JENGO JIPYA LA HALMASHAURI YA RUNGWE AMBALO LIMEANZA KUTUMIKA BAADA YA UJENZI ULIJENGWA KWA AWAMU KWA PESA YA MAPATO YA NDANI |
MADIWANI WA HALMASHAURI YA RUNGWE LEO WAKIWA KATIKA KIKAO CHA KAWAIDA |
MADIWANI WAKIWA KWENYE KIKAO |
KUSHOTO MR SHIRIMA DT WA WILAYA YA RUNGWE |
WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE |
MHE. A.M MWAKASANGULA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE |
MHE, MWALUSAMBA AKICHANGIA MAADA YA UJENZI WA BARABARA ZINAZOSIMAMIWA NA HALMASHAURI ILI KUONGEZA UBORA NA KUJENGWA KWA WAKATI |
EGN WA UJENZI RUNGWE AKIELEZA JINSI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UJENZI UNAVOENDELEA WILAYANI RUNGWE |
WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE |
...............................................................................................................................
BI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA
Msanii mkongwe na maalufu wa muziki wa taarabu Fatma bint Baraka (Bikidude) amefariki Dunia leo mchana huku visiwani Zanzibar,habari zaidi zitawajia hivi punde.
Mwanamuziki gwiji nchini Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa toka kwa familia yake zinasema Bi Kidude aliekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.
Pumzika kwa amani Fatuma Binti Baraka.
................................................................................................................................
WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa baada Gari aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana Usiku. Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
Gari aina ya scania yenye nambali za usajiri T578 ALS likiwa na tela nambli T125 AGM lililobomoa nyumba na kusababisha vifo vya watu 3 wa familia moja |
Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi hii ni miili ya watu walifariki kwa gugongwa na roli hilo |
Wananchi wa kijiji cha Ilongo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakiwa msibani |
WATU
watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa baada Gari
aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana Usiku. Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
Tukio
hilo lilitokea jana majira ya saa Tatu na Robo usiku katika Kijiji cha Ilongo
Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ajali hiyo ilihusisha magari kugongana na
kugonga nyumba na kusababisha vifo na majeruhi.
Alisema
chanzo cha ajali kilitokana na Gari lenye namba za usajili T578 ALS likiwa na
tela lenye namba za usajili T125 AGM aina ya Scania likiendeshwa na dereva
ambaye hakuweza kutambulika liligonga kwa nyuma gari lenye namba
T959 ASC aina ya Scania.
Alisema
gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Juhudi Saimon(34)Mnyiha mkazi wa Dar
Es Salaam kisha gari hilo kugonga nyumba mali ya Matia Mwagala
mkazi wa Kijiji cha Ilongo.
Aliwataja
matrehemu kuwa ni Asia Yahaya (52)mkulima na Msangu, Abubakari Yahaya(8) Msangu
na mwanafunzi darasa la pili aliyekuwa anasoma katika Shule ya msingi
Ilongo na Fatuma Yahaya (6) Msangu mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule
ya Msingi Ilongo wote wakazi wa kijiji hicho.
Aidha
aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na Abuu Fadhil (22)Mzigua
mkazi wa Dar Es Salaam ambaye ni tingo wa gari lililogonga Nyumba pamoja na
Steven Chiwa (26) mbembe raia na mkazi wa Nchi jirani ya Zambia ambaye ni
msindikizaji wa gari hilo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya
Chimala.
Hata
hivyo wa dereva wa gari lililosababisha ajali alikimbia na gari mara baada ya
tukio ambapo Kaimu Kamanda anatoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu ya
mahali alipo dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo azitoe katika mamlaka
husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake, vinginevyo ajisalimishe mara
moja.
Wakati huo huo
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Asajile Mwamtina (46) mkazi
wa kijiji cha Syukula Wilaya ya Rungwe mkoani hapa akituhumiwa kufanya mapenzi
na binti yake wa miaka 13.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
lilitokea juzi majira ya saa Kumi na Mbili jioni baada ya kumvizia binti
huyo (jina limehifadhiwa) ambaye aliacha shule akiwa darasa la tano mwaka 2011
kwa matatizo ya ugonjwa wa kifafa akiwa anapika.
Alisema mtuhumiwa
alipata mwanya wa kufanya unyama huo kutokana na mkewe ambaye mama
mzazi wa mhanga huyo Tumikigwe Samalinga akiwa kijiji cha Kiwira
kuuguza mgonjwa na kuongeza kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika.
Aidha
katika tukio lingine eneo la Makunguru Jijini Mbeya Vyumba 12 vya biasharaa
viliteketea kwa moto jana majira ya saa Tano asubuhi vilivyokuwa vimetoka
kujengwa mali ya Dominick Mbinga Mkazi wa Dar Es Salaam.
Hata
hivyo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza baada ya moto huo kudhibitiwa
kwa ushirikiano baina ya kikosi cha zima moto na uokoaji na wananchi.
Thamani halisi ya uhalibifu bado kujulikana
pamoja na chanzo ingawa kwa mujibu wa majirani walisema inawezekana ikawa ni
hitilafu ya umeme kutokana na muda huo wapangaji wa nyumba hiyo kutokuwepo
wakati moto ukitokea ambao ulijulikana baada ya majirani kuona.
.....................................................................................................................
DKT. MUKANGARA ATAJA WAJUMBE WA KAMATI YA USHINDI WA TAIFA STARS WATAJWA
Kama
mnavyofahamu, hivi sasa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu kwa Wanaume
(Taifa Stars) ipo kwenye michuano ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe
la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Katika
Afrika, Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C kati ya makundi 10.
Kundi C linajumuisha timu za Ivory Coast, Morocco, Gambia na Tanzania.
Kwa
sasa katika kundi C, Taifa Stars inashika nafasi ya pili ikiwa na alama
sita (6), nyuma ya Ivory Coast yenye alama saba (7), Morocco ina alama
mbili (2) na Gambia ina alama moja(1).
Kwa
mara nyingine Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapenda
kuwapongeza Taifa Stars, kwa kazi nzuri ambayo wameishaifanya ikiwemo
ushindi wa Bao Tatu kwa Moja dhidi ya Morocco. Watanzania wote na Wadau
wa Soka nchini wamefurahishwa sana na mafanikio yaliyofikiwa na Taifa
Stars na yenye kutupa matumaini katika kuitayarisha Taifa Stars kufuzu
kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014 nchini Brazil.
Kwa
hali ilivyo hivi sasa, Taifa Stars ipo katika nafasi nzuri ya kufuzu.
Ili Tanzania tuweze kufuzu, Taifa Stars inatakiwa ishinde mechi zote
tatu (3) na kuongoza kundi C na baadae iingie katika Timu kumi (10) bora
na kisha zipatikane Timu tano (5) kutoka Afrika ambazo zitakuwa
zimefuzu kwenda Brazil katika Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014.
Tunaamini hili linawezekana.
Sasa
kwa kuzingatia uzito wa jukumu lililo mbele yetu na kwa Taifa Stars kwa
ujumla; Serikali imeunda Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars.
Jukumu
la msingi la Kamati tunayoiunda ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa
na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha
kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati ya
Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa
wafuatao:-
1. Mhe Mohamed Dewji - Mbunge
2. Bi. Teddy Mapunda - Montage
3. Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
4. Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT
5. Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel
6. Bw. George Kavishe - TBL
7. Mhe. Mohamed Raza - Zanzibar
8. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
9. Bw. Joseph Kusaga - Clouds
10. Mhe. Kapt. John Komba - Mbunge
11. Mhe. Zitto Kabwe - Mbunge
Kamati
hii iliyoteuliwa leo, naomba ianze kazi mara moja. Hadidu za rejea
zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati
itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa.
Serikali
inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii
inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote
zilizombele yetu.
Aidha
nichukue fursa hii kutoa wito kwa Watanzania wote, kuiunga mkono Taifa
Stars na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars kwa hali na mali katika
kuhakikisha timu yetu inafuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu naomba
niwasilishe salaam zao za kuwapongeza Vijana wetu wa Taifa Stars,
pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Kim Poulsen. Kwa
pamoja wanaomba Taifa Stars iendelee kujipanga kwa mechi zijazo.
Nawahakikishia kuwa Serikali, Watanzania na wadau wa Soka nchini wapo
nyuma yao.
Mungu Ibariki Taifa Stars. Mungu Ibariki Tanzania.
Dkt. Fenella Mukangara (Mb)
WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
16 Aprili, 2013
...................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment