Sunday, July 14, 2013

MZIMU WA MKOA MPYA WA SONGWE WAENDELEA KUWATESA WANAMKOA MPYA; MAPYA YAIBUKA KUHUSU MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA WA SONGWE.

Mbunge wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona  ambaye pia alikuwepo katika Mkutano huo alisema kwa niaba ya Wananchi wa Ileje hayuko tayari kukubaliana na maamuzi ya Kupeleka Makao makuu Mkwajuni Wilayani Chunya. 

Wananchi wa ileje wakiwa katika kongamano hilo katika hoteli ya Kiwira Motel
Wakazi wa Wilaya ya Ileje wanaoishi mikoa ya Iringa,Njombe,Rukwa na Mbeya Mjini,kwa pamoja wamemuomba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuona umuhimu wa kubadilisha mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya iliyopendekeza makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe yawe eneo la Mkwajuni wilayani Chunya,kwa madai kuwa ni mbali ukilinganisha na Jiografia ya wilaya ya ileje.
Wananchi wa wilaya ya Ileje wametoa maombi yao wakati wa Kongamano lililoshirikisha wakazi wa ileje wanaoishi Nje ya wilaya hiyo,lililofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel Jijini  Mbeya,wakijadiliana maendeleo ya wilaya hiyo pamoja na mgawanyo wa mkoa wa Mbeya na kupata mkoa mwingine mpya,ambao wameomba mapendekezo ya makao makuu ya mkoa huo yasogezwe.
Wakizungumza katika Mkutano huo Wananchi hao wamedai kuwa umbali kutoka Wilayani Ileje kwenda Mbeya Mjini ni mbali sana hivyo kuwapeleka Mkwajuni ni kuzidi kuwaongezea safari zaidi.
 Yohana Seme Mkazi wa  Ileje amesema lengo la kugawanya Mkoa ni kusogeza huduma kwa Wananchi lakini Mapendekezo ya Kupeleka Makao makuu ya Mkoa Wilayani Chunya ni kupokonya huduma kwa Wakazi wa Ileje ambao huduma nyingi hutegemea Nchi jirani ya Malawi.
Mjadala wao wanaileje ukaenda mbali zaidi,baada ya mapendekezo ya awali ya wajumbe wa kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya,kupendekeza makao makuu ya mkoa wa Songwe yawe ni Mkwajuni Kilometa 321 kutoka kusini mwa wilaya ya Ileje.
Kutokana na umuhimu wa Kongamano hili,Mbunge wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona  ambaye pia alikuwepo katika Mkutano huo alisema kwa niaba ya Wananchi wa Ileje hayuko tayari kukubaliana na maamuzi ya Kupeleka Makao makuu Mkwajuni Wilayani Chunya.

Kibona amesema mapendekezo ya Wanaileje ni kwamba Makao makuu ya Mkoa wa Songwe yasogezwe na kuwekwa katika kijiji cha Henje wilayani Mbozi, mapendekezo ambayo yameungwa Mkono na Wakazi wa Momba, Mbozi na Ileje yenyewe.
Na Mbeya yetu
......................................................

kipanya leo


kipanya 8cce3
(HM)
 ....................................................................
Post a Comment