Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti
wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe
Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki.
Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama
Fatma Mrisho na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.
(PICHA NA IKULU)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu baada ya taarifa ya utafiti wa
viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe
Mizengo Pinda’, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi
(TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kuzindua rasmi taarifa ya
utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27,
2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi taarifa ya
utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27,
2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe
Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt
Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa.
Wadau
kutoka sekta mbalimbali wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na
Malaria wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya
ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam.
Meza
kuu ikimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi
(TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya
ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam.
..................................................................................................................................................................
SIRI YA KUUAWA ZITTO’-ZITO ATOA TAMKO
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’
na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa
atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa
kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na
wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja, sijawahi katika maisha
yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao
ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi
kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika,
pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha
pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari
iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa
vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu
Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya
hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi
itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu
mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku
moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria
kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu
maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto
yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo
yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari
na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli
huo.
Tatu, nawashauri watu ambao
wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama
vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio
wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya
kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili
asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha
malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji.
Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu
ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria
kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo
ya taasisi.
Nne, Nawashauri viongozi wa
CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya
chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama
chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za
binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano.
Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya
kuanzishwa chama chetu.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 201
.......................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment