Tuesday, April 16, 2013

Maggid Mjengwa, "Leo Nimefika Tena Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi..."

SIKU NIKIWA NA KAKA MAGGID MJENGWA SIKU AMBAPO NILIANZA KUPATA MAFUNZO YA KUENDESHA MTANDAO WA KIJAMII NA KUFANIKIWA KUANZA KUWATUMIKIA WATANZANIA KUPITIA NJIA HII HA HABARI KWA NJIA YA MTANDAO

KUSHOTO JESEPH MWAISANGO KATI MAGGID MJENGWA NA KULIA ALLY KINGO

5 cd034
Ndugu zangu,
Leo nilifika tena Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Nilikutana na Kamishna wa Polisi ( Upelelezi) Advocate Nyombi na Afisa mwingine wa Idara hiyo.
Kamishna Nyombi alinijulisha kuwa uchunguzi wa suala la Kibanda ungali ukiendelea. Nami nabaki kwenye kundi la watuhumiwa; tuhuma za kumjeruhi Absalom Kibanda. 
Tumekubaliana nifike tena Makao Makuu ya Polisi Aprili 23.
Ahsanteni sana kwa kuendelea kunifariji kwenye kadhia hii iliyonikuta. Na hakika, nawashukuru sana kwa kuendelea kuniamini.
Ni dhahiri, kuwa kweli itakuja kudhihiri, hata kama kweli hiyo itachelewa kutufikia. Na tuwe wenye subira.
Maggid,
Dar es Salaam.
salamu zangu kwa kaka yangu Maggid 

kingotanzania pamoja na KINGO SUPER PRODUCTION inakutakia kial la heri katika hili maana niaminicho kuwa ukweli huwa unajitenga na uongo, jua kuwa hizi ni hatua za uchunguzi na katika hatuha hizi mambo mengi huwa yanajitokeza lakini jipe moyo kila jaribu liingiapo lina mlango wa kutokea.

KINGO
0752881456
................................................................................................................................... 


Marekani na mashambulio ya kigaidi tena...


Shirika la ujasusi la FBI nchini Marekani limesema linachunguza kile inachodhania kuwa shambulio la kigaidi kufuatria mashambulizi mawili ya mabomu mwishoni mwa mbio za marathon za Boston.
Ikiwa mashambulizi haya yatathibitishwa kuwa mashambulizi ya kigaidi, basi yatakuwa mashambulizi mabaya zaidi kushuhidiwa tangu yale ya Septemba 11 mwaka 2001
Milipuko hiyo miwili mikubwa iliyotokea kwenye mstari wa mwisho wa kumalizia mbio za Boston Marathon nchini Marekani imewauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine zaidi ya mia moja.
Mlipuko wa pili ulitokea sekunde chache tu baada ya ule wa kwanza kutokea wakati mamia ya wanariadha wakikamilisha mbio zao huku wakishangiliwa na umati. Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini huku wengi wao wakitokwa na damu.
Rais Barack Obama amesisitiza kuwa serikali serikali itakahikisha kuwa washukiwa wa mashambulizi hayo lazima atakamatwa.
Picha na video kutoka Boston zilionyesha watu wakiwa wamechanganyikiwa wasijue pa kwenda, huku magari ya huduma za dharura yakielekea katika eneo la tukio na watu waliojeruhiwa vibaya wakipelekwa kwenye hema la matibabu ya haraka.
"Kuna watu wengi wamelala chini," alisema mwanariadha mmoja akinukuliwa na chombo cha habari cha AP.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea saa tatu baada ya washindi kuvuka mstari wa ushindi.
"Kulikuwa na mlipuko, polisi, moto na EMS kwenye eneo la tukio. Hatuna namna ya kufahamu namna watu walivyojeruhiwa," msemaji wa Polisi Boston alisema.
Shirika la habari la AP linasema kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko upande wa kaskazini mwa mtaa wa Boylston Street, karibu tu daraja linaashiria mstari wa kumalizia mashindano. Mlipuko mwingine ukasikika dakika chache baadaye.
Mike Mitchell wa Vancouver kutoka Canada, mwanariadha aliyemaliza kukimbia alisema alikuwa akiangalia nyuma ya mstari wa kumalizia mashindano ndipo aliposikia ‘mlipuko mkubwa’
Inataarifiwa kuwa moshi ulipanda juu hewani kiasi cha futi 50 (mita 15),' aliliambia shirika la habari la Reuters , na watu wakaanza kukimbia wakipiga mayowe baada ya kusikia
Wanariadha waliomaliza mbio za Boston Marathon

"Kila mtu alichanganyikiwa,’ alisema.
Waliokuwa wakimalizia mbio hizo waliongozwa kuepuka eneo lenye moshi kwenye mlipuko wakati huo huo eneo hilo likifungwa.
Tawi la Msalaba Mwekundu la Mashariki mwa Massachusetts limetenga kituo cha kusaidia majeruhi.
....................................................................................................................................................................

Abiria wanusurika kufa baada ya ndege kutumbukia ufukwe wa Bali, Indonesia

ndege 859b3
Zaidi ya abiria 100 wamenusurika kimiujiza jana baada ya ndege kuvuka njia ya kutua/kuruka na kwenda hadi ufukwe wa Bali na kujikita kwenye bahari.

Mashuhuda walisema abiria waliokuwa wakihofia maisha yao walipiga makelele kutokana na kuchanganyikiwa huku ndege hiyo ya Lion Air ilipovuka njia ya kutua/kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Ngurah Rai, karibu na Denparsar.
Ndege hiyo, ilikuwa imebeba abiria 101 na wafanyakazi saba - kisha ikatumbukia baharini kutoka urefu wa karibu mita 50 juu.

Abiria waliojawa na hofu walipigwa picha wakitoka kwenye ndege hiyo iliyovunjika vipande, huku wengi wakisubiri juu ya mabawa yake wakati waokoaji wakifanya juhudi za aina yake za ukoaji.



Uwanja huo wa ndege unafahamika zaidi kutokana na njia yake ya kuruka/kutua kurefushwa hadi baharini.Wengi wa abiria waliokoka kupitia milango ya dharura ambayo ilifunguliwa nusu sambamba na kiunzi hicho cha ndege na kufanya njia yao kuelekea ufukweni.

Baada ya kuwa wameokolewa kutoka kwenye ndege, walipelekwa kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Maofisa wa Uwanja wa Ndege walisema kwamba watu kadhaa walijeruhiwa kwenye ajali hiyo, lakini ukubwa wa majeraha yao haukuweza kufahamika.
Lion Air kwa sasa imefungiwa kusafiri katika Umoja wa Ulaya sababu ya hofu kuhusu viwango vya usalama wake.
Mkuu wa Polisi Bali, Arif Wahyunadi alisema: "Abiria wote na wafanyakazi wameondolewa kwenye ndege hiyo huku ikiwa imelala kwenye maji.
"Wamepokelewa na kuhudumiwa kwenye uwanja wa ndege."
Abiria wote na wafanyakazi wameokolewa salama na kwamba watu 22 wamepelekwa kwenye hospitali tatu tofauti kutokana na majeraha mbalimbali.
Taarifa za awali zinaonesha kwamba kulikuwa na abiria 101 na wafanyakazi saba ndani ya ndege hiyo.
Wahyunadi alisema ndege hiyo asili yake ni mji wa Bandung, mji wa tatu kwa ukubwa nchini Indonesia - kivutio cha utalii sababu ya ujenzi wake.
KUHUSU SHIRIKA LA NDEGE LA LION AIR:
Ndege ilikuwa ikimilikiwa na Lion Air, ambalo kaulimbiu yake ni: Tunawezesha Watu Kuruka.Ni shirika la ndege binafsi la pili kwa ukubwa nchini Indonesia, likishikilia sehemu kubwa ya soko la ndani.

Shirika hilo linafanya safari zake kwenda miji mikuu ya Indonesia, na pia safari nyingine Kusini Mashariki mwa Asia, ikichukua abiria kwenda Vietnam, Singapore, Malaysia na hata Saudi Arabia. Likianzishwa mwaka 1999, shirika hilo lilianza kutumia ndege moja aina ya Boeing 737-200.

Lion Air ni ndege zinazotoza viwango vya chini vya nauli ambalo linashikilia asilimia 45 ya soko nchini Indonesia.


Lion Air limesaini mkataba wa Dola za Marekani bilioni 24 mwezi uliopita kwa ajili ya kununulia ndege 234 aina ya Airbus, oda kubwa kabisa kuwahi kupokewa katika karakana ya kuunda ndege nchini Ufaransa. Pia ilitoa oda kubwa kabisa kwa Boeing pale ilipokamisha mkataba wa kununua ndege 230 mwaka jana. Ndege hizo zitaanza kukabidhiwa kwa Lion Air kuanzia mwaka 2014 hadi 2026.

ndege2 0bc59
ndege3 89b75

ndege4 74f47
 .....................................................................................................................................................................

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ya kabila la Wapogoro wakati alipowasili katika Tarafa na Kijiji cha Mwaya Wilayani Ulanga mkoani Morogoro katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kukagua uhai wa chama lakini pia kuwahimiza wananchi katika kushiriki shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Ndugu Kinana anaendelea na ziara yake leo ambapo leo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika mji wa Ifakara, Katika mkutan.o huo Kinana ametoa wito kwa viongozi wa CCM kuacha kupenda kuitwa waheshimiwa kwani neno hilo halina maana nzuri ya kuwatumikia wananchi waliowachagua na badala yake wapende kutumia neno Ndugu neno lililokuwa limezoeleka sana Enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MAHENGE MOROGORO) 2 
Katibu wa NEC Oganizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib akionyesha kadi zilizorudishwa kwa CCM na waliokuwa wanachama wa CHADEMA wakati wa mkutano wa Hadhara 6 
Wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano huo wa hadhara 14 
 .................................................................................................................................................................

No comments: