WANANCHI Wilayani Rungwe wameaswa kutunza vyanzo
vya maji pamoja na mazingira ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa asasi
zisizokuwa za kiserikali zinazohamasisha suala la maji.
Mamlaka ya maji ya bonde la Ziwa Nyasa, imesema
kuwa itaenedelea kushirikiana na asasi zisizokuwa za Kiserikali, kuhakikisha
inatoa elimu kwa wananchi na wadau wa maji ilikutambua umuhimu wa
kutunza vyanzo vyote vya maji vinavyotililisha katika ziwa hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa wa Maji wa bonde
hilo la Ziwa Nyasa, Wilgal Mkondola, wakati wa warsha iliyowajumuisha
wenyeviti wa vijiji vyote vya halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe,
iliyoandaliwa na asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Elimisha ya Jijini Mbeya huku
ikiwa na lengo la kujadili na kutambua vyanzo vyote vya maji vilivyopo ndani ya
halmashauri hiyo na chgangamoto zake.
Alisema kuwa ili kukabiliana na janga la
kupungua kwa maji katika vyanzo mbalimbali vya maji Serikali inatambua umuhimu
wa kushirikiana na asasi za kiraia kwa kuelimisha jamii juu ya utunzaji
wa vyanzo hivyo.
Alisema kuwa kilio kikubwa duniani kote ni
kupungua kwa maji baridi kutokana na uharibifu wa mazingira ambao
kwa nman moja ama nyingine unatokana na shughili za kibinadamu hivyo Serikali
kwa kushirikiana na asasi za kiraia zainawajibu wa kuelimisha wananchi ili
kujiokoa na janga linaloonekana kujitokeza.
“Nia ya Serikali ni kushirikiana na asasi
zisizokuwa za kiraia ili kufikia malengo yanayokusudiwa kwa jamii
nzima, na hivi sasa duniani kote kuna kilio kikubwa cha uharibifu wa
mazingira wa kupungua na kutoweka kwa maji katika vyanzo hivyo ndio maana
asasi hii imeliona suala hili la utunzaji vyanzo vyetu vya maji na kuandaa
warsha hii,’’alisema Mkondola.
Mtendaji Mkuu wa Elimisha, Festo Sikagonamo,
alisema kuwa lengo la kuwashirikisha wenyeviti wa vijiji vyote vya Halmashauri
hiyo ya Busokelo, ni kutaka kuwakutanisha na wataalum mbalimbali wa mazingira
ili kujadili na kuweza kuangalia namna ya kutunza na kuhifadhi
vyanzo hivyo vya maji na sambamba na kuangalia vyanzo vya kuharibika kwa vyanzo
vingine vilivyopo kwenye maeneo husika.
“Lengo la kuandaa warsha hii ni kutaka
kuwakutanisha wenyeviti wa Vijiji pamoja na wataalam wa maji kutoka bonde la
Ziwa Nyasa ili kujadili vyanzo vyote vya maji vilivyopo ndani ya
halmashauri ya Busokelo na kuangalia namna ya kuendelea kuhifadhi pia kuangalia
sababu za kuharibika kwa baadhi ya vyanzo hivyo sambamba ili jamii ipewe elimu
ya kuvijenga na kuvitunza vyanzo hivyo,” alisema Sikagonamo.
|
No comments:
Post a Comment