Mwakilishi
wa Wabunge waliomaliza mafunzo maalumu ya muda mfupi ya Jeshi la
Kujenga Taifa(JKT)katika kambi ya RUVU Ester Bulaya akikabidhi risala
kwa niaba ya wenzake kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
leo mchana. Wabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita
kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mris Wabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita
kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho kikwete
wakati wa gwaride maalumu la kumaliza mafunzo hayo huko kambi ya RUVU
leo. Wabunge walihudhuria mafunzo ya muda mfupi Ruvu JKT wakionesha walijifunza kwa vitendo. Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga risasi hewani
kuashiria kuzundua mafunzo ya JKT kwa vijana katika kambi ya RUVU JKT
yatakayo itwa Operesheni Miaka Hamsini. Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Waziri wa
Ulinzi Mh.Vuai Shamsi Nahodha mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza
pamoja na viongozi wa JKT wakiwa katika picha ya pamoja na wabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi katika kambi ya JKT Ruvu. Rais Jakaya Kikwete akikagua mradi wa ufugaji kuku katika kambi ya Ruvu JKT leo(picha na Freddy Maro). Rais Jakaya Kikwete akikagua mradi wa ufugaji kuku katika kambi ya Ruvu JKT leo(picha na Freddy Maro).
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.(Picha na Freddy Maro)
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani
.........................................................................................................................................................
NWAKA MWAKISU AKONGA NYOYO ZA VIJANA MBEYA
Nwaka Mwakisu akiongea na vijana wa Uyole hivi karibuni |
Timu ya Redio Bomba fm, |
Timu ya Veterani ya Uyole |
Timu mbali mbali zilikuwepo uwanjani hapo |
Vijana mbali mbali walijitokeza kuchangia damu siku hiyo
BAADHI ya Wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya
wamepongeza jitihada za Vijana wanaojitolea kusaidia makundi ya watu
wasiojiweza na wenye uhitaji kutokana na kufanya hivyo bila kujali itikadi za
vyama wala dini zao.
Kijana anayetajwa kukonga mioyo ya wananchi wa
Mbeya kutokana na kusaidia makundi mbali mbali ya Vijana, Yatima na wazee ni
Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Nwaka Mwakisu.
Wananchi hao wamesema Nwaka Mwakisu amekuwa
kivutio kwa Vijana wengi wa kada mbali mbali kutokana na ushiriki wake katika
kazi za maendeleo ndani ya Mkoa wa Mbeya ambapo pia amekuwa akiwaunganisha
vijana hao kwenye makundi ili waepukane na shughuli zisizofaa katika jamii.
Wamesema Mwakisu ameonesha moyo wa tofauti
miungoni mwa Vijana Mkoani Mbeya ambapo katika kipindi kifupi cha kuanzia
Januari hadi Machi Mwaka huu ameshiriki na kuambatana na vijana kutembelea
vituo vya watoto yatima vilivyopo Uyole na Simike Jijini Mbeya.
Wakizungumza na Mbeya yetu katika mahojiano
maalumu juu na namna Vijana wenye uwezo wanavyoweza kusaidia makundi
mbali mbali katika kuwakomboa kiuchumi ambapo hawakusita kumtaja Nwaka
Mwakisu kuwa ni miongoni mwa vijana wachache wanaojitolea kwa moyo wote.
Iddi Ramadhani ni Mwenyekiti wa Bajaji Jiji la
Mbeya ambaye alisema Mwakisu amewatembelea mara kadhaa katika kujua wanahitaji
nini ili aweze kwasaidia ambapo ameshwasaidia vijana hao Vifaa vya michezo kama
vile Jezi, Soksi na Viatu kwa ajili ya timu ya Waendesha bajaji yenye makao
makuu Ilemi Jijini Mbeya.
Mbali na waendesha bajaji vijana wengin
walionufaika na Msaada wa Mwakisu ni timu za Mpira kutoka Uyole katika kata ya
Itezi Jijini Mbeya ambao walipatiwa vifaa vya michezo ambavyo ni seti tatu za
Jezi na mipira kwa ajili ya mashindano ya Umoja yaliyomalizika hivi karibuni.
