Sunday, July 21, 2013

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA SIKU MOJA WA TROIKA YA SADC JIJINI PRETORIA, AFRIKA KUSINI

p1 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC Mhe  Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt  Tomaz Augusto Salomão na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah
p2
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku.
p3
 Mwenyekiti wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Armando Guebuza baada ya mkutano wa kamati ya Troika  katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku.
p4  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
p5 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation). Kutoka kulia ni Mwenyeiti wa Chama cha Wataalam Watanzania waishio Afrika Kusini, Dkt Hamza Mokiwa, Mwenyekiti wa Tanzania Women in Gauteng (TWIGA), Mama Scholastica Kimario, Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe Radhia Msuya, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Afrika ya Kusini Bw. Deusdedit Rugaiganisa na Bw. David Mataluma, mratibu wa Vijana katika Jumuiya ya Watanzania.
p6 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na balozi pamoja na maofisa wa ubalozi muda mfupi kabla ya kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
p7 (1) 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomndoka  leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
p8 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya  leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
PICHA NA IKULU

  ..............................................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum kabla ya kuondolewa katika uwanja wa jeshi
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni
 
Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum kabla ya kuondolewa katika uwanja wa jeshi 
Baadhi ya askari wa JWTZ wakifunika majeneza ya askari hao kwa bendera ya taifa mara baada ya kushushwa kwenye ndege maalum 
Baadhi ya wanajeshi na wahudumu wa ndege wakishusha miili ya wanajeshi wa JWTZ waliouwawa Darfur hivi karibuni 
Baadhi ya maofisa wa JWTZ na maofisa wa UN waliosindikiza miili ya wanajeshi wa JWTZ waliouwawa Darfur wakishuka kwenye ndege 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni 
Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam 
Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur 
Baadhi ya wananchi waliofika kupokea na kushuhudia mapokezi hayo ya miili ya mashujaa wetu 
Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege 
Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akishikiliwa na wenzake wakati akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege 
Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima 
 
Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria 
Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo. 
Na www.sufianimafoto.com 
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla.  Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi. 
Mbali na Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, ni pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete. 
Mara baada ya kuwasili miili hiyo iliongozwa na msafara kuelekea hospitali ya rufaa ya Jeshi, Lugalo, kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi siku ya Jumatatu Julai 22, 2013 itakapoagwa rasmi kwa heshima zote katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es Salaam, ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi Mkabala na Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. 
Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.

No comments: