Sunday, August 4, 2013

WILAYA YA RUNGWE NA MVUA ZA MWAKA MZIMA;...

LEO TUKUYU MKOANI MBEYA

WENYEJI WA RUNGWE WANASEMA SIO KAWAIDA SANA KUNYESHA MVUA ZA MASIKA KIPINDI CHA MWEZI WA NANE NA HII INATOKANA NA MABADIRIKO YA HARI YA HEWA HIVYO KUIFANYA RUNGWE KUWA NA KIANGAZI CHA MWEZI MMOJA MWEZI WA KUMI

WATU WENGINE WANASEMA KWAKUWA MISITU MINGI ILIHARIBIWA SANA KWA KUVUNWA NA SASA WATU WAMEPANDA SANA MITI NA KUTUNZA MISITU YA ASILI SASA HARI YA HEWA IMERUDI KAMA ZAMANI KWA RUNGWE KUWA NA MVUA KWA MSIMU WA MWAKA MZIMA

LEO NI SIKU YA TANO TANGU HARI YA HEWA YENYE BARIDI , UKUNGU NA MVUA NA IKIWA NI MWAKA WA PILI KUNYESHA KWA MVUA KAMA HII KIPINDI HIKI CHA MWEZI WA NANE AMBAPO MWAKA JANA 2012 MVUA KAMA HII ILINYESHA. HIVYO JITIHADA ZA UTAFITI ZINATAKIWA ILI KUJUA MSIMU WA KUPANDA MAZAO MBALIMBALI YANAYOENDANA NA MVUA HIZI

 .................................................

RAIS JAKAYA KIKWETE AMPONGEZA KIJANA HAMISI MOHAMED KWA MKUIBUKA BINGWA WA DUNIA KATIKA MCHEZO WA KURUKA KAMBA

Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye  awali
alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo  Dar es Salaam,
alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika
Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre
 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 
 Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
 Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
 Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
 Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa.
 
Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi
amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana
huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. 
Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki
kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani
Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili
huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika
Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480
kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo
jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo
alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa
amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa
usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania
ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini
kwao  na kuitangaza Tanzania.
Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika
kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea
katika kukiendeleza kipaji chake.
............................................................................

Clinton atua Dar kiaina


Rais Jakaya Kikwete akimpokea mgeni wake Rais mtaafu wa Marekeni Bill Clinton anayepanda gari (HM)

Rais wa Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton jana alifanya ziara katika makazi ya watu duni eneo la Vingunguti, wilayani Ilala Dar es Salaam, ambapo alikagua miradi midogomidogo ya wananchi inayofadhiliwa na mfuko wake (Bill Clinton Foundation).
Clinton alitembelea eneo hilo akitokea moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za Afrika kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.
Katika eneo hilo rais huyo mstaafu alipokewa kwa shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku baadhi ya wananchi wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi huyo kutembelea makazi yao.
Aidha, Clinton alipata wasaa wa kusalimiana na wakazi wa Vingunguti wakiwamo watoto ambao walishindwa kuzuia hisia zao wakijaribu kumsogelea, hali iliyomsukuma Clinton kuwasogelea na kuwasalimia kwa kuwashika mikono.
Maneno ya ‘Welcome Vingunguti Clinton‘ yalisisika kutoka kwa wananchi kuashiria kumkaribisha rais huyo wa 42 wa Marekani wakati alipowasalimia akitumia takriban dakika 15.
Clinton alikagua miradi ya midogomodogo ya wananchi iliyo chini ya mfuko wake ikiratibiwa na kutekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (Plan) pamoja na Benki ya Barclays kupitia Vikoba.
Miradi aliyokagua ni pamoja na saluni za kinamama, ushonaji na chips ambapo pia alishuhudia mmoja wa wanachama wa vikundi hivyo akikabidhiwa mkopo wa Sh100,000 ambaye alieleza mbele ya Clinton kuwa atazitumia kwa mradi wa maandazi, hali iliyomfanya rais huyo na umati wa watu uliohudhuria kucheka.
Akizungumza katika ziara hiyo Clinton alizishauri benki nchini, kuwekeza kwenye vikundi vya kuweka na kukopa (Vikoba) akieleza kuwa ndiyo mkombozi kwa wananchi hasa wanawake.
“Nimekuwa kwenye miradi hii kwa miaka 30 kabla sijawa rais, hivyo basi najua umuhimu wake. Benki zinatakiwa zisaidie Vikoba kwani vikundi hivyo huwafikia wananchi kwa haraka na wepesi hivyo basi kunahitajika njia mbadala za kuhakikisha vinakuwa imara,” alisema Clinton na kuongeza;
“ Raha ya maendeleo ni kuona watu wanajitegemea wenyewe katika shughuli za kujiingizia kipato.”
Mmoja wa wananchi walionufaika, Zainab Paul ambaye ni mwanachama wa Kikundi cha Amani Hisa alisema kuwa kupitia Mfuko wa Bill Clinton na Vikoba ameweza kujikwamua kimaisha ikiwamo kumlipa mtoto wake karo ya shule.
“Kikundi chetu kina wanachama 30 na huwa tunanunua hisa kwa Sh2000 na kila mwanachama anaruhusiwa kukopa zaidi ya mara tatu,” alisema Paul.
Clinton alieleza kufurahishwa kwake na hatua walizofikia wakazi hao wa Vingunguti akiwapongeza kinamama kwa jitihada zao na baada ya ziara hiyo alielekea Ikulu kwa mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete.
Awali, Mtendaji Mkuu wa Plan, Tanzania, Jorgen Haldorsen alisema shirika lake limekuwa likihudumia nyanja za kiuchumi na kijamii kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa kada ya chini wanapata huduma mbalimbali ikiwamo afya.
Naye, Mshauri wa Mambo ya Kujikimu wa Plan Stella Tungaraza aliwataka wananchi kujiunga zaidi na Vikoba na kwamba shirika lake limepanga kuanza kutoa mafunzo ujasiriamali kwa vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Baadaye Rais Clinton alitia saini makubaliano ya taasisi yake ya Bill Clinton Foundation kusaidia sekta ya kilimo nchini.
Makubaliano hayo yalitiwa saini Ikulu jijini Dar es Salaam na Sophia Kaduma ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Chakula pamoja na mwakilishi wa taasisi ya rais huyo mstaafu, Walker Morris.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Clinton alisema wakulima wa Tanzania wanatakiwa kutambua kuwa kuna nchi nyingine zinashindwa kuendesha shughuli za kilimo kutokana na uhaba wa ardhi au kuwa na ardhi isiyokuwa na rutuba na kuwataka watumie fursa hiyo kukuza uzalishaji wa kilimo .
Alisema kama wakulima hao watajituma Tanzania inaweza kuzalisha chakula ambacho kinaweza kulisha dunia. Chanzo: mwananchi
 
.................................................................................

NANE NANE SIKU YA 4: LIVE MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI YA NANE NANE MBEYA


 MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)  AKIWASILI KATIKA UWANJA WA NANE NANE MBEYA 
 MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKISAINI KITABU KATIKA JENGO LA MAPOKEZI

 MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITEMBELEA BANDA LA TANZANIA CHAMBER OF COMMERCE INDUSTRY   AND AGRICULTURE(TCCIA)

BANDA LA TANZANIA CHAMBER OF COMMERCE INDUSTRY   AND AGRICULTURE(TCCIA)

 MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)  AKISALIMIANA NA MWENYEKITI WA TCCIA DR. LWITIKO MWAKALUKWA 
 MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)  AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MWENYEKITI WA TCCIA DR. LWITIKO MWAKALUKWA 

MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITEMBELEA BANDA LA CRDB

MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)  AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MENEJA WA  CRDB MOBILE BANK  MAPUNDA 

MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)   AKIZUNGUMZA JAMBO KATIKA  BANDA LA CRDB 
MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)  AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MENEJA WA  CRDB MOBILE BANK NDUGU MAPUNDA


MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)  AKITEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)



MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB)   AKIPATA MAELEZO KWA AFISA HUDUMA NA ELIMU KWA WALIPAKODI BWANA PHILIPO ELIAMINI 

MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITEMBELEA BANDA LA BENKI KUU YA TANZANIA 
MENEJA MSAIDIZI WA IDARA YA UCHUMI  BENKI KUU TANZANIA MBEYA SUNGURA MASHINI AKITOA MAELEZO KWA  MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) 
MENEJA MSAIDIZI WA IDA
RA YA SARAFU  BENKI KUU TANZANIA-MBEYA  VICENT MTANI AKITOA MAELEZO KWA  MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) 
MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITAKA KUJUA JAMBO KUTOKA KWA  JAMBO KWA IBRAHIM MALOGOI WA IDARA YA BENKI KUU YA TANZANIA
MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITEMBELEA BANDA LA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE 

MKUU WA MKOA WA IRINGA MH.DR. CHRISTINE ISHENGOMA (MB) AKITEMBELEA BANDA LA 
TEOFILO KISANJI 



PICHA ZOTE NA Jem
 
............................................................................

MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKIWA KATIKA BANDA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOROJIA MBEYA.


MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKIPATA MAELEZO KATIKA BAADHI YA VIFAA NDANI YA BANDA HILO

MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKIFURAHIA JAMBO KATIKA BANDA HILO
MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKITAZAMA RAMANI ZA NYUMBA
BANDA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA

MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKITAZAMA MAELEKEZO NDANI YA BANDA HILO
MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA  AKITAZAMA GARI AMBALO LINATUMIA GESI
MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA  AKIPOKEA MAELEKEZO YA JINSI GARI HILO LINAVYOFANYA KAZI
HILI NDILO  GARI LINALOTUMIA GESI
MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKIELEKEA KATIKA ENEO  LA UMWAGILIAJI
HILI NI ENEO LA UMWAGILIAJI

MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA  AKIZUNGUMZA JAMBO
 MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA  AKITAZAMA SHUGHULI ZA UMWAGILIAJI.


MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA  AKITAZAMA BIDHAA MBALIMBALI ZINAZOTENGENEZWA NA VETA 

 BANDA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA NKASI



WADAU WAKITAZAMA MABANDA YA NKAS
 MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKITAZAMA BIDHAA MBALIMBALI

 BAADHI YA MAZAO KATIKA BANDA HILO LA  NKASI

MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA  AKITAZAMA KIKUNDI CHA BANADETHA KIPENDA  KIKUNDI CHA UPENDO 
 
BANDA LA HALMASHAURI YA SUMBAWANGA
MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKIPOKELEWA KATIKA BANDA LA SUMBAWANGA
MAZAO MBALIMBALI
MKUU WA MKOA WA RUKWA MH. ENG. STELLA M. MANYANYA AKITAZAMA MAZAO MBALIMBALI

 BANDA LA TCRA
 Mwanasayansi wa masafa Peter Kihogo  kushoto pamoja na wafanyakazi wengine wa TCRA wakitoa maelekezo kwa watu waliotembelea Banda hilo.

 Mwanasayansi wa masafa Peter Kihogo kushoto akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Eng Stella M. Manyanya 

 Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Eng Stella M. Manyanya akipata  maelezo kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa
 
 Meneja wa Uwanja Mzee Kasilati akitoa maelezo mafupi kwa mgeni Rasmi 
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akitoa taatifa ya majumuisho ya Mabanda aliyo Tembelea
............................................................................

Wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya elimu ya juu wakwama TCU

tcu 
Hussein Makame, MAELEZO
MAJINA ya wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2013/2014 yamekataliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kutokana na sababu  mbalimbali zilizojitokeza kwenye fomu zao za maombi.
TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekataa kuyachagua majina ya wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2013/2014  kutokana na sababu  mbalimbali zilizojitokeza kwenye fomu zao za maombi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Sifuni Mchome, wanafunzi hao hawakuchaguliwa na tume hiyo kujiunga na vyuo vikuu kutokana na maombi yao ya programu zote walizochagua kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa.
Ilieleza taarifa hiyo kuwa sababu za kutochaguliwa kwa wanafunzi hao ni pamoja na ushindani wa wanafunzi katika programu walizochagua, wanafunzi kushindwa kuwasilisha programu walizochagua na kuchangua programu ambazo hawana sifa nazo.
Hata hivyo, taarifa hiyo imewapa nafasi nyingine wanafunzi hao kuomba tena kwa awamu ya pili kwa kuchagua programu nyingine ambazo wana sifa nazo kupitia mfumo wa udahili wa TCU ambao umeshafunguliwa tangu Julai 29 hadi Agosti 9 mwaka huu utakapofungwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanafunzi anatakiwa kuangalia jina lake katika orodha ya wanafunzi ambao hawakuchaliwa na TUC, orodha inayopatikana kwenye tovuti ya taasisi hiyo ya www.tcu.go.tz na kufuata utaratibu uliowekwa kuomba upya.
“Baada ya mwanafunzi kuthibitisha jina lake kwenye orodha ya wanafunzi ambao hawakuchaguliwa iliyoko kwenye tovuti ya TCU, unatakiwa kufuata masharti yafuatayo, chagua program moja tu kutoka kwenye orodha ya programu inayopatikana kwenye tovuti ya TCU” alisema sehemu ya taarifa hiyo.
.....................................................................................
 

No comments: