Kamishna wa madini kitengo cha lesenwatano kutoka kulia akiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa uchimbaji madini wa Katundasi wilayani Chunya Mkoani Mbeya. |
Kwa sasa kuna kila
sababu kwa serikali kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata fursa ya mafunzo ya
uchimbaji ili kuweza kuwainua katika tasnia ya uchimbaji wa madini nchini.
Wito huo umetolewa
na Kamishana Msaidizi Kitengo cha Leseni
(Wizara ya Nihati na Madini), Mhandisi John Nayopa, katika Kituo cha mafunzo
kwa vitendo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo,
Matundasi, Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya ambaye alikua Wilayani humo kukagua na
kujionea miradi mbalimbali ya uchimbaji madini wilayani humo.
Mhandisi John Nayopa
amesisitiza kuwa kituo hicho kinahakikisha kina panua wigo wake kwa kujitangaza
ili watu wenye uhitaji wa mafunzo kufikiwa na kwamba hilo ndilo lengo la Wizara
ya Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla.
Alisema kuwa kituo
hicho kinatakiwa kutoa ushirikiano mzuri kwa serikali ili kuwepo na uratibu
mzuri kati ya kampuni inayo simamia kituo hicho na Wizara ya Nishati na Madini
ambao wote ndiyo wadau wakuu wa kituo hicho.
Naye Kamishana Masaidizi
wa Madini Kanda ya Kusini, Magharibi Mhandisi John Shija ameutaka uongozi wa Kampuni
hiyo kuhakikisha kituo kinafikia malengo yaliyowekwa na Wizara ya Nishati na
Madini ili kuleta tija kwa wachimbaji wadogo.
Awali, akizungumza
Mahandisi Paul Gongo Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya Matundasi ASM Limited inayo ratibu, kuendesha na kusimamia
kituo hicho, alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2005 na ilipofika mwaka
2008 kituo kili kabidhiwa rasmi kampuni hiyo ili kukiendesha.
Pia, Mhandisi Gongo alisema
kazi zinazofanyika kwa sasa kituoni hapo ni kuanzisha mashapo ya uchimbaji
madini ya dhahabu, kukusanya nguvu kazi ya rasilimali watu, kufanya marekebisho
ya mitambo na kusimika mitambo wa uchenjuaji wa madini.
Alieleza kuwa mwitikio
wa wachimbaji wadogo kupata mafunzo ni mzuri, na kwamba kuna vikundi vya
wachimbaji wadogo vilianzishwa vikasaidiwa na kituo kupata mafunzo na vitendea
kazi, alidai baadhi ya wachimbaji hao wanacho subiri ni maeneo yatakayo tengwa
na Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogo.
“tumejenga mtambo
ambao tumekiwa tukiwasagia mawe
wachimbaji wadogo kwa gharama nafuu” alisema
Mhandisi
……………ameongeza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopo kituo kinakabliwa na
changamoto mbalimbali zikiwemo upungufu wa vifaa vya kuendeshea shughuli za
uchimbaji, gharama kubwa za umeme utokana na kutumia jenereta.
Kituo hicho
kilianzishwa mwaka 2005 na Wizara ya Nishati na Madini kikiwa na lengo la kuratibu, kuendesha na kusimamia
mafunzo ya vitendo kwa wachimbaji wadogo. Ilipofika mwezi Januari 2009 kituo
kilikabidhiwa kwa Kampuni ya Matundasi ASM Limited. Kampuni hiyo kwa sasa
inajumla ya wafanyakazi 65 katika eneo la kituo na tayari katika shughuli
zauchimbaji inazofanya inauwezo wa kuzalisha Gramu 500 za dhahabu kwa mwezi.
Huko ikiuza dhahabu hiyo kwa wafanyabishara wa ndani ya nchi pekee.
Kamanda wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN Ametoa vyeti kwa madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda zaidi ya 151 wa Igurusi Wilaya ya Mbarali.
Madereva Bodaboda wakijipanga tayari kwa kwenda kupokea vyeti vyao |
Madereva Bodaboda wakiandamana kuelekea kupokea vyeti vyao toka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya |
Kamanda wa wa Polisi Mkoani MBEYA DIWAN ATHUMAN akiongea na madereva Bodaboda kabla ya kuwakabidhi vyeti vyao |
Madereva walikabidhiwa vyeti hivyo baada ya kupatiwa mafunzo ya alama za usalama barabarani kwa msaada wa shirika lisilo la Kiserikali kwa kushirikiana na Kikosi cha usalama Barabarani Mkoani Mbeya. |
Picha ya pamoja |
..........................
Mungu aliniamuru nijiuzulu, asema Papa Benedict XVI;
Jana, vyombo vya habari vilimkariri Papa Mstaafu Benedict akimweleza mgeni wake kuwa aliitwa na Mungu kwa miujiza.
