Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. Sospeter Muhongo amekutana na katibu mtendaji wa Tume ya Uchumi Afrika
(ADF), Dr. Carlos Lopes ofisini kwake jumanne asubuhi.
Akizungumzia ujio wake Dr Carlos alisema chombo
hicho chenye makao makuu yake Adis Ababa kinafanya kazi kwa ushirikiano na
Umoja wa Africa, Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB) na
washirika wengine muhimu katika kuleta maendeleo kupitia programu maalumu za
kimaendeleo.
Carlos alisema tume ya uchumi ina wadau ambao
hufanya midahalo ya kujadili na kuanzisha mikakati madhubuti kwa ajili ya
maendeleo ya Africa.
Alisema, lengo la ADF
ni kuwasilisha matokeo ya utafiti na maoni juu ya masuala muhimu ya maendeleo
ili kuweka malengo, vipaumbele na mipango pamoja na kufafanua mazingira yatakayo
wezesha mataifa ya Afrika kutekeleza programu husika.
Aliendelea kusema mabadiliko makubwa yanatarajiwa kufanyika
katika sekta za madini na nishati na kwamba wanamaono ya kuanzisha kituo cha
maendeleo cha madini (Mining development
centre), kuhamasisha utunzaji wa mali asili pamoja na kuboresha masuala ya kilimo.
Mpango huu huwasilishwa
kwa wadau mbalimbali Afrika wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, watunga sera,
wadau wa maendeleo, taasisi za kimataifa na taasisi zisizo za kiserikali ili
kujadili namna ya kuleta mapinduzi hayo yatakayoinua uchumi wa bara la Africa.
Mheshimiwa Waziri
alimshukuru Dr. Calos kwa kuona umuhimu wa kufika na kuzungumza nae, Mheshimiwa Muhongo alisema amefurahishwa na mpango wa
UNECA (United Nation, Economic Commision for Africa) wa kufanya mabadiliko ya
kiuchumi na kukazia kwamba yuko tayari kushirikiana katika kuleta mabadiliko
hayo. Aidha, Mheshimiwa Muhongo alisisitiza kuwa ni lazima kubadilisha mtazamo wa
baadhi ya waafrika wa kujiona hawawezi kila wakati.
Muhongo alisema
anaamini kwamba Tanzania inaweza kuongoza katika uzalishaji wa madini miaka
ijayo na japo kuwa inakabiliwa na tatizo la uhaba wa wataalamu na mafundi
katika sekta za nishati na madini. Muhongo alisema wataalamu wengi waliopo
wamefikia umri wa kustaafu na hivyo kuacha pengo kubwa kwa tasnia za nishati na
Madini.
Muhongo alisisitiza
umuhimu wa kujenga uwezo wa kitaaluma katika Nyanja za utafutaji na uendelezaji
wa mafuta na gesi aliomba ADF kusaidia
katika kufanikisha suala hilo.
Mpaka sasa Wizara
imejitahidi kutafuta na kupata wafadhili ili kuwawezesha watanzania kujiendeleza katika masuala ya petroli
na gesi katika nchi za Brazili na China na mpaka sasa kuna jumla ya wanafunzi 40. Lakini
pia vyuo mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Technolojia Dar es Salaam na chuo
kikuu cha Dodoma watawezeshwa kutoa mafunzo katika tasnia ya mafuta na gesi.
Waziri aliongeza
kwamba tunahitaji kuongeza uwezo pia katika masuala ya nishati katika maeneo ya
uzalishaji wa umeme, usafirishaji pamoja na usambazaji kwani nishati ni huduma
muhimu ya msingi sana katika kupata maendeleo.
Nuru I. Mwasampeta
Information Officer II
Ministry of Energy and Minerals
Information Officer II
Ministry of Energy and Minerals
.............................................................................................................................................................
WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012 WAMEFELI TENA
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani
la Taifa (NECTA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo
zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi waliokata rufaa wamefeli
zaidi na hata walioongezewa alama matokeo hayakubadilisha madaraja
waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa, wanafunzi waliokata rufaa NECTA
kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni takribani 10,000 na kwamba
baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo
vya habari kutoka ndani ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa
wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa
Machi 15, mwaka huu na kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi
kadhaa kukata rufaa, NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika
masomo yote na kuanza kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa
umakini, kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli
kimeongezeka,” alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake
lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.
Wakizungumza
na NIPASHE, baadhi ya walimu walisema walioshiriki kusahihisha mitihani
hiyo walisema kuwa maoni yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya watu kwamba
matokeo mabaya ya mtihani huo yalitokana na uchakachuaji, hayakuwa ya
kweli.Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na
NIPASHE jana alithibitisha kuwa mitihani ya wanafunzi waliokata rufaa
ilianza kusahihishwa Machi 12 mwaka huu.
Dk
Ndalichako alisema hata hivyo, hana taarifa kama matokeo ya wanafunzi
hao yanaonyesha kuwa wanafunzi wengi wamefeli zaidi kwa kuwa alikuwa
safarini kikazi.“Unavyozungumza na mimi nipo Arusha na wageni, sifahamu
kama baada ya kusahihishwa upya mtihani wa wanafunzi waliokata rufaa
matokeo yamekuwaje, nitafahamu baada ya kurejea Dar es Salaam Jumatano
wiki hii,” alisema Dk Ndalichako ambaye hata hivyo, hakutaja idadi ya
wanafunzi waliokata rufani.Dk Ndalichako alisema suala la kufeli zaidi
wanafunzi waliokata rufaa linawezekana kutokea kwa sababu kila mwaka
imekuwa ikijitokeza hali kama hiyo, hivyo ni jambo la kawaida
NIPASHE
..................................................................................................................................
ABOMOLEWA NYUMBA NA KUCHOMEWA VYOMBO VYA NDANI KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA ILEMI MBEYA
Wananchi wenye hasira kali wakibomoa nyumba ya mama Atupele Kalile akidhaniwa kuwa mchawi maeneo ya ilemi Mbeya |
Kazi ya kubomoa nyumba ya mama huyo inaendelea |
Wengine wameshaingia ndani na kuanza kutoa vyombo nje tayari kwa kuvichoma |
Mtoto wa mama Atupele akijaribu kuokoa vitu vya mama yake visichomwe moto na wanakijiji |
Vyombo vinazidi kutolewa ndani ilivichomwe moto |
Tayari wameshaanza kuchoma moto vyombo vya mama Atupele |
Mwingine anaendelea kubomoa nyumba ya mama Atupele |
Wamefyeka shamba lake lote la mahindi |
Wengine wanapongezana kwa kazi waliofanya |
Kushoto mama Atupele Kalile anaedhaniwa kuwa ni mshirikina akiwa na mtoto wake
MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Atupele
Kalile (60) mkazi wa Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya amenusurika kifo
baada ya wananchi wa Mtaa huo kutaka kumpiga kisha kubomoa nyumba yake
wakimtuhumu kwa ushirikina.
Wananchi hao kumtuhumu Mwanamke huyo kuhusika na
upotevu wa motto mwenye umriwa miaka mitatu(3) (Judith Chengula) aliyepotea
katika mazingira ya kutatanisha Februai 22, Mwaka huu.
Kwa mujibu wa wakazi hao walisema Mtoto huyo
alipotea majira ya saa 11 jioni baada ya kupoteana na dada yake Anitha
Mgaya wakiwa wametokea kanisani ambapo hadi sasa mototo huyo hakuweza
kupatikana licha ya juhudi kubwa za wakazi hao kumtafuta bila Jitihada.
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa
mtaani hapo kwa ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtotolakini Mwanamke
huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu miongoni mwa wakazi hao
hali iliyopelekea kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23
Mwaka huu majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea kusisitiza
kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa
motto ambapo iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na
kufanya upekuzi walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina
ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo Mwanamke huyo baada ya
kuulizwa alishindwa kutolea ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na
hasira na kuanza kumpiga.
Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa
huo Nedy Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo kutoka kwa wananchi
kwa kumpeleka katika kituo kikuu cha Polisi kwa usalama zaidi.
Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa
katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba zao ambapo waliamua
kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa
yamepandwa jirani na nyumba yake.
Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia
hapo bali walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Agnes Sika
ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost Groly kwa madai kuwa ni
rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa akimfichia siri.
Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na
kumnusuru Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa nyumba yake
ambayo tayari wananchi hao walionekana kuikimbilia kwa ajili ya kutaka
kuibomoa.
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia
mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba mzazi wa
Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya kutatanisha akisema anamwachia
Mungu baada ya juhudi za kumtafuta kushindikana.
picha na E. Kamanga
................................................................................................................................
BAISKELI; USAFIRI UNAOTEGEMEWA NA WAJAWAZITO KYELA
Wanawake wa kijiji cha Masoko wakiwa wamekusanyika ili kuongea na mwandishi wa habari hii
Na Stella MwaikusaWajawazito wa vijiji vya Masoko na Busoka vinavyopatikana kata ya Busale wilaya ya Kyela, wamekuwa wakitumia usafiri wa baiskeli wakati wa kwenda kupima maendeleo ya ujauzito katika zahanati ya Lema, ambayo iko umbali wa km sita kutoka vijiji hivyo. Zawadi Oscar (22) mkazi wa kijiji cha Masoko anasema alipokuwa na ujauzito alikuwa akitumia usafiri wa baiskeli kwenda kliniki ,kutokana na zahanati ya Lema kuwa mbali na kijiji hicho. “Nilikuwa na ujauzito wa miezi nane, ,lakini niliendesha baiskeli kwenda kliniki, maana afadhali kwenda huko kwa baiskel kuliko kutembea kwa mguu, unachoka sana” anaeleza Zawadi. Chistina Musa mkazi wa kijiji cha Masoko anasema usafiri wa baiskeli kwa wajawazito katika kijiji hicho ni kitu kilichozoeleka, kwani hata yeye hutumia usafiri huo anapoenda kliniki katika zahanati ya Lema. Anasema haoni tatizo kuendesha baiskeli, japo alikiri kwamba baada ya kutoka zahanati hujisikia kuchoka, lakini hana namna kwani katika kijiji anachoishi hakuna zahanati. Mganga mkuu wa zahanati ya Lema, Mariam Ninde anasema ni kweli wajawazito kutoka vijiji vya Masoko na Busoka hutumia usafiri wa baiskeli na kuutaja usafiri huo kutokuwa na madhara kiafya kwa wajawazito. “Mjamzito anapoendesha baiskeli ni moja kati ya mazoezi kwa hiyo hakuna ubaya,” anaeleza Ninde.
...............................................................................................................................
WABUNGE ZITTO, AZAN WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA),
Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo Machi 26,2013 wamemaliza rasmi
mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani
Tanga.
Pichani juu ni Zitto na Azan
akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani
pamoja na Mbunge mwenzake Iddi Azan,
Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.
Aidha Zitto Kabwe amesema
anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa
katika maisha yake.
.............................................................................................................................
ELIZABETH T. MOSHI AMBAYE NI AFISA UTUMISHI WA WILAYA YA RUNGWE AFANYIWA SHEREHE YA KICHENPART NA WAMAMA WA TUKUYU MJINI ANATARAJIA KUFUNGA NDOA MWANZONI MWA MWEZI WA NNE JIJINI ARUSHA
|
No comments:
Post a Comment