Saturday, March 30, 2013

SAMAHANI WADAU KWA KUTOKUWA HEWANI SIKU MBILI NILIPATWA NA MSIBA WA MPANGAJI NINAYEISHI NAYE KWANGU ALIFIWA NA MTOTO WAKE NA MAZIKO KWENDA KUFANYIKA KIJIJI CHA MAYOTA WILAYA YA MBARALI MKOANI MBEYA. KINGO TANZANIA INAWATAKIA PASAKA NJEMA WADAU WOTE

MAREHEMU SAADA KUSHOTO AKIWA NA WADOGO ZAKE

FAMILIA YA KAWOGO WAKIFURAHI KWA PAMOJA

MAREHEMU DADA SAADA ENZI ZA UHAI WAKE NA HII PICHA NI YA MWEZI MMOJA KABLA YA KIFO
SAFARI YA KUTOKA TUKUYU HADI MBARALI KIJIJI CHA MAYOTA NI MWENDO WA MASAA 4 KWA GALI DOGO NA SAFARI ILIKUWA NI USIKU NA UKIFIKA LUJEWA UNATAKIWA KUVUKA MTO MKUBWA NDIPO UNAFIKA KIJIJI CHA MAYOTA NA NDIKO MAZIKO YANAFANYIKA. SASA HAPO NI USIKU SANA TUNAVUKA MTO NA MAJI YANAFIKA KIFUANI NA HUKU TUMEBEBA JENEZA
KWASABABU BINTI SAADA ALIKUWA MUISLAM ASUBUHI JENEZA TULILOSAFIRISHIA MWILI WA MAREHEM TUKAKUTA JENEZA LIKO NJE

NIKAPATA NAFASI YA KUWA MMOJA WA WATU WALIO TENGENEZA SANDA YA MAREHEMU

MAZIKO
KIJIJINI MAYOTA MVUA ZILICHELEWA KUNYESHA ZIMESABABISHA MAHINDI KUANZA KUKAUKA YAKIWA BADO MACHANGA KITENDO KINACHOASHIRIA NJAA KUBWA SANA MWAKA HUU
MAJI YAMEJAA MTONI SASA KAZI NI TUTAPITAJE
UKAFIKA MUDA WA KUVUKA MAJI YA MTO MAYOTA HAPO LAZIMA NGUO ZIVULIWE
MWANZO WA KUVUKA MTO

SASA KINA CHA MAJI KIMEKUWA KIFUPI NIMEPATA NAFASI YA KUPIGA PICHA
 ..........................................................................................................


MTU mmoja Mkazi wa Kitongoji cha Iponjola Kijiji cha Isange Wilaya ya Rungwe Mkoani hapa anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumzika mwanaye wa kumzaa kwa siri ndani ya nyumba yake.
  
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema lilitokea juzi majira ya saa Saba  mchana baada ya kugundua kuwa  mtoto Debora Riziki (3) kyusa, mkazi wa Iponjola, aligundulika akiwa amefariki baada ya kufukiwa kwenye shimo ndani ya nyumba ya baba yake mzazi.
  
Alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Riziki Saidi Mwangoka (27),kyusa,mkulima ,mkazi wa Iponjola na kuongeza kuwa tukio hilo lilifanywa na mzazi huyo Novemba 29, Mwaka 2012.
 
Alisema  chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kindoa kati ya mtuhumiwa na aliyekuwa mke wake Esther  Msafiri Mwambenja (23),kyusa,mkulima ,mkazi wa Kibumbwe-Kiwira.
  
Kamanda Diwani alisema mgogoro wao ulipelekea wagombee nani aishi na mtoto huyo baada ya wanandoa hao kutengana hivyo Novemba 28, Mwaka 2012 majira ya saa 11 Jioni  mtuhumiwa alimchukua kwa nguvu marehemu kutoka kwa mama yake na kwenda nae kwake kisha kumuua na kumfukia sebuleni ndani ya  nyumba yake.
Alisema  mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya kuzikwa ambapo mtuhumiwa amekamatwa na taratibu zinafanywa ili afikishwe mahakamani.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  anatoa mwito  kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika.
  
Pia  anatoa rai kwa wanandoa kutatua matatizo na migogoro yao kwa njia ya  kukaa meza ya mazungumzo badala ya kutanguliza hasira na matumizi ya nguvu.
................................................................................................................................

No comments: