Tuesday, June 18, 2013

HALMASHAURI YA BUSOKELO WATOA MAPENDEKEZO YAO YA JINSI YA KUUGAWA MKOA WA MBEYA, MAKAO MAKUU YA MKOA KUWA KATIKA MJI WA TUKUYU WILAYANI RUNGWE NA HALMASHAURI YA BUSOKELO KUKUBARIKA KUWA WILAYA NA MAKAO MAKUU KUWA KATIKA MJI WA LWANGWA

 
RAMANI INAYOONYESHA HALMASHAURI YA BUSOKELO

KARIBUNI BUSOKELO NI SEHEMU YENYE VIVUTIO VYA KIUTALII NA ARDHI YENYE RUTUBA KWA UWEKEZAJI KWA KILIMO NA UCHIMBAJI WA MADINI

OFISI YA HALMASHAURI YA BUSIKELO

MWENYEKITI  WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSON MWAKIPUNGA AKIONGEA NA WATENDAJI NA MADIWANI WA BUSOKELO NI JINSI GANI YA KUTOA MAON YATAKAYO KUWA NA NGUVU YA HOJA ILI MCHAKATO WA KUUGAWA MOA WAMBEYA MAKAO MAKUU YAKE YAWE KATIKA MJI WA TUKUYU WILAYANI RUNGWE NA KUWA SASA ENEO LA HALMASHAURI YA RUNGWE LIWE NI WILAYA ITAKAYO JITEGEMEA

MAKAMU MWENYEKITI WA BUSOKELO AKIONGEA NA WATENDAJI NA WAHESHIMIWA MADIWANI

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIONGEA NA MADIWANI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO NA WATENDAJI MALA BAADA YA KUSIKIA RIPOT ILIYOANDALIWA NA HALMASHAURI YA BUSOKELO NA HIVYO MKUU WA WILAYA AMEWASHUKURU SANA KWA HALMASHAURI YA BUSOKELO KUOMBA HALMASHAURI YA BUSOKELO KUWA WILAYA ITAKAYOJITEGEMEA KWA KUWA NIKWA MUDA MFUPI TANGU WAPEWE HALMASHAURI WANANCHI WA WATENDAJI WAMEKUWA NI WATU WA KUFANYA KAZI KWA MOYO HASA KATIKA KUPANGA MIUNDOMBINU YA ARDHI ILI MJI KUPANGWA MAPEMA KABLA HAUJAVAMIWA

WAHESIMIWA MADIWANI NA WATENDAJI WALIO HUDHURIA WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA KWA MAKINI RIPOT MAALUM YA KUUGAWA MKOA WA MBEYA

AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MR MASANJA AKISOMA RIPOT YA MAALUM YA MAPENDEKEZO YA KUUGAWA MKOA WA MBEYA KWA KUELEZA FURSA ZINAZOPATIKANA WILAYANI RUNGWE NA UZOEFU WA UONGOZI PIA WILAYA YA RUNGWE KUWA NA VIVUTIO VYA UTALII KAMA MLIMA RUNGWE AMBAO NI WA TATU KWA UREFU TANZANIA PIA VIVUTIO 19 AMBAVYO VINAPATIKANA WILAYANI RUNGWE TU

MHE DIWANI KATA YA ITETE GODWIN KOMBOTEKA AKITOA SHUKRANI KWA RAIS JK. KIKWETE BAADA YA KUTANGAZA KUANZA MCHAKATO HUU WA KUUGAWA MKOA WA MBEYA LAKINI KWA MHESHIMIWA KOMBOTEKA AKASEMA KUWA KWA KUMBUKUMBU ZILIZOPO RAIS HAJAKOSEA KWAKUWA WILAYA YA RUNGWE WALIANZA MCHAKATO WA KUOMBA MKOA TANGU MWAKA 1974 NA PIA AMESEMA FULSA ZIPO

WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO WAKIWA NA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA KIKAO MAALUM CHA KUGAWA MKOA WA MBEYA KUWA MIKOA MIWILI

..............................................................................................................................

BOSS WA MALAWI CARGO TAWI LA MBEYA AFIKISHWA MAHAKAMANI AKITUHUMIWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA YA NGONO


Bosi Mmalawi Evance Mwale akiongozwa na askari polisi kuingia katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Mbeya alikoshitakiwa kwa kosa la Rushwa ya Ngono na Ushawishi wa ngono, amerudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.


Askari Polisi wakimrejesha rumande Bosi Mmalawi Evance Mwale anayeshitakiwa kwa makosa ya Rushwa ya Ngono


ALIYEKUWA  Meneja wa Kampuni ya Malawi Cargo tawi la Mbeya Evason Mwale(49) raia wa nchi jirani ya Malawi, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya akituhumiwa kujihusisha na Rushwa ya Ngono.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe akisoma Mashtaka ya mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuluo alisema Mtuhumiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni Rushwa ya Ngono kinyume cha kifungu cha 25 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007.
  
Namkambe alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa anashtakiwa kwa kosa lingine la matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha kifungu cha 31 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007.
  
Alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo April 11, Mwaka huu katika Hoteli moja iliyopo Iyunga Jijini Mbeya ambapo alikamatwa akitaka kujihusisha na rushwa ya Ngono na Mke wa Mfanyakazi wake.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Ndeoruo aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 1, Mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza ambapo pia alisema Dhama iko wazi kwa Mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili wenye hati za mali isiyohamishika yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, Barua zinazotambuliwa na mamlaka, ambapo pia mtuhumiwa  anatakiwa kuacha hati zake za kusafiria na kutoruhusiwa kutoka nje ya Jiji la Mbeya bila ruhusa ya mahakama.
Awali  ilidaiwa kuwa Meneja huyo alitaka kujihusisha na Rushwa na Mke wa Mfanyakazi wake wa nyumbani ambaye alimfukuza kazi na baadaye alimtumia Mkewe ili amrudishe kazini baada ya kufanya naye mapenzi.
Na Mbeya yetu
....................................................................................................................

No comments: