|
KAZI IMEANZA TAYARI |
|
KAZI IKIENDELEA HUKU MWENDESHA BODABODA AKIWA HAFUATI SHERIA KAMA KAWAIDA YAO HAWA WATU PAMOJA NA KUONA ALAMA ZA KUWA KAZI INAENDELEA NA KUFUNGWA KWA BARABARA HII LAKINI HAWAJARI |
|
UJENZI WA BARABARA YA KUTOKA TUKUYU MJINI KUELEKEA LWANGWA BUSOKELO NA KUFIKA KATUMBA TUKUYU IKIWA NI AHADI YA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIWA KATIKA KAMPENI ZA URAIS IMEANZA KUTEKELEZWA KWA KUJENGWA KWA AWAKU NA WATATU WAKIWA KATIKA KAZI |
.....................................................................................................................
MGOGORO WA BIASHARA YA USAFIRISHAJI YA GALI AINA YA HAICE NA NOAH MJINI TUKUYU WAPATIWA UFUMBUZI
|
SSP BUTUSYO MWAMBELO RTO MBEYA AKIFAFANUA SHERIA MPYA YA SUMATRA YA JINSI YA KUENDESHA BIASHARA YA USAFIRISHAJI HASA KW GALI ZA ABILIA AINA YA NOAH SEHEMU ZA MIJINI |
|
SHERIA YA MPYA YA SUMATRA YA NINI KINATAKIWA ILI KUKUBARIWA KUFANYA BIASHAYA YA GALI AINA YA NOAH |
|
MADEREVA NA WAMILIKI WA MAGARI YA DALADALA TUKUYU, USHIRIKA NA KIWIRA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI RTO WA MBEYA SSP BUTUSYO MWAMBELO AKIWAELEZA MAMBO MAMBO MBALIMBALI HASA KUFANYA BIASHARA KWA KUFUATA SHERIA ZA NCHI |
|
MAGALI YA DALADALA YAKIWA YAMEPAKI BAADA YA WATU WENGI KUYASUSIA KUPANDA KWAKUWA MENGI NI CHAKAVU PIA UWEPO WA USAFIRI WA GALI AINA YA NOAH KURAHISISHA SAFARI NA PIA NI MAGALI YA KISASA HIVYO HUKIMBILIWA NA WATU KUPANDA |
|
DALADALA AINA YA NOAH IKIWA IMEPAKIA ABILIA WAKE NA KUONDOKA KUELEKEA KIWIRA TUKUYU |
|
GALI AINA HII ZIKIWA FOLENI NA BILA YA WATU KUPANDA NA KUWA SEHEM YA KUANIKIA NGUO STANDI MPYA TUKUYU MJINI |
|
MPAKA KINGOTANZANIA NAONDOKA KATIKA UKUMBI HUU WA CCM AMBAPO WAMIRIKI NA MADEREVA WA DARADARA TUKUYU, KIWIRA KATUMBA NA USHIRIKA WALIENDELEA NA MAFUNZO YA KUFUATA SHERIA KATIKA BIASHARA YA USAFIRISHAJI KUTOKA KWA SSP BUTUSYO MWAMBELO RTO MBEYA NA WADAU WA USAFIRI PIA WALIPATA NAFASI YA KUULIZA MASWALI MBALIMBALI YA UFAHAMU WA BIASHARA YA USAFIRISHAJI |
.............................................................................................
na Christopher Nyenyembe, Mbeya
|
|
|
MRADI mkubwa wa ujenzi wa Soko jipya la Mwanjelwa ulioanza baada
ya soko lililokuwapo kuteketezwa kwa moto mwaka 2006, umekwama
kumalizika kutokana na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kuishiwa fedha.
Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini kukwama kwa ujenzi wa soko hilo
katika hatua za mwisho huku timu ya wataalamu kutoka Benki ya CRDB
iliyotoa mkopo wa sh bilioni 13 wakihaha kufuatilia deni lao.
Benki ya CRDB iliikopesha Halmashauri ya Jiji la Mbeya fedha hizo ili
kufanikisha ujenzi wa soko hilo na mkopo ulitakiwa utumike ndani ya
miaka mitano na baada ya hapo jiji hilo lianze kurejesha mkopo huo na
riba.
Kushindwa kukamilika kwa soko hilo ambalo ni kitega uchumi kikubwa
katika halmashauri ya jiji hilo kumeibua hisia tofauti huku baadhi ya
wafanyabiashara wakilalamikia uzembe uliofanywa na mkandarasi, Kampuni
ya Tanzania Building Works Ltd (TBWL).
Mkurugenzi wa Tawi la CRDB Mbeya, Benson Mwakyusa, alisema ingawa si
msemaji alikiri kupokea ugeni kutoka CRDB makao makuu na kwamba walikuwa
na jukumu la kufuatilia masuala mengine ya kikazi na kukutana na
mkopaji ambaye ni halmashauri ya jiji hilo, ili kuangalia njia nyingine
ya kukamilisha ujenzi wa soko hilo.
Mhandisi mshauri wa ujenzi wa soko hilo, Dudley Mawalla, kutoka
Kampuni ya MD Consultancy Limited alipohojiwa ili aeleze hali
iliyosababisha ujenzi wa soko hilo usimame, naye aliruka na kudai kuwa
si msemaji na anayetakiwa kusema ni mmiliki wa soko hilo ambao ni Jiji
la Mbeya.
Mkurugenzi wa jiji hilo, Musa Zungiza, alikiri mkandarasi aliyepewa
kazi ya ujenzi wa soko kushindwa kumalizia ujenzi licha ya kuomba
aongezewe muda ambao nao ulimalizika na ndipo walipogundua kuwa
aliishiwa fedha na ameshindwa pia kutimiza masharti waliyokubaliana.
“Sisi kama jiji hatumdai hadi pale alipofikia, kweli alituomba fedha,
tulimuomba atupatie mpango mzima wa kazi na mtiririko wa fedha kutoka
benki, tumefikia mahali tumekosana kwa kuwa hajatimiza masharti na
tumezungumza na mhandisi mshauri ili tuone jinsi ya kumpata mkandarasi
mwingine,” alisema Zungiza.
.............................................................................................................
Bw.
Richard Engel kutoka NBC News mmoja kati ya waandishi wanne walioalikwa
na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kueelezea uzoefu wao na mikikimikiki
wanayokumbana nayo wanapotekeleza majukumu yao ya kiuandishi. Bw. Engel
ambaye amesema amewahi kutekwa, alilitaka Baraza Kuu la Usalama
linapojadiliana kuhusu dhana nzima ya usalama wa waandishi, kujadili pia
ni nani hasa mwandishi wa habari anaye stahili ulinzi na akahoji kama
wanaharakati ambao nao wanachukua picha za matukio mbalimbali na
kuzipost kwenye blog kama nao ni waandishi wa habari. pembeni yake ni
Bi. Kathleen Carroll, ambaye ni mhariri mtendaji wa Associated Press na
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kulinda Waandishi ( CPJ) yeye
katika mchango wake alisema licha ya kwamba waandishi wengi wanapoteza
maisha wakati wakitafuta habari kwenye maeneo yenye migogoro lakini
waandishi watano kati ya sita wanauawa ndani ya nchi zao wakati
wakitimiza majukumu yao.
.................................................................................................................
|
|
No comments:
Post a Comment