Monday, April 1, 2013

MTOTO AYUBU MWAKALENGELA MIAKA SITA AUAWAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA WAUAJI HAO KUONDOKA NA KICHWA TUKIO LIMETOKEA KIJIJI CHA IJOKA MWAKALELI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA. MMOJA WA WAUAJI AMEKAMATWA NA WANAKIJIJI HAO NA WAMEMPIGA NA KUMCHOMA MOTO HADI KUFA

BAADHI YA WAZAZI WA MAREHEM MTOTO AYUBU MWAKALENGELA
AGENI NGALELE BABA MZAZI WA MTOTO MAREHEM AYUBU MWAKALENGELA
MWILI WA MAREMEMU MTOTO AYUBU UKIWA KATIKA JOKOFU LA KUHIFADHIA MAITI
MWILI WA MAREHEMU AYUBU UKIWA HAUNA KICHWA BAADA YA KUUWAWA NA KUCHUKULIWA KICHWA
DR STAPHORD JOHN  KULIA AKIWA NA WAHUDUMU WA MOCHWALI YA TUKUYU WAKIFANYA UCHUNGUZI

BAADA YA UCHUNGUZI WA KINA DR STAPHORD AMESEMA KUWA WAUAJI WAMETUMIA KITU CHA NCHA KALI KUKATA KICHWA NA VIUNGO VYOTE VIKO SALAMA
MWILI WA MTU ASIYEFAHAMIKA KWA JINA HADI SASA. HUYU MTU NDIYE ALIYEFANYA MAUAJI YA MTOTO AYUBU
BAADA YA MAUAJI YA MTOTO AYUBU WANANCHI WA KIJIJI CHA IJOKA MWAKALELI WALIFANYA MSAKO NA KUMGUNDUA MUUAJI NA KUMWEKA CHINI YA ULINZI LAKINI BAADA YA MUDA MFUPI WAKAJITOKEZA WENGINE NA KUMSHAMBULIA MTU HUYU NA KUUMPIGA NA KUMMCHOMA MOTO HADI KIFO

DR STAPHORD NA WAHUDUMU WA MOCHWALI NA ASKALI POLICE WAKIFANYA UCHUNGUZI
KULIA NI BABA MZAZI WA AYUBU AKIONGEA NAMI JINSI ALIVYOPATA TAARIFA NA KUMUONA MWANAE AKIWA TAYARIA KAUWAWA. BWANA AGENI ANASEMA KUWA ALIONDOKA NYUMBANI SAA KUMI JIONI NA ALIWAACHA NYUMBANI WATOTO WOTE AKIWEPO NA MAREHEMU AYUBU. AKIWA KILABUNI KWENYE MAONGEZI NA WENZAKE BWANA AGEN ANASEMA AKALETEWA TAARIFA KUWA AYUBU AMEUWAWA NDIPO AKACHUKUA JUKUMU LA KWENDA KWENDA KWENYE TUKIO NA KUKUTA MWANAE AMEUWAWA KWA KUKATWA KICHWA NA WAUAJI KUONDOKA NA KICHWA HICHO
KULIA NI RAPHAEL MWAIKENDA AMBAYE NI MTENDAJI WA KIJIJI CHA IJOKA MWAKALELI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA. AMBAYE AMESEMA KUWA BAADA YA WANANCHI KUKUSANYIKA NA HUKU MSAKO UKAENDELEA NA WANANCHI KUFANIKIWA KUMPATA MTUHUMIWA MMOJA NA KUMUWEKA CHINI TA ULINZI ILI POLISI WAKIFIKA WAMCHUKUE LAKINI IKASHINDIKANA KWAKUWA WATU WALIOKUWA NA HASIRA WAKAAMUA KUMPIGA NA  KUMCHOMA MOTO HADI MAUTI IKAMFIKA NA POLISI WALIPOFIKA WALIKUTA MTUHUMIWA AMEUWAWA.

MHUDUMU WA MOCHWALI AKIUBEBA MWILI WA MTOTO AYUBU NA KUUKABIDHI KWA FAMILIA YA MAREHEMU NA KURUDI MWAKALELI KWA AJILI YA MAZIKO

BABA MZAZI WA AYUBU AKIWA NDANI YA GALI LA POLICE AKIWA AMEUBEBA MWILI WA MWANAE TAYARI KWA KURUDI KWAO MWAKALELI KATIKA KIJIJI CHA IJOKA

ERNESTH KALINGA MFANYAKAZI WA MOCHWALI YA TUKUYU KWA WATU WANAO MFAHAM SANA HUYU JAMAAA NI MTU MCHAPA KAZI NA MWENYE UPENDO SANA. BAADA YA MATUKIO KADHAA KUJITOKEZA WILAYANI RUNGWE AMEJIKUTA AKIZUNGUKA SANA KUTOA HUDUMA." MFANO BIZE ILIANZIA  TUKIO LA MWAKALELI LA MTOTO ALIYEZIKWA HAI, NILIPORUDI TU USHIRIKA MTU ALIPIGWA NONDO HADI KIFO USIKU WAKE MTU ALIGOGWA NA GALI KAYUKI NIKAENDA SIJAKAA SAWA NDIO TUKIO LA MTOTO KUUWAWA NA KUTENGANISHWA KICHWA, TUKO NJIANI NARUDI TUKUYU MUUAJI AKAWA AMEUWAWA NA KUCHOMWA MOTO SASA NAFIKA TU OFISIN NIKAWA NAENDA KIWIRA KWENYE AJALI YA PIKIPIKI NDIPO NILIPOANZA KUONA KAMA NAKOSA NGUVU ILE NAFIKA TU HUKO NAPATA TAARIFA MTU MWINGINE AMEPIGWA NA NONDO HAPO NDIPO NILIPOPOTEZA FAHAM NA KUJIKUTA NIPO HOSPITAL KWA MATIBABU, KIUKWELI NILIKUWA NIMECHOKA NA SIJATULIA KUPUMZIKA NA KUPATA CHAKULA LAKINI NAMSHUKURU MUNGU NAENDELEA VYEMA SASA. SASA WILAYA YA RUNGWE MAUAJI YAMEZIDI  " AMESEMA KALINGA. KINGO TANZANIA INAMTAKIA KILA LA KHERI APONE NA KURUDIA MAJUKUMU YAKE YA KILA SIKU.

MATUKIO ya kutisha na ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya kummbana ili aeleze sehemu  walikokificha kichwa cha marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.
Habari za uhakika kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ijoka  katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda,  zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti  huyo alisema,  marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba nyumbani kwao.
Mwaikenda alisema  mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu .
“Marehemu alichukuliwa na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na wenzake baada ya kuona hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi walianza kumtafuta bila mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea na harakati hizo waliukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa kichakana na wauaji hao kuondoka na kichwa” alifafanua Mwaikenda.
Mkazi mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia mashaka.
Alisema baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo hapo.
Hata hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigo mtu huyo licha ya kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu huyo hakijaonekana  na jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki mauaji hayo naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira  ambao licha ya kumuua waliuteketeza mwili wake kwa moto”.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 35  na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa  na imani za kishirikina
.......................................................................................................................................................................

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013

Kikwete-707591 
Ndugu Wananchi;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi.  Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania
Ndugu wananchi; 
Jambo la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013.  Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania.  Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake.  Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake. 
Kwa niaba yenu, nimepokea salamu za shukrani kutoka kwa Rais Xi Jinping akielezea kufurahishwa na mapokezi mazuri tuliyowapatia. Naomba tuendelee kuonesha moyo wa upendo na ukarimu kwa wageni wetu wengine mashuhuri watakaotutembelea siku za usoni.
Ndugu wananchi;
Nami pia, nimemshukuru sana Mheshimiwa Xi Jinping kwa kukubali mwaliko wangu na kufanya ziara ya kihistoria na yenye mafanikio makubwa kwa nchi yetu.  Ameifanyia nchi yetu jambo la heshima kubwa na kumbukumbu isiyosahaulika.  Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kuitembelea, tena siku kumi tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi yake.  Na, kubwa zaidi ni kutumia fursa ya ziara yake hapa nchini kutangazia dunia Sera ya China kwa Afrika katika kipindi cha uongozi wake. 
Tumefarijika sana kusikia kuwa uhusiano na Afrika bado unapewa kipaumbele cha juu na viongozi wapya wa China.  Pia, kuwa China itaendelea kukuza biashara na uwekezaji na kuongeza misaada ya maendeleo kwa Afrika ikiwemo kutoa nafasi 18,000 za mafunzo kwa vijana wa Kiafrika.  Kama mtakumbuka nchi zetu mbili zilitiliana saini mikataka 16 ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali.  Misaada ya maendekeo kwa maeneo yetu ya kipaumbele nayo imejumuishwa.
Ndugu Wananchi;
Rais Xi Jinping alielezea na kusisitiza dhamira yake na ya Serikali na Chama cha Kikomunisti cha China ya kudumisha na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China. Kama mjuavyo uhusiano huo ulianzishwa mwaka 1964 na waasisi wa nchi zetu, yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na Mwenyekiti Mao Zedong aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa China na Waziri Mkuu wake Chou En Lai. 
Rais wa China aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika medani ya kimataifa na kuchangia katika jitihada zetu za kujiletea maendeleo kwa kuongeza misaada ya maendeleo.  Katika miaka 49 ya uhusiano na ushirikiano na China nchi yetu imepata misaada mingi ya maendeleo ikiwemo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere ambao ulizinduliwa na Rais Xi Jinping wakati wa ziara yake.
Ndugu wananchi; 
Kuna miradi kadhaa mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini, Bara na Zanzibar, kwa msaada wa Serikali ya China.  Wakati wa ziara yake, Rais Xi Jinping iliahidi kuendelea kutusaidia miradi mingine ya maendeleo kama tulivyoomba wakati wa mazungumzo yetu licha ya ile ambayo ilitiwa saini siku ile. 
Ajali ya Kuporomoka Jengo la Ghorofa
Jijini Dar es Salaam
.............................................................................................................................................................

No comments: