika kusini kujiridhisha na uchuguzi wa maabara za huko baada ya kulalamikiwa na wakulima
Aidha naibu waziri alisitisha leseni za makampuni ya STACO na Mohamed Enterpries mnamo August 07 mwaka jana, ambapo baada ya siku kadhaa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania Suzana Ikelya alitua Mbozi na kukamata Mbolea kwenye duka la STACO
“Maamuzi ya mamlaka ya ukaguzi wa ubora wa Mbolea yanawaacha wananchi wilayani Mbozi wakikosa imani kutokana na namna maamuzi yanavyofikiwa hata katika mambo ambayo hayahitaji utaalamu kuthibitisha ubora kama suala la Mbolea iliyoganda” anaeleza bwana Keneth Mwazembe mmoja wa wakulima wakubwa wilayani Mbozi.
Msimamizi wa duka la STACO bwana Julius Masai licha ya kufurahia kufunguliwa kwa ofisi yake ya chakula, amesema ni kweli kwamba kuna mbolea ambayo haimo kwenye barua ya kuruhusu uuzwaji ambayo haifai kwa matumizi lakini wanatumia busara kuitenga licha ya kutoelezwa kwenye barua hiyo
Ni kweli kuna mifuko kama 37 hivi ya mbolea mchanganyiko ambayo ni mbovu na tumeitenga pembeni na hatutaiuza” alisema meneja huyo bwana Julius Masai
Duka hilo limefunguliwa jana chini ya usimamizi wa maofisa wawili wa idara ya upelelezi ya jeshi la polisi na ofisa anayesimamia ubora wa MBOLEA wilaya ya Mbozi, na shughuli hiyo imefanyika kimya kimya tofauti na mbwembwe zilizofanyika wakati wa kufunga duka hilo ambapo wananchi waliokuwa wakipita barabarani waliitwa kushuhudia namna wanavyotendwa!
Kwahisani ya Indaba Africa
................................................................................................................................
 

Mary Mwanjelwa: Kuwa Mbunge wa viti maalumu siyo kubweteka




Kumekuwa na dhana kwamba, Wabunge wa viti maalum ambao hutokana na vyama vya siasa, hawawajibiki moja kwa moja kwa wananchi.
Hata hivyo, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Dk Mary Mwanjelwa anasema kuwa, nafasi hiyo inamweka moja kwa moja katika kuwatumikia wananchi kama walivyo wabunge.
Akizungumza hivi karibuni wakati wa kukagua miradi ya maendeleo mkoani, amesema kuwa anawajibika kuisaidia jamii katika sekta za elimu, afya na maendeleo ya jamii.
“Nitahakikisha najiotolewa kwa nguvu zangu zote nikishirikiana na wananchi bila kubagua makundi ya walemavu, vijana, watoto, wajane, wajawazito, yatima. Vilevile nitaboresha sekta ya elimu katika kuwepo kwa madarasa ya kutosha, uhakika wa upatikanaji wa vitabu,”
Dk Mwanjelwa anasema hatajali itikadi za vyama na udini katika kuwatumikia wananchi wa mkoa huo kwani wajibu wake kama mbunge ni kunoa makali katika kusaidia jamii.
Anasema katika kipindi cha miaka mitatu yaani tangu mwaka 2011 hadi 2013 mfululizo amechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Itagano, ujenzi wa mabweni ya wasichana na vitanda 16 na kutoa misaada mbalimbali katika kukabiliana na ukosefu wa miundombinu ya shule.
Mwanjelwa anasema kuwa mbali na kujikita katika sekta ya elimu pia amejitoa kusomesha watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi 10 na kugawa sare za shule kwa watoto 300 katika wilaya za Mkoa wa Mbeya ili kuwaandalia maisha bora ya baadaye.
Anasema kuwa katika uongozi na kama kiongozi ninapaswa na kutambua jukumu langu kwa wananchi wangu hususan kuhakikisha tunatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama wajane ili waweze kuanzisha miradi endelevu katika kujikwamua kiuchumi miongoni mwao.
“Kwa kweli jamii ina changamoto kubwa ambayo kama viongozi tunapaswa kubeba jukumu hilo kwa kuangalia pale tunapoweza katika kuhakikisha tunaboresha huduma za kijamii katika nyanja mbalimbali nchini bila kuangalia jinsia,”
Kwa upande wa afya, anasema kwa kipindi cha mwaka 2012 ametoa misaada ya magodoro 300 katika hosptali za wazazi katika wilaya za mbeya hususan katika wodi ya wazazi ya hosptali ya rufaa ya Meta kwa lengo la kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaolazwa na kusubiri kujifungua.
“Nikiwa kama mwanamke ninapaswa kulenga maeneo yaliyo na changamoto kubwa kwani tuliangalia katika hospitali ya Meta ambapo kulikuwa na changamoto ya muda mrefu ya upungufu wa vitanda na magodoro hali iliyokuwa ikipelekea wagonjwa wawili kulala kitanda kimoja,” anasema.
Mwanjelwa anaziita kuwa changamoto wanazokabiliana viongozi katika jamii.
Kuhusu maendeleo ya jamii, anasema kuwa katika kuhakikisha wanawake wanaachana na utegemezi ametoa mashine za kutotolea vifaranga vya kuku katika wilaya nane za jiji la Mbeya na kuhamasisha kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali.
“Licha ya kutoa mashine hizo nimetoa mitaji ya kuanzishia katika vikundi (saccos) za wanawake ili kuwajengea misingi imara ya usimamizi wa miradi na kujiwamua kiuchumi pindi miradi hiyo inapokuwa endelevu,” anasema na kuongeza:
“Kinamama wakiwezeshwa wanaweza hivyo ni jukumu letu kusimamia miradi wanayoanzisha kiuchumi ili kuweza kusaidia familia zao kielimu, afya na jamii ili waache kuwa tegemezi katika familia.”
Kuhusu elimu ya viongozi, Dk Mwanjelwa anasema ili kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa rasilimali, ameanzisha semina kwa madiwani katika halmashauri zote kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji kazi kwa wananchi na kutambua na kuchanganua changamoto zinazoikabili jamii kwa kuzingatia demokrasia, utawala bora na uwajibikaji
Chanzo Mwananchi
..............................................................................................................................
 

Wito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala ya kukubali kupandikizwa chuki na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa na Taifa kwa ujumla.




Wito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala  ya kukubali kupandikizwa chuki  na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa  na Taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa  Scourt Mkoa wa mbeya Ndugu Pablo Sanga akizungumza na waandishi wa habari jijini humo amesema kuwa kuna kila sababu ya wananchi mkoani humo kuilinda amani ya mkoa huo ilikuvutia shughuli za kimaaendeleo .

Amesema katika kipindi cha hivi karibuni  kumekuwepo na matukio mbalimbali yanayoashiria kuvuruga amani ya mkoa huo hivyo nivema wananchi wa mkoa huo wakawa makini na baadhi ya watu wanaopandikiza chuki  zidi ya viongozi wao na serikali yao kwa ujumla.

Pablo amesema siasa chafu zinazo enezwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini ndizo zitakazo weza kusababisha madhara ambayo ndiyo yatakayo changia kuvuruga kwa amani ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.
Kauli hiyo ya kiongozi wa scourt mkoani humo imekuja kufuatia kuwepo kwa ujio wa kiongozi wa kitaifa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kufanya ziara ikiwa ni pamoja na kuzungumza katika sherehe ya mei mosi kitaifa ambayo itafanyika mkoani hapa.

Hata hivyo Kiongozi huyo wa Scourt amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanampokea vyema Raisi Kikwete katika kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anafanya ziara yake  kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa vitendo viovu.
............................................................................................................................

  JK ,AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA KIKRISTO


zz 27152
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam2 4ae245 91442
.......................................................................................................................

WATANZANIA 342 WANUFAIKA NA UFADHILI WA MASOMO NJE YA NCHI KWA KUANZIA 2010

1Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Philipo Augustino Mulugo
Na Benedict Liwenga, Maelezo, Dodoma.

Jumla ya Watanzania 342 wamepata fursa ya kusoma masomo mbalimbali nje ya Tanzania  kati ya mwaka 2010 hadi 2012. Kauli hiyi imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Philipo Augustino Mulugo wakati akijibu swali la

Mbunge wa Jimbo la Gando, Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa aliyetaka kujua ni vijana wangapi wamepata nafasi za masomo nje ya nchi kuanzia mwaka 2010-2012 na ni vijana wangapi kutoka Zanzibar pamoja na nchi gani walikwenda kusoma.

 Mhe. Mulugo amesema kuwa katika kuwapatia ufadhili unaotolewa na vijana wanashindanishwa kwa kutumia vigezo vya kitaaluma, umri na uraia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Aidha, ameongeza kuwa kinachozingatiwa zaidi ni kigezo cha kitaaluma, mwombaji yoyote anayetimiza kigezo hicho anayo haki ya kunufaika na ufadhili bila kujali anatokea sehemu gani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe.Mulugo amebainisha kuwa kutokana na mwingiliano wa wananchi wa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa vigumu kutofautisha sehemu ya Jamhuri alipotokea muombaji.
 “Napenda kusisitiza kuwa nafasi za masomo zinatolewa kwa ajili ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba wote wanashindanishwa kwa vigezo vya kitaaluma na si vinginevyo.

 Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012, nchi ambazo zimekuwa zikitoa nafasi za masomo kwa Watanzania nje ya nchi ni Cuba, Algeria, Urusi, Msumbiji,Serbia, Uingereza, Misri, Korea Kusini, Macedonia, Uturuki, China, Ujerumani na Oman.
.............................................................................................................

No comments: