Tuesday, July 16, 2013

WAANDISHI WA HABARI WAPONGEZWA LAKINI VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FULSA ZA SERIKALI

habari 1
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa akifungua mkutano kati ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam leo kushoto ni msemaji wa Wizara hiyo Bw. Godlease Malisa na kulia ni Prof. Elisante Ole Gabriel wa Wizara hiyo habari 3
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Bw. Godlease Malisa akizungumza na vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa azma ya Serikali kusaidia Vijana, jumla ya shilingi Bilioni 6.1 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2013 kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam leo, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.

Tunatambua kwamba hivi karibuni Serikali ilipitisha bajeti yake kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Vijana ambayo imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa ajira,hata hivyo
Serikali imekuwa ikifanya jitihada za makusudi ili kuhakikisha inamkwamua kutoka katika janga la umasikini.

Katika kutekeleza azma ya kusaidia Vijana, jumla ya shilingi Bilioni 6.1 zimetengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2013 ikiwa ni kwa ajili ya kusaidia mfuko wa Maendeleo ya Vijana, ambapo Vijana watapatiwa mikopo yenye unafuu katika riba na upatikanaji wake. Natoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa hii ambayo haimuhitaji mkopaji kuwa na dhamana isiyo hamishika bali kuwa na uaminifu wa kurejesha mkopo huo na kujiunga kwenye SACCOS.

Kwa kutambua umuhimu wa vijana katika maendeleo ya taifa letu, Serikali iliamua kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana mnamo mwaka 1993/94, chini ya Sheria Na. 21 ya mwaka 1961 kifungu cha 17(1), ukiwa  na lengo la kuwasaidia Vijana kupata mikopo yenye masharti nafuu na kuwajengea uwezo kiuchumi  ili waweze kuanzisha au kuimarisha miradi yao kwa lengo la kuwawezesha kujitegemea na kukuza uchumi wa nchi.

Takwimu zinaonyesha kuwa kuna jumla ya Vijana milioni 16,195,370 ambapo takribani vijana 1,200,000 humaliza elimu ya vyuo mbalimbali kila mwaka na kati yao ni vijana 200,000 huajiriwa kwa mwaka. Ikumbukwe kuwa Vijana wanachukua asilimi 68 ya nguvu kazi ya Taifa lakini takwimu zinaonyesha kuwa upungufu wa ajira kwa Vijana ni asilimia 14.4.
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuendesha mfuko huu tayari imeshapeleke muongozo mpya wa namna bora ya vijana kunufaika na mikopo katika Halmashauri zote nchini. Hivyo Vijana mnashauriwa kujiunga katika vikundi na kufanya mawasiliano na Maafisa Vijana katika Halmashauri zenu ili kujua taratibu za kupata mikopo hiyo.

Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano SerikaliniBw. Godlease Malisa ametumia fursa hii kuwapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuhabarisha umma hasa katika matukio makubwa yaliyotokea hivi karibuni nchini kwetu. Mmefanya kazi kubwa sana ya kutangaza mabadiliko ya ratiba ya Bunge la Bajeti kutoka Juni – Agosti na kuwa Aprili hadi Juni kila mwaka. Kadhalika mlitangaza ziara ya Rais Obama, ziara ya Rais wa Sri Lanka, Mkutano wa Smart partnership na Maonyesho ya Sabasaba.

Serikali imepokea kwa msikitiko kifo cha mwandishi mkongwe marehemu David Majebele aliyefariki jana alfajiri na msiba upo nyumbani kwake Sinza Plot Na. 262 Block E, Mtaa wa Lion Hotel, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi katika makaburi ya Kinondoni. Wizara inatoa pole na salam za rambirambi kwa ndugu, jamaa na familia ya Marehemu, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilianzishwa mwaka 2006. Wizara hii inaundwa na Idara nne za kisekta ambazo ni Idara ya Habari, Idara ya Maendeleo ya Vijana, Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Idara ya Maendeleo ya Michezo.

Imetolewa na
Bw. Godlease Malisa
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
......................................................................................................................................

 DR. MARY MWANJELWA AHAMASISHA WAPENDA MICHEZO KUUNDA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI NA KUWATAFUTIA WAFADHILIATOA LAKI TANO KKKT UYOLE

 Nani kama Mungu wetu mwema, aliniokoa kwenye ajali, mimi ni nani, lazima nimrudishie utukufu kwa kumwabudu na kuwatimukia watu.
 Siku nyingine mkiniita, mnitaarifu mapema nitawaleta na rafiki zangu hapa kanisani kwa ajili ya kusali na kuchangia.
 Asanteni sana kwa ukarimu wenu, sasa natoka naenda kwenye majukumu mengine.
 Lazima nimwimbie Mungu....
 Kwa kununua gari hili kwa lengo la kueneza Injili, mtabarikiwa....
 Mch. Mwakapalile wa kanisa la KKKT usharika wa Uyole Jijini Mbeya, akionesha tabasamu la furaha baada ya Dr. Mwanjelwa kutoka kanisani ambako alimtamkia maneno ya baraka.
 Baadhi ya wanakwaya wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa viti maalum(CCM) Mkoa wa Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa.

KIPANYA LEO...!



kp06062013 5623e

  ........................................................................

MISAADA ZAIDI YAENDELEA KUTOLEWA KWA MTOTO ALIYEFUNGIWA NDANI MIAKA MIWILI.

 Christian Mwakapusya Mtanzania anaeishi Marekani  akiwa amembeba mtoto Joshua Joseph baada ya kumtembelea nyumbani kwao Iyunga Jijini Mbeya
 David Mwakapusya ambaye alifuatana na Baba yake akitoa msaada wa nguo kwa mtoto ambaye hakufahamika jina lake kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mtaani hapo.
 Baadhi ya Majirani wa familia ya Joshua wakiwa na nguo walizopewa na Christian Mwakapusya
 Christian Mwakapusya akizungumza na mama mlezi wa mtoto Joshua Joseph Nyumbani kwake Iyunga Jijini Mbeya.
Christian Mwakapusya akizungumza na Amina Mwasankinga aliye simamishwa masomo kwa kisingizio cha ushirikina alipo kutana nae 
 
MTANZANIA anayeishi Marekani Christian Mwakapusya aliyeguswa na kitendo alichofanyiwa  mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili kufungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Kutokana na kuguswa na tukio hilo Mtanzania huyo amelazimika kumtembelea Nyumbani anakoishia na kujionea hali halisi aliyonayo mtoto huyo kwa sasa.
Akizungumza kwa masikitiko nyumbani kwao eneo la Iyunga Mwakapusya amesema Wazazi wanaofanya vitendo kama hivyo wanapaswa kulaaniwa na kukemewa.
Mwakapusya aliyekuwa amefuatana na Mtoto wake wa Kiume David waliofunga safari kutoka Marekani hadi Mbeya kumwona Mtoto huyo wametoa zawadi mbali mbali zikiwemo Nguo na fedha taslimu alizokabidhiwa Mama mlezi pamoja na Balozi wa Nyumba kumi.
Mhanga wa tukio hilo, Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Balozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaakwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Wakati huo huo Msamaria mwema huyo kutoka Nchini Marekani pia amezungumza na Mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Amina Mwasankinga ambaye alifukuzwa Shule kwa kisingizio cha Ushirikina.
Aidha amemuahidi kumsaidia ili aweze kumaliza masomo yake huku akilaani vikali kitendo cha Walimu wa Shule ya Hollwood ya Wilayani Mbozi kuamini imani za Kishirikina na kumharibia masomo Mwanafunzi huyo.

No comments: