Na John Bukuku, Morogoro
HAKIKA kwa muda mrefu Chama Cha Mapinduzi(CCM), kimekuwa kikijaribu kujiweka katika mazingira mazuri zaidi kisiasa.
HAKIKA kwa muda mrefu Chama Cha Mapinduzi(CCM), kimekuwa kikijaribu kujiweka katika mazingira mazuri zaidi kisiasa.
Hata hivyo licha ya kufanikiwa kwa
kiwango fulani lakini bado kuna maeneo ambayo yamekuwa kikwazo cha CCM
kushindwa kutimiza lengo lake.
Ni wazi mzimu ambao unaimaliza CCM
hivi sasa ni hili la baadhi ya watendaji wa Serikali kwa ngazi
mbalimbali kuonekana kikwazo cha utekelezwaji wa Ilani ya chama hicho
ambayo inataka maisha bora kwa wananchi wake.
Utafunwaji wa fedha za umma
umekuwa mkubwa katika nchi hii hali inayofanya katika halmashauri
mbalimbali Tanzania kujikuta ikishindwa kufanikisha maendeleo.Kisa kuna
kundi la watu ambalo lipo ndani ya Serikali kwa ajili ya kukwamisha
juhudi za CCM katika kufikisha maendeleo kwa watu.
Moja ya malalamiko ya Wana-CCM
katika maeneo mbalimbali ya nchini ni hili la ubadhirifu wa fedha ambazo
zinatolewa na Serikal Kuu na kwenda kwenye halmashauri kwa ajili ya
kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo ndio imeunda Serikali.
Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), Abdulrahaman kuanzia Aprili 14 hadi Aprili 21(Jumapili) ,
alikuwa akifanya ziara katika Mkoa wa Morogororo ambapo amezunguka
katika wilaya zote za mkoa huo.
Moja ya kero kubwa aliyokutana
nayo ni hii ya fedha za umma kuliwa na baadhi ya wajanja wachache ambao
hawaitakii mema CCM kwa kuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo.
Kinana anaonesha wazi
kutofurahishwa na hali hiyo ambayo inafanywa na watendaji wasiokuwa
waamini ambao wao wanachojua ni kufanya ubadhirifu wa fedha za umma
ambapo katika hilo anatoa agizo kwa viongozi wa CCM kuwa makini nao na
kufuatilia karibu.
Kwa lugha harisi Kinana anataka
Wana-CCM kwa ngazi mbalimbali kuibana Serikali pale ambapo watendaji wao
wanaonekana kufanya mambo kinyume na Ilani ya uchaguzi inayozungumzia
maendeleo ya watu.
Akiwa katika wilaya ya Mvomero
wakati wa ziara yake,Kinana anakutana na malalamiko makubwa ya wana-CCM
wakiwamo madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambao wamechoshwa na
ubadhirifu wa fedha uliofanywa na moja ya watendaji wa halmashauri.
Wanachama hao wanakwenda mbali
zaidi na kuamua kumueleza Kinana kuwa kwa hali iliyofikia na namna
ambavyo mtendaji huyo analindwa licha ya kula fedha za umma huenda
analindwa na watu waliowaita ‘Wakubwa’.
Kutokana na hali hiyo Kinana
anaamua kutoa agizo la kuhakikisha wabadhirifu wa fedha za umma wakiwemo
waliohusika kutafuna fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero zaidi ya
sh.bilioni moja wanachukuliwa hatua.
“Hatutakubali kuona baadhi ya
watendaji wanashindwa kutekeleza majukumu yao.Kazi yao imebaki
kukwamisha utekelezaji wa ilani ya chama changu.
Hatuwezi kukaa kimya, tutaibana
Serikali na pale ambapo tutaona ufumbuzi wake unahitaji mjadala wa kina
tutakwenda kuzungumza haya kwenye Kamati Kuu ya CCM ili kupata ufumbuzi
wake,”anasema.
Mbali ya Kinana kutofurahishwa na
watendaji wa Serikali ambao wanakwamisha maendeleo ya wananchi kwa kula
fedha, anatumia nafasi hiyo kuwageukia viongozi wa CCM ambao nao
wanashindwa kusimamia majukumu yao.
Anasema katika maeneo ambayo
amepita katika ziara yake yapo mambo mengi yanayolalamikiwa lakini la
viongozi wa CCM kutowajibika ipasavyo nalo ni tatizo lingine kwa chama
na lazima hatua madhubuti zichukuliwe kurudisha heshima ya chama .
Kwa mazingira hayo ili CCM
kupambana na mzimu huo unaokwamisha kasi ya maendeleo ni wakati muafaka
kwa Wana-CCM kutofumbia macho madhambi yanayofanywa na baadhi ya
watendaji wa Serikali.
Ni jambo baya sana wakati CCM
inataka kutatua kero za wananchi lakini kuna kundi ambalo lipo kwa ajili
ya kukwamisha kasi hiyo ya kimaendeleo.Inasikitisha na kama Mtanzania
nina haki ya kutoa maoni yangu kwa mustakabali wa taifa langu.
MUONEKANO WA MJI WA KATUMBA NA KIWANDA CHA CHAI CHA WATCO |
WANANCHI WA TUKUYU WAKIWA SOKONI KUUZA NA KUNUNUA SOKONI TANDALE MJINI TUKUYU |
KAZI NI KAZI |
BAADHI YA MAGARI YAKIPAKIA NDIZI NA MAPARACHICHI NA MAZAO MENGINE TAYARI KWA KUSAFIRISHA KWENDA MASOKO YA NJE YA MKOA HASA DSM |
UGALI TAYARI BADO MBOGA TU KARIBUNI KIJIWE CHA MR NGENYILE MAENEO YA SOKONI TANDALE |
WATEJA WANATAFUTWA |
"KUPENDA SIO KAZI" NAMI NIMESOMA HAPO, |
BAADA YA GALI KUJAZA LAZIMA HONDACTA WA GALI ATOE PESA KWA WAPIGA DEBE HAPO SASA LAZIMA KIELEWEKE |
JENGO LA OFISI YA BONDE LA MAJI NYANDA ZA JUU KUSINI MJINI TUKUYU |
WATEJA WA KUNUNUA MBAO WAKISUBIRIWA |
DARAJA LA MUNGU LILIOPO MTO KIWIRA TUKUYU WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA |
MAPOROMOKO YA MAJI KAPOLOGWE MJINI TUKUYU WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA |
ZIWA NGOSI LILILOPO JUU YA SAFU ZA MILIMA YA ISONGOLE MAJI YASIYOPUNGUA WALA KUONGEZEKA NA HAMNA MAJI YANAPOINGILIA WA KUTOKEA |
MWAKA 2007 NIKIWA JUU YA SAFU ZA MILIMA RUNGWE AMBAPO LIPO ZIWA NGOSI LILILOPO WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA |
HAYA NI MAJI YA MTO KIWIRA YAKIFIKA HAPA MAJI YOTE YANAINGIA KATIKA JABARI LA MVILINGO MFANO WA CHUNGU WENYEJI WANAPAITA KIJUNGU |
TEMBEA UJIONEE MAAJABU YA MUNGU KATIKA UUMBAJI WAKE |
No comments:
Post a Comment