Nwaka Mwakisu alipotafutwa kuzungumzia maswala
hayo alisema binadamu tumeumbwa kwa ajili ya kusaidiana hivyo si vibaya kwa
yeye kujitolea kwa watu wenye uhitaji ambapo aliongeza kuwa hafayi hivyo kwa
ajili ya kujinufaisha yeye binafsi.
Alisema kiu yake ni kuona Vijana wanakuwa na
umoja kwani baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana kuvuruga amani
Mkoani Mbeya ambapo baada ya vurugu viongozi hao hawajitokezi kuwasaidia pindi
wanapopata madhara kutokana na athari wanazopata katika vurugu hizo.
Kutokana na kuwaunganisha vijana hao katika
baadhi ya michezo ambapo vijana hao hupata nafasi pia ya kuchangia damu
kutokana na uhitaji wa damu katika michezo iliyomalizika Uyole Jijini Mbeya katika
viwanja vya Shule ya Msingi Gombe iliyowahusisha timu ya kituo cha Redio cha
Bomba fm, Veterani ya Uyole na vijana wengine.
Mbali na vijana hao kumpongeza Nwaka Mwakisu kwa
kujitolea na kuwaunganisha Vijana hao, Diwani wa Kata ya Itezi Frank Maemba
alisema wanachokifanya Vijana hao ni kutekeleza sera za chama cha mapinduzi
inayotaka Vijana waunganishwe kwenye makundi ili iwe rahisi kupatiwa misaada
ikiwa ni pamoja na kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana.
Hata hivyo wajibu huo umeonekana kuekelezwa
zaidi na viongozi vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya ambao wameonekana
kuunga mkono juhudi hizo ambao ni Mjumbe wa Mkutano mkuu taifa(CCM), Charles
Mwakipesile ambaye aliwahi kutoa Kompyuta yenye thamani ya Shilingi Laki tano
na Nusu(550,000/=) kwa Vijana wanaoendesha Bajaji Jiji la Mbeya.
...........................................................................................................................
IGP MWEMA: HUDUMA BORA KWA WANANCHI SIYO HIARI
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
…………………………………………………………….
Askari Polisi Nchini wametakiwa
kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi ili kuendeleza mahusiano mema
na Jamii pamoja na kushirikiana katika kuendeleza mpango wa Polisi
jamii na Ulinzi shirikishi ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwafichua
wahalifu hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Jeshi
la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati alipokuwa akizindua Programu za
Mafunzo kazini kwa askari Polisi Tanzania nzima katika Chuo cha Taaluma
ya Polisi Jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi huo ulihudhuriwa na
Maofisa mbalimbali wa Polisi pamoja na Askari kutoka Makao makuu ya
Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam pamoja na Vikosi vilivyopo jijini
Dar es Salaam.
IGP Mwema alisema jambo la kutoa
huduma bora kwa wananchi siyo la hiari bali ni la lazima hivyo kila
askari anapaswa kuboresha huduma anayoitoa kwa kuzingatia mafunzo
aliyonayo ili kuleta ufanisi wa kazi na kuimarisha usalama wa raia na
mali zao.
Alisema Wananchi nao wanapaswa
kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na
wahalifu kwa Jeshi hilo ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka katika
kuzuia, kubaini na kutanzua uhalifu hapa Nchini.
“Usalama unaanza na mimi, wewe
na sisi sote hivyo kila mmoja anatakiwa ajiulize anachangia nini katika
kuimarisha ulinzi wake binafsi, wa jirani yake na wa taifa kwa ujumla
kwa vile suala hili siyo la Jeshi la Polisi peke yake ni wajibu wa kila
mmoja” Alisema IGP Mwema.
Aidha aliwataka Maofisa na
Askari kuitumia vyema fursa ya Mafunzo kazini kujiendeleza kielimu ili
kuboresha ufanisi wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku pamoja
na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kazi na maisha.
Mwema alitoa wito kwa kila Askari
na Ofisa kuutumia vyema mpango huo wa mafunzo kazini kujitengea muda
vizuri kwa ajili ya kujisomea nje na saa za kazi ili kuboresha huduma
bora kwa wananchi ambapo alisisitiza suala la kutoa huduma bora kwa
wananchi siyo la hiari ni kuto na maboresho ya Jeshi la Polisi
yanayolenga kufanya kazi kwa weledi na usasa katika kuihudumia jamii na
wananchi ..
.............................................................................................................................................................................................................
|
No comments:
Post a Comment