Kiongozi huyo ambaye alishangaza watu kwa uamuzi huo wa Februari 8, mwaka huu, hata hivyo alisema sauti ya Mungu imejibu kupitia kwa mfuasi wake, Papa Francis.
Papa Benedict alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Februari 11, maelezo yake yalielekeza katika afya yake.
Alisema nguvu zake zilikuwa zimepungua kiasi cha kutokuweza kumudu majukumu yake ipasavyo.
Alisema, "Mungu aliniambia 'niondoke,' nami nikatimiza wajibu huo bila kusita," alisema Papa Benedict ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza kufikia uamuzi huo baada ya miaka 600 ya Kanisa Katoliki. Alisema tangu wakati huo ameishi maisha ya sala.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 86 alisema ameshuhudia maono ya Mungu kwa miezi kadhaa huku akisikia sauti na tamaa ya kuendelea kuwa karibu naye (Mungu).
Papa Benedict, hata hivyo alisema Mungu amembariki na kumwezesha kuuona utukufu wake kupitia kwa Papa Francis, akielewa kwa nini alitakiwa kuondoka mapema kwa kuitika sauti na utashi wa Mungu.
Shirika la Habari la Kikatoliki (Zenit), hata hivyo halikueleza ni nani aliyekuwa akizungumza na Papa Benedict.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Papa Benedict imeungwa mkono na vyanzo vya kuaminika kutoka Vatican.
"Ni ripoti ya kuaminika, ina usahihi, inaeleza mchakato wa kiroho ambao Papa Benedict aliupitia kabla ya kujiuzulu, vyanzo hivyo vililiambia gazeti la The Times.
Wachunguzi wa mambo wamekuwa wakieleza kuwa Papa Benedict alikatishwa tamaa na kuvuja kwa siri za mawasiliano yake binafsi na msaidizi wake .
.............................................................................
WATU MILIONI 2.9 KUCHUKULIWA ALAMA ZA VIDOLE NA PICHA
Bw.
Thomas William Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na hifadhi hati wakati
alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu idadi ya watu waliochukuliwa
alama za vidole kushoto ni Georgina Misama afisa habari wa Idara ya
Habari Maelezo.
Meneja
wa Uchambuzi wa mfumo wa kompyuta NIDA Bw. Mohamed Mashaka akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari jinsi mtambo huo unavyofanya kazi.
………………………………………………………………………………………
Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la uchukuaji alama za
vidole, picha na saini za kielekroniki kwa waombaji wa Vitambulisho vya
Taifa katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo watu wapatao milioni 2,900,000
wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo.
Zoezi hili
lilianza Julai 15 katika wilaya ya Temeke ambayo imegawanywa katika
kanda tano, itafuatiwa na Wilaya ya Ilala na kuhitimishwa na Kinondoni.
Kila Wilaya
imegawanywa katika kanda, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri
na kurahisisha zoezi kwa kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kukaa muda
mrefu kusubiri katika foleni.
Zoezi la
uchukuaji alama za vidole linakwenda sambamba na ujazaji fomu kwa
waombaji wapya ambao hawakupa fursa ya kujaza fomu wakati wa zoezi la
ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa.
Waombaji
wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usajili na nyaraka halisi za
kuthibitisha uraia na umri mathalan, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, vyeti
vya elimu ya msingi na sekondari, leseni ya udereva, kitambulisho cha
bima ya afya na kitambulisho cha mpigakura.
Zoezi la
Utambuzi na Usajili wa watu lina hatua mbalimbali ambazo zinatakiwa
kufuatwa kwa lengo la kuweza kukusanya taarifa sahihi kwa lengo la
kutumika na mifumo mingine. Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-
- Ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili;
- Uhakiki wa awali wa fomu za maombi;
- Uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta;
- Kuthibitisha taarifa za mwombaji zilizo katika mfumo wa kompyuta;
- Uchukuaji wa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki;
- Utengenezaji wa Daftari Kuu la Taarifa za Watu;
- Uhakiki wa mwisho;
- Uchapishaji na Ugawaji wa Vitambulisho.
Mfumo
huu una faida kubwa sana kwa taifa hili, hususan katika nyanja za
kiuchumi kijamii na kiulinzi. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo:-
- Kumtambua Mtanzania, mgeni na mkimbizi
- Kusidia katika kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi ya Serikali kwa njia ya kuwatambua wachangiaji wengi zaidi
- Kuondoa wafanyakazi hewa katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini
- Kusaidia suala la utambuzi hususan kwenye mabenki na hivyo kuwasaidia wananchi kupata mikopo kwa urahisi zaidi
- Continue reading →