Monday, October 21, 2013

BABA AUZA NYUMBA MTOTO AKIWEMO NDANI NA KUTOKOMEA


“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  
Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.
Hii ndiyo nyumba iliyouzwa mtoto akiwa ndani
Mwandishi Joseph Mwaisango akizungumza na mwenyekiti wa kijiji cha Hatwelo Ibrahim Mponzi katikati akiwa  na barozi juu ya uuzwaji nyumba hiyo

Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.


VITENDO vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hususani vijijini, licha ya Serikali na asasi mbali mbali kulipigia kelele ambapo hivi karibuni Baba mmoja aliamua kuuza nyumba ikiwa na watoto ndani na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wasijue la kufanya.
Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.
Akizungumzia sakata hilo kijijini hapo, Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku tano.
Alisema baada ya kumfungulia mtoto huyo ndipo ilipobainika kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeshauzwa huku mtoto akiwa ndani na ndipo mnunuzi alipofunga na kufuli bila kujua kama kuna mtoto ndani huku watoto wengine wakiwa kwa ndugu zao ambao pia hawakuelezwa kama nyumba imeuzwa.
Nyumba hiyo iliuzwa kwa Dati Nsagaje kwa gharama ya shilingi 750,000/= ikiwa ni nyumba mbili pamoja na kiwanja ambapo mnunuzi huyo alilipa kianzio cha shilingi laki nne biashara iliyofanyika tangu April 26 mwaka huu  na kiasi kilichobaki wakiwa wameahidiana kulipana Mwezi Mei 15, Mwaka huu.
Wahanga wa tukio hilo ambao ni watoto walisema hawakuwa na taarifa zozote za kuuzwa kwa nyumba wanayokaa ambapo walisikia kuwa baba yao ameenda Sumbawanga kumfuata  mke wake ambaye inasemekana aliolewa na mwanaume mwingine.
“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel.  
Mtoto mwingine aliyetelekezwa ambaye siku ya tukio alikuwa ameenda kulala kwa bibi yake Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuonesha kukosa uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walishiriki moja kwa moja zoezi hilo huku wakiwa wamesaini kama mashahidi na kugonga mhuri wa Serikali ya Kijiji walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo hawakuwa na majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Hatwelo, Ibrahimu Mponzi, alisema kitendo alichokifanya muuzaji ni cha kawaida kwa sababu ameuza mali yake mwenyewe na kwamba wao kama majirani na serikali ya kijiji hawawezi kuhoji atakako waacha watoto kwa sababu ni mipangilio ya maisha ya kila mtu.
Mbali na mwenyekiti wa Kijiji kuwa shahidi wa upande wa mnunuaji akiwa sambamba na watu wengine wanne akiwepo Mkewe ambaye pia ni Balozi wa nyumba kumi pia waliosaini wengine ni ndugu wa mnunuaji ili hali muuzaji akiwa hana shahidi hata mmoja.

No comments: