Wednesday, September 18, 2013

WANAHABARI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, WANOLEWA NA MCT KATIKA UKUMBI WA PARADISE MBEYA

 Mwezeshaji wa semina ya mazingira hatarishi kwa waandishi wa habari na Taifa, Beda Msimbe akitoa mada mbele ya wanahabari kutoka mkoa wa Ruvuma, Mbeya, Rukwa na Katavi.
 Darasa linaendelea..
 Baadhi ya washiriki...
 Baadhi ya washiriki wakiwa wanasikiliza kwa makini... Sikilizeni vizuri maana ni lazima pia waandishi tujikosoe na kutambua kuwa hakuna kosa ambalo halileti madhara, na muhimu kabla ya kuandika, tujiulize kuwa je tupo ndani ya nchi au tupo nje?''


  PIC PAMOJAWaandishi Habari wa mikoa ya Mbeya,  Katavi,  Rukwa na Ruvuma wakiwa nje  ya Hoteli ya Mbeya Paradise katika Picha ya Pamoja na wawezeshaji mara baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili iliyohusu nanma ya kujilinda wakatika wa kuandika habari maeneo hatarishi au maeneo yasiyorafiki kama maeneo ya vita.

Waandishi Habari wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili taratibu na Kanuni zinazotawala taalum ya Habari ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza katika jamii.
Rai hiyo imetolewa na Beda Msimbe wakati akiwasilisha mada inayohusu maadili ya uandishi Habari   kwenye mafunzo ya siku mbili  ya Waandishi wa Habari  katika maeneo hatarishi na  jinsi gani ya waandishi watakavyoweza kujilinda ili wasiweze kuzulika wakati wanatekeleza kazi zao za uandishi wa Habari. 

Akiwasilisha Mada inayohusu maadili ya Uandishi wa Habari Mwezeshaji huyo kutoka (MCT) ambaye pia ni Mwandishi Mkongwe katika Tasinia ya Habari  hapa Nchini  ameeleza kuwa tatizo kubwa kwa waandishi wa sasa hawazingatii madili ya Uandishi wanapokuwa wanafanyakazi za uandishi hali ambayo inaleta migongano miongoni mwa jamii.

“Waandishi kwanza niwavivu wa kusoma hawataki kujituma ili kuweza kufanya mambo kwa uhakika tofauti na waandishi wa siku za nyuma na wengine miongoni mwetu hao hao wanajifanya polisi, usalama wa taifa Uhamiaji hao hao achana na mambo hayo fanya kazi yako ya uandishi kwa kufuata misingi ya kazi yakomtakufa hatutaki maiti sisi tunataka ututlete habari maiti hataweza kuongea naye wala hatoweza kutusaidia sisi”alisema Msibe.
Utaacha familia inateseka bure watoto wako wazazi wako hao ndi watakaohangaika,”Sisi tunapenda uishi tuona unaendelea kuishi hatupendi mfe ndiyo maana tunakuja kuwapa mbinu za kujilinda,na ipo haja ya watu kujiunga na mafunzo ya mgambo angalau muelewe jambo mbinu kidogo za kujilinda kwa wale ambao hawakupita Jeshila kujenga Taifa JKT”aliongeza kusema.

Mwezeshaji huyo ameendelea kueleza kuwa kulingana na mazingira yaliyopo sasa waandishi wamekuwa wahanga wa mashambulio ya kupigwa kumwagiwa tindikali,kujeruhiwa na pengine kuuwawa kutokana na migongano inayojitokeza .
Kutokana na waandishi wenyewe wakati mwingine wanachangia wanapoandika habari ambazo zinapendeea upande mmoja au zinazoegemea upande mmoja upande wa pili unaonekana kama umeonewa inakuwa chanzo cha migogoro.
Naye Liliani Timbuka akiwasilisha mada inayohusu jinsia na unyanyaswaji unaofanyiwa wanawake, watoto,  na watu wenye ulemavu katika jamii alieleza kuwa habari za wananwake na watoto  zinaandikwa vibaya  na kwa wingi zaidi.

Timbuka alfafanua kuwa   tofauti na habari za watu wengine kama wanaume badala  ya kuuandikwa kwa uzuri unakuta ubaya zaidi ndio unaotawala katika habari za jinsia fulani hasa wananawake hapo haki haitendeki yale mabaya wanayofanyiwa ndiyo yanayoandikwa kwa wingi sana hali hiyo siyo zuri kwa jamii inayohusika inajisikia kutotendewa haki.
Ameasa wandishi wa Habari  waisaidie jamii kwa kuandika mambo ambayo yatasaidia kujenga na kuondoa matatizo katika jamii husika ili jamii hiyo iweze kupata maendeleo.
Alieleza kuwa Waandishi wa Habari ni watu muhimu sana wao ndio wanaoweza kujenga nao wao hao hao ndio wanaoweza kubomoa hvyo ni wajibu wa waandishi kufanya kazi zao kwa kuzingatia madili taratibu kanuni  na sheria za uandishi zinavyosema ili kueousha migogoro.
Kwa upande wake Mshiriki wa semina hiyo kutoka Rukwa Nsima Ernest ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Semina hiyo alieleza kuwa waandishi wa Habari wamekosa uzalendo ndiyo maana wanafanya mambo ambayo hayaendani na taalamu waliyosomea wanatakiwa wajitume wajitoe wawe na uzalendo na nchi na kile wanachikifanya,.

Aidha ameleza kuwa wajitoe na  watambue kuwe Dhaman ya ulinzi wake uko mikononi mwake mwenye kwanza kabla ya mtu mwingine,  kwanza watambue hilo na wasijiingize katika masuala ya kisiasa wafanye mambo kulingana na taaluma waliyonayo.
Ili waandishi wa Habari waweze kwenda vizuri ni lazima warudi kwenye misingi ya Uandishi wa Habari wazingatie 5Ws+H iwapo watafuata hayo wataandika habari zenye ukweli, usahihi,zisizopendelea upande wowote na hapo wataepusha migongano na kupunguza chuki na kupigwa kwa kuwa watakuwa hawajapendelea upande wowote bali watakiwa wametenda haki.
Lakini  kwa wakati huu waandishi wa Habari wamekuwa sehemu ya ushabiki kwa kuandika taarifa bila kuzifanyia utafiti matokeo yake ni kuchochea migogoro katika jamii.
Semina hiyo iliwashirikisha waandishi wa Habari kutoka  Mikoa Minne ya Mbeya, Rukwa,  Katavi na Ruvuma, iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa ajili ya kuwapatia Mafunzo na mbinu  za kujilinda wakati wakiwafanya kazi katika maeneo hatarishi kwa maisha yao kulingana na hali ilivyo kwa sasa kulingana na mabadiliko na Mazingira yaliyopo kwa sasa ambayo waandishi wengi wanauwawa kila kukicha kote dunia na Tanzania ikiwemo.

TCRA WAANZA KUWANOA MA BLOGGERS TANZANIA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sekta ya watumiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya Viongozi na Bloggers wakiwa wanafuatilia kwa umakini Mafunzo
 Sehemu ya Wapiga Picha kutoka Vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea na zoezi la kuchukua matukio mbali mbali wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Bloggers mbali mbali hapa nchini  wakiwa kwenye Warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.


 Kutoka Kulia ni Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joesph Mwaisango akiwa na Blogger Rashid Mkwinda wakifuatilia kwa umakini mafunzo
 Baadhi ya Bloggers wakifuatilia Jambo kwa umakini
 Kutoka kushoto ni Fredy Anthony ambaye anatokea Blogs za Mikoa pamoja na Muwakilishi wa Full Shangwe Blog
 Kutoka kushoto ni Dotto Kahindi kutoka Blog ya Tabia Nchi akiwa na Adela Kavishe
 Mkurugenzi wa Google Africa Joe Mucheru akitoa mada wakati wa Mafunzo kwa Bloggers
 Mmoja ya watoa Maada katika Maswala ya Mitandao ya Kijamii Liz Wachuka akizungumza jambo wakati wa Mafunzo kwa Bloggers.

 Meza kuu wakifuatilia Mada kwa umakini
 Liz Wachuka Akijibu maswali yaliyo ulizwa na Bloggers
 Afisa Habari wa TCRA Doris Saivoye  akizungumza Jambo wakati wa Mafunzo kwa Bloggers.

Baadhi ya Bloggers wakiwa katika jengo la Mawasiliano Tanzania Baada ya Mafunzo katika siku ya kwanza.

Post a Comment