Na Baraka Mpenja
KOCHA
wa klabu inayosumbua na kuumiza vichwa wa wanamichezo wengi kwa sasa
nchini, timu bora ya Mbeya City, Mwalimu Juma Mwambusi amesema malengo
yake kila anapoingia uwanjani ni kutafuta ushindi, lakini anaacha
asilimia kadhaa ili matokeo ya mpira yaamua.
Akizungumza na Mtandao wa FULLSHANGWE mara
baada ya kupata ushindi wa jana wa mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers
Uwanja wa A.H. Mwinyi mjini Tabora, Mwambusi alisema timu yake bado ni
mpya, imepanda ligi kuu msimu huu, lakini kila wakati anajipanga
kupambana kusaka pointi tatu muhimu na ndio maana wamekuwa wakipata
matokeo mazuri wakiwa wahawajapoteza mchezo wowote mpaka dakika hii.
“Ligi
ni ngumu na sisi ni wageni kwa sasa, tumefanya maandalizi ya mechi zote
26, kila timu tunayocheza nayo tunatarajia kushinda. Tumepata sare
nyingi sana, ila kwa sasa tunashinda, tunamshukuru Mungu kwa hilo na
tunaendelea kujipanga zaidi na zaidi”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi
alisisitiza kuwa mpaka sasa wameshakutana na timu kubwa zenye uwezo
mkubwa na majina makubwa kuliko wao wakiwemo Simba, Yanga, Kagera na
wamehimili mikikimikiki, lakini kwasasa wanakutana na timu zenye uwezo
kama wao, hivyo matokeo ni muhimu kabla ya kuelekea mzunguko wa pili
ambao huwa na changamoto nyingi zaidi.
Kocha
huyo mwenye historia ya mafanikio kila anapokabidhiwa timu mpya,
aliwasifu na kuwapongeza mashabiki wa Mbeya ambao kwa kiasi kikubwa
wamekuwa wakiiunga mkono timu toka inacheza ligi daraja la kwanza na
mpaka sasa ligi kuu.
“Nawapa
mkono wa hongera masbaiki wetu, wamekuwa pamoja na sisi na kuonesha
umoja mkubwa, hakika wazidi kutitia moyo katika safari hii ya kusaka
mafanikio. Lengo letu ni kuwapa raha kwa kufanya vizuri na ndio maana
kila mechi tunapoingia uwanjani tunawafikiria wao kwanza”. Alisema
Mwambusi.
Baada
ya matokeo ya jana, Mbeya City wamejikusanyia pointi 14 sawa na Yanga,
lakini wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Akizungumzia
mechi ijayo dhidi ya Mgambo JKT katika dimba la Mkwakwani jumapili
(septemba 13), Mwambusi alisema hesabu zake ni kutafuta pointi tatu,
huku akisema wapinzani wao wana uwezo unaoelekeana na wao tofauti na
timu walizokutana nazo.
“Tunaelekea
Tanga kusaka ushindi, na hayo ndio malengo yetu. Mara zote tuko tayari
kushindani na timu yoyote inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara,
hivyo mashabiki wajiandae kupata burudani”. Alisema Mwambusi.
Mechi
nyingine za jumapili zitawakutanisha Ashanti United dhidi ya Coastal
Union, Azam fc watavaana na JKT Ruvu, Mtibwa Sugar watawakaribisha JKT
Oljoro, wakati Ruvu Shooting watakula sahani moja na Rhino Rangers ya
Tabora.
No comments:
Post a Comment