Monday, June 3, 2013

Ajali mbaya imetokea katika kijiji cha katumba eneo la wanaposimama trafki wa Tukuyu maarufu kama kwa mwambenja, ambapo mwendesha bodaboda mmoja maarufu kama Juta mkazi wa KK muuzaji wa Spea za pikipiki alikuwa akijaribu ku- overtake gari aina ya costa T347AWD bila kuangalia mbele yake kuna gari nyingine inayokuja hali iliyopelekea kugongana uso kwa uso na gari hiyo na hatimaye kusagwasagwa na kufariki hapo hapo

MASALIA YA PIKIPIKI BAADA YA KUROKEA AJALI MBAYA ILIYOHUSISHA PIKIPIKI NA GALI DOGO NA COSTA
MAREHEMU MWENDESHA BODABODA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA TU LA JUTA AKIWA AMEFARIKI VIBAYA HUKU KICHWA NA MHUU MMOJA VIKIWA HAVIPO VIKIWA VIMESAGWASANGWA

GALI LA WAGONJWA LIKIONDOKA NA BAADHI YA MAJERUHI
PAMOJA NA KUJITAHIDI KUMKWEPA WA PIKIPIKI HAIKUWA RAHISI SANA HADI GALI HILI LILILOKUWA NA ABILIA 29 KUSIMAMA KWENYE KIFUSI CHA MCHANGA NA VICHAKA
................................................................................................................................................................

  WANAWAKE MSISUBIRI KUWEZESHWA DEREVA: MWANAMKE WA BASI LA NDENJELA COACH AWA KIVUTIO KWA ABIRIA WA SAFARI ZA MBEYA KWENDA DSM

DEREVA NUSURA MAGULUKO 28 AKIMWOMBA MUNGU KABLA YA KUANZA SAFARI
SASA HAPA YUPO KAZINI
BAADHI YA ABIRIA WAKIFURAHIA MWENDO MZURI WA DEREVA NUSURA MGULUKO

ABIRIA WAKIPATIWA HUDUMA YA VITAFUNWA NDANI YA BASI HILO LA NDENJELA
WAFANYAKAZI WA BASI LA NDENJELA KABLA YA KUANZA SAFARI
MABASI YA NDENJELA NIYAKISASA YANAFANYA SAFARI ZAKE MBEYA  DSM KILA SIKU

 .........................................................................................................

KAMPUNI YA COCA COLA MBEYA YAKARABATI KITUO CHA POLISI IYUNGA JIJINI MBEYA


Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Barakaeli Masaki wakipeana mkono na Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya cocacola  Lovis Cotyee mara baada ya kukabidhiwa kituo hicho


Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika kuimlaisha ulinzi na usalama katika jiji la mbeya.

Mkuu wa kituo cha Polisi Iyunga Laison Kasimbilu
Akizungumza katika makabidhiano ya kituo cha polisi Iyunga jijini Mbeya  Ndugu Haji Ally Promosheni Meneja kutoka  Kampuni vinywaji baridi ya Coca cola ambayo imefadhili ukarabati wa kituo hicho kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 10 amesema wao kama kampuni wametoa msaada huo kwa lengo kurudisha kile walicho kipata ndani ya jamii.Baadhi ya wakazi wachache waungwana wa Iyunga walishuhudia tukio hilo

Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali na wananchi  mkoani mbeya kuhakikisha wanatoa michango yao katika kuhakikisha jeshi la polisi linaendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa jamii.
  
Michango hiyo ni pamoja na kujenga vituo vya Polisi na ukarabati ambao utaweza kutoa fursa kwajeshi hilo kufanya kazi kwa bidii katikakuhakikisha jamii inaendelea kuishi maeneo salama na tulivu.
  
Akizungumza katika makabidhiano ya kituo cha polisi Iyunga jijini Mbeya  Ndugu Haji Ally Promosheni Meneja kutoka  Kampuni vinywaji baridi ya Coca cola ambayo imefadhili ukarabati wa kituo hicho kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 10 amesema wao kama kampuni wametoa msaada huo kwa lengo kurudisha kile walicho kipata ndani ya jamii.
Amesema yapo maeneo mbalaimbali ambayo wameweza kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu .afya  pamoja na maeneo mengine hivyo kitendo cha wao kusaidia jeshi hilo la polisi ni kama muendelezo wa matukio yanayo fanywa na kampuni hiyo .
 Meneja huyo ameyataka mashirika mbalimbali mkoani humu kuhakikisha wanasaidia maeneo yanayo hitaji misaada kama ambavyo wao wameweza kuonyesha mfano kwa kukarabati kituo hicho cha Iyunga ambacho awali kilikuwa katika hali mbaya.
  
Amebainisha kuwa msaada huo haujaishi kwa jeshi la polisi pekee kwani bado kuna maombi mbalimbali ndani ya jamii ambayo yanahitahi kupatiwa misaada kutoka katika kampuni hiyo hivyo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wao katika kuijenga  jamii ya mkoa wa mbeya.
Kwa uapande wake kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika kuimlaisha ulinzi na usalama katika jiji la mbeya.
Amesema mchangho ulio tolewa na Kampuni hiyo ni mkubwa kwani umeweza kuboresha mazingira bora ya kituo hicho na kulifanya jeshi hilo kufanya kazi zake  kwa usanifu.

Pia amezitaka taasisi mbalimbali pamoja na mashirika mengine kuendelea kutoa michango yao kwa jeshi la polisi mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuimalisha vituo vingine vya polisi ambavyo hali yake hairidhishi.

Picha na Mbeya yetu
.....................................................................................................................................................

UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA MPYA KUFANYIKA LEO KARIMJEE

Karimjee
Ili kuwafikia wananchi wengi, uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika leo, Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana  katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam utarushwa moja kwa moja na vituo vya TBC1, TBC Taifa, ITV, Star TV, Channel Ten, ZBC TV na ZBC Redio. Wadau hawa wamekubali kufanya hivyo baada ya kuombwa.

Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo hivyo kuanzia saa 8:00 mchana.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo.
.....................................................................................................................

POLE SANA MR BEDO MWAKAJE KWA MFULULIZO WA AJALI KATIKA BIASHARA YAKO YA USAFIRISHAJI MBEYA , LWANGWA  NA KYELA
 


 
Post a Comment