Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo kuanzia asubuhi |
Matairi yanachomwa katikati ya barabara |
Mambo hayo |
ISHU NI KUCHINJA NYAMA SASA WANACHOMA NA BARABARA ZILIZOJENGWA KWA KODI ZA WATANZANIA |
MIENDOMBINU YA UMEME NAYO INAHUJUMIWA |
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiongea na waandishi wa habari |
Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao |
Polisi wakiendelea kazi yao katika mitaa ya Tunduma |
Baadhi ya magati ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo |
...........................................................................................................
Jaji Mstaafu Ernest Mwipopo Amefariki Dunia
JAJI MSTAAFU ERNEST MWIPOPO AMEFARIKI DUNIA JANA ALASIRI KWA AJALI YA GARI MKOANI MOROGORO:
TAARIFA ZAIDI TUTAZIWEKA HUMU KADRI TUKAVYOZIPOKEA
................................................................................................................................
MWANAMKE ABAMBWA AKIMUUZA MTOTO WA KUMZAA KWA SHILINGI 100,000/=
Mwanamke mmoja mkazi wa kitongoji cha Seif katika
kijiji cha Chiwezi-Mpemba TABU MWASHITETE
anashikiriwa na polisi wilayani Momba kwa tuhuma za kuumuuza mtoto wake
wa kumzaa mwenye umri wa miaka mitano kwa shilingi 100,000/=.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 12 jioni baada ya majadiliano ya biashara hiyo yaliyodumu
kwa saa 7 baina ya muuzaji na mnunuzi.
Akizungumzia mchezo
ulivyokuwa mpaka kumkamata mtuhumiwa, Bwana John Sinyinza ambaye alishakuwa
mtumishi wa umma na kustaafu anaeleza kuwa alifuatwa na Bi Tabu majira ya saa
tano asubuhi nyumbani kwake.
Anaeleza kuwa katika
mazungumzo na mama huyo alishitushwa
alipoambiwa kuwa anamuuza mtoto ambaye amemtoa Malawi na kwamba lengo la
kumuuza anataka kupata fedha kwaajili ya kugharimia kumtoa baba yake mzazi wa
mtoto huyo ambaye amefungwa nchini Malawi.
Hata hivyo katika
majadiliano ya biashara hiyo, mwanamke huyo alitaka kulipwa kiasi cha shilingi
1,000,000/=(Milioni Moja) ambapo walikubaliana kuwa wangeuziana majira ya saa
12 jioni baada ya kupatikana kwa fedha hizo.
Ndipo bwana Sinyinza
kutokana na tukio hilo kutokuwa la kawaida aliwasiliana na vyombo vya usalama
na kupewa askari wa kike wa upelelezi ili waongozane eneo la tukio ambapo
katika mtego wa kufanyika biashara hiyo, mwanamke huyo alifika akiwa na mwanaye
ambaye alikuwa uchi ili wakabidhiane.
Bwana Sinyenga katika
kuhakikisha kuwa mwanamke huyo hashtukii mchezo alimtambulisha askari huyo kama
binti yake na kwamba walikubaliana kulipata fedha hizo kwa awamu ambapo
angemlipa shilingi 100,000/= kwanza na kesho yake angemaliziwa kiasi cha
shilingi 900,000/= zilizobakia.
Kufuatia makubaliano
hayo mwanamke huyo alimkabidhi mtoto wake kwa mnunuzi na baadaye kuagana kwa makubaliano kuwa angepewa kiasi
kilichobakia na binti huyo wa upelelezi kesho yake.
Baada ya mteja kutoweka na “bidhaa ya mtoto” ndipo askari wa upelelezi huyo alipomweka chini ya
ulinzi bi mkubwa huyo na baadaye kufikishwa
kituo ch polisi cha Tunduma ambako
katika mahojiano imebainika kuwa mtoto huyo ni mwanaye ambaye baba yake alishafariki.
Alisema kuwa kutokana
na ugumu wa maisha aliamua kumuuza mtoto wake huyo ili apate fedha kwaajili ya
shughuli za kiuchumi kama mtaji na kwamba anatambua kuwa wanunuzi wangeweza
kumuua mtoto huyo ama kwa matumizi mengine!
Kulingana na fununu za
jeshi la polisi mwanamke huyo atafikishwa mahakamani leo jumatano katika
mahakama ya wilaya ya Mbozi
na DANNY TWEVE
MBOZI
.................................................................................................................................
Kamati Kuu Chadema Kukutana Dar
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa siku mbili kwenye kikao chake cha
kawaida jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 3-4 Aprili, 2013.
Katika kikao hicho cha siku mbili,
Kamati Kuu itajadili pamoja na mambo mengine, yatokanayo na kikao
kilichopita, hali ya kisiasa nchini, pia itapokea taarifa ya utekelezaji
wa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika mwezi Februari mwaka
huu, ikiwemo mpango wa uendeshaji chama kwa kanda.
Aidha, Kamati Kuu pia itajadili mpango kazi na bajeti ya Chama kwa mwaka 2013-2014
Imetolewa Aprili 2, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
..............................................................................................................................
ATCL KUANZA SAFARI ZAKE HIVI KARIBUNI KATIKA MKOA WA MBEYA
NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE ATCL IKITUA KWA MARA YA KWANZA KATIKA KIWANJA CHA KIMATAIFA CHA NDEGE SONGWE KUASHIRIA KUA WAKATI WOWOTE WANAANZA SAFARI YA KUJA MBEYA |
BAADHI YA ABIRIA WAKISHUKA KATIKA NDEGE HIYO AKIWAMO MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJIRI ROSE MHANDO |
MUONEKANO WA NDANI YA NDEGE |
SEHEMU YA RUBANI WA NDEGE..................................................................................................................................TTCL YAZINDUA HUDUMA YA ‘BANDO NA TTCL’ NA KAMPENI YA PUNGUZO KUBWA LA BEI YA INTANETI
Peter
Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha moja ya simu zinazouzwa
na kampuni hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo
la makao makuu ya kampuni ya TTCL mtaa wa Samora wakati kampuni hiyo
ilipozindua rasmi huduma za Bando na TTCL na Basti leo jijini Dar es
salaam kulia ni Kisamba Tambwe Mkuu wa Mauzo Kampuni ya TTCL.
Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha
kampeni ya Bando na TTCL mara baada ya kuizindua rasmi kushoto
anayepiga makofi ni Ernesti Isaya Mkuu wa Maendeleo ya Bidhaa TTCL.
Peter Ngota Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko akionyesha kampeni ya BASTI ambayo ina viwango vipya vya muda wa kuperuzi kwenye mtandao wa kampuni hiyo.
…………………………………………………………………………
TTCL, imezindua huduma mpya ya Bando Na TTCL inayoambatana na punguzo
kubwa la bei kwa huduma ya INTERNET. Mtakumbuka ni Juzi tu tareha 21 Machi 2013
tulifungua kituo chetu kipya cha huduma kwa wateja kilichopo Kariakoo katika mkoa
wa Dar es Salaam katika kupanua mtandao wa huduma kwa wateja nchini (>30 CSC
network nchini).
Kifuatacho sasa ni kupanua wigo wa huduma kwa wateja.
Vilevile mtakumbuka kuwa baada ya kujitambulisha sokoni na huduma ya ‘Mobile Internet’
isiyo na kikomo ya BANJUKA; kampuni ya simu ya TTCL sasa inazindua huduma mpya
inayojulikana kama ‘BANDO NA TTCL’. Huduma hii inamuwezesha mteja kufaidika na meseji
za bila kikomo, kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa wakati
mmoja kwa bei hadi ya shilingi 500. BANDO NA TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za
kisasa za smart phones za TTCL (zinazopatikana ktk vituo vya huduma kwa wateja
nchini). Maelezo zaidi ya juu ya huduma hii yanapatikana kwa kupiga 100 huduma kwa wateja
au tembelea ofisi zetu za mauzo zilizoenea nchi nzima.
Aidha, TTCL imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa
kampeni ya BASTI ikimaanisha peruzi intaneti zaidi kwa gharama nafuu. Hili ni punguzo la bei
la aina yake. Mathalani; kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000
sasa kinauzwa kwa shilingi 25,000 tu. Hii ni nafasi si tu kwa wateja waliopo wa TTCL kuongeza
matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga
na mtandao wa TTCL. (Haki ya mawasiliano kwa wote)
Leo hii, wateja wengi zaidi na hasa wanafunzi na wajasiliamali wanatumia simu za kisasa (smart
phones, tablet PCs kama iPad, Samsung Galaxy nk) na kompyuta ili kupata huduma za intaneti
na mitandao ya kijamii kwa mfano, Michuzi blog, facebook twitter, LinkedIn n.k ) kwa shughuli
zao za kila siku. Upatikanaji wa vifaa hivi vya kisasa (sambamba na ukuaji wa teknolojia) na
kumewezesha kukua kwa kasi kwa tabaka la kati lawatumiaji hivyo kumesababisha kukua
maradufu kwa soko la intaneti hapa nchini. (Hili nijambo jema sana kwa nchi yetu na maendeleo
ya watu wake kiuchumi na kijamii)
Kwa kuzingatia haya (na kutambua kuwa mawasiliano na habari ni swala mtambuka), TTCL ina
mikakati wa kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za intaneti na mawasiliano &
habari kwa ujumla na hivyo kuwa chachu kubwa ya maendeleo nchini. Huduma mpya ya
BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI ni juhudi za makusudi za TTCL katika kutimiza
adhma hii.
|
No comments:
Post a Comment