Saturday, August 3, 2013

MBEYA BADO HAWAKOMI NA MAJANGA YA MOTO: BAADA YA LORI LA MAFUTA KUPINDUKA MBALIZI ,WANANCHI WAPIGANA VIKUMBO KUGOMBEA MAFUTA .

 Lori lenye namba za usajili  T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia

Lori  likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Magari yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo


YALE YALE!!! Wananchi  wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka 
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka

Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji 
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali

Kushoto ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba mafuta yasiendelee kuvuja
Tingo wa Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.

Ezekiel Kamanga
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.

  ......................................................................

MADIWANI NA WAKUU WA IDARA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WATIMULIWA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA MAHESABU

KAMATI ya bunge ya hesabu za (LAAC) jana ililazimika kuwatimua kwa muda madiwani na wakuu wa idaya za halmashauri ya jiji la Mbeya kwenye kikao cha kupitia taarifa za matumizi ya fedha za umma kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 
 
Kamati ililazimika kuwaondoa kwenye kikao watu hao kufuatia kuwepo kwa mkanganyiko wa maelezo kwenye vitabu vya taarifa za matumizi hayo ambapo vitabu vya wajumbe wa kamati vilikuwa na maelezo sawa na vile vya maofisa kutoka ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) lakini vikatofautiana na vitabu walivyokuwa nanvyo wakuu wa idara. 
 
Hoja ya matumizi ya kiasi cha shilingi milioni 104 kwaajili ya ukarabati wa mabweni ya Kawawa na Sokoine kwenye shule ya sekondari ya Iyunga iliyopo jijini hapa ndiyo iliyozua mgogoro na kukatisha kikao kwa muda.
 
Taarifa za CAG zilionesha zilionesha kuwa hadi ukaguzi unafanyika bweni moja lilikuwa limekarabatiwa lakini fedha zote zilionekana kutotumika bado huku pia kukiwa hakuna mkataba uliowekwa kati ya halmashauri na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo na muda wa mkataba haukujulikana. 
 
Katika harakati za kuijibu hoja hizo ndipo wakuu wa idara akiwemo mweka hazina James Jorojike na madiwani wakiongozwa na meya Athanas Kapunga walipoanza kujichanganya kwa kutoa majibu yanayokinzana hali iliyosababi mwenyekiti wa Laac Rajab Mohamed kuahirisha kwa muda kikao na kuomba madiwani na wakuu wa idara watoke nje ya ukumbu kuanzia saa 7:40 hadi saa 8:9 mchana.
 
“Tuna takriban hoja 25,bado tupo kwenye hoja moja ambayo tumeshindwa kukubaliana.
 
Taarifa mliyompa ninyi wenyewe CAG inaonesha bweni moja limekarabatiwa lakini fedha zote zipo.
 
Tunataka kujua fedha mlizotumia mlitoa wapi.Ninyi manasema mabweni yote yamekarabatiwa na fedha zimetumika.
 
Naomba tubaki wabunge tujadiliane tuone nini kifanyike” alisema Mohamed kabla ya kuwatoa nje madiwani na wakuu wa idara. 
 
Hata hivyo baada ya kurejea ukumbini,mwenyekiti huyo alisema wabunge walikubaliana kutoa maagizo siku ya maazimisho ya ziara yote kwa mkoa wa Mbeya itakayofanyika Agosti 3 mwaka huu katika ofisi ya mkoa.

 

  ...................................................................

MAONESHO YA NANE NANE LEO NI SIKU YA MKOA WA MBEYA , BURUDANI ZAENDELEA.

 KAIMU MKUU WA MKOA WA MBEYA MHESHIMIWA DEODATUS KINAWIRO AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA YA CHUNYA (MWENYE BAGARASHIA) AKIWA MEZA KUU PAMOJA NA WAGENI WENGINE.
 AFISA KILIMO WA MKOA WA MBEYA AKIELEZA KUHUSU KILIMO NA MIFUGO KWA MKOA WA MBEYA.
 BAADHI YA MAZAO YANAYOPATIKANA MKOANI MBEYA
 MC WA SHUGHULI ZA LEO CHARLES MWAKIPESILE AMBAYE PIA NI MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA MBEYA , AKIENDELEA NA SHUGHULI ZAKE.
 WASHIRIKI WALIHUDHURIA SIKU YA MKOA WA MBEYA WAKIFUATIA KWA MAKINI KINACHOENDELEA KATIKA UKUMBI WA JKT NANE NANE 

 NGOMA MBALIMBALI ZINAZO PATIKANA MKOA WA MBEYA ZIKITUMBUIZA KATIKA SIKU HII
MWENYEKITI WA HALIMASHAURI YA MBEYA VIJIJINI PAMOJA NA TIMU YAKE WAKIFUATILIA KWA MAKINI
KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MBEYA AKIONGEA NA WASHIRIKI  
KAIMU MKUU WA MKOA WA MBEYA MHESHIMIWA DEODATUS KINAWIRO AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AKIHUTUBIA WASHIRIKI NA WAKULIMA  WA MKOA WA MBEYA
BAADHI YA WANAHABARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI WAKIFUATILIA  MATUKIO MBALIMBALI
 VYAKULA MBALIMBALI VYA MKOA WA MBEYA
 MGENI RASMI AKIANGALIA KITOWEO AINA YA PANYA , WENYEJI WA MKOA WA MBEYA WANAKIITA MBEBHA
 WAKIFURAHIA BAADA YA KUONA KITOWEO AINA YA PANYA

KULIA MWENYEKITI WA HAL,ASHAURI YA RUNGWE AKISHUHUDIA NGOMA ZA ASILI ZIKITUMBUIZA

PICHA NA JEM
Post a Comment