Jeraha katika mguu wa mwandishi wa habari Shomi Mtaki lililotokana na risasi baada ya kuvamiwa na majambazi |
Shomi Mtaki akionesha jeraha lililotokana na risasi katika mguu wake wa kushoto |
Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One wilayani Mbozi Danny Tweve alipomtembelea Shomi Mtaki kumjulia hali baada ya kuvamiwa na majambazi na kujeruhiwa kwa risasi |
Mke wa Shomi Mtaki ambaye naye alijeruhiwa na baruti kifuani kwake |
Sehemu ambayo risasi ilipigwa katika mlango |
Mwandishi wa habari Dany Tweve akishuhudia Eneo la tukio
Namna ambavyo majambazi yalivyofanya upekuzi katika chumba cha Mtaki kutafuta fedha walizodhani kuwa amehifadhi |
Shomi Mtaki aliyejeruhiwa kwa kipigwa risasi na majambazi |
Ndugu na jamaa wakiifariji familia ya Mtaki baada ya tukio hilo la uvamizi na kupigwa risasi |
Kamanda wa Polisi wilaya ya Momba Bw. Chitanda akimpa pole Shomi Mtaki |
Nyumba na trekta katika shambani kwa Shomi Mtaki katika mji mdogo wa Mpemba Tunduma wilayani Momba |
NI
wiki ya majanga kwa waandishi wa habari nchini, muda mfupi baada ya
kupata taarifa ya kupigwa risasi kwa Mwandishi wa habari wa ITV /Radio
One Mwandishi mwingine wa gazeti la Uhuru mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya Shomi Mtaki amepigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi shambani kwake katika mji mdogo wa Mpemba.
Mtaki
ambaye alikuwa katika nyumba iliyopo shambani kwake alivamiwa usiku wa
Octoba 10 na watu watano waliokuwa na silaha aina ya bunduki kisha
kumlazimisha kutoa fedha.
Wanablogu
waliomtembelea shambani kwake walishuhudia majeraha aliyokuwa nayo
Mtaki katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo alisema kuwa siku
hiyo majira ya saa 9:00 usiku alisikia mchakato wa miguu nje ya nyumba
yake na kwamba alipochungulia aliwaona vivuli vya watu wakiwa wamesimama
karibu na trekta lake nje ya nyumba.
Alisema
kuwa alipowashitua watu hao walitamka wazi wazi kuwa wanataka fedha na
muda huo huo akasikia kishindo kikubwa katika mlango wa kuingilia
sebuleni ambapo wavamizi hao walikuwa wamepiga jiwe aina ya FATUMA kwa
lengo la kuuvunja mlango ili waingie ndani.
Alisema
kuwa mara akasikia mlio wa risasi ikipigwa katika mlango wake na mara
ukafunguka na vijana watatu waliingia sebuleni ambapo walichukua jiwe
walilotumia kuvunja mlango wa sebuleni na kupiga katika mlango wa
chumbani na kisha baadaye walimimina risasi katika mlango huo ambazo
zilimpata katika mguu wa kushoto na kumjeruhi.
Mtaki
alisema kuwa yeye na mkewe walikuwa wakihangaika na kujaribu kujiokoa
maisha yao ambapo mkewe aliposikia mlio wa risasi aliingia chini ya
mvungu wa kitanda ili kujinusuru.
‘’Nilijiona
nakikaribia kifo vijana walimimina risasi katika mlango wa chumbani
zikanikuta mguuni na kunijeruhi vibaya, mlango ukafunguka wakaingia
vijana watatu ambao hawakujiziba sura zao,’’alisema.
Alisema
kuwa mara baada ya kuingia walianza kumuamrisha atoe fedha, akawajibu
kuwa hana fedha ndipo walipoanza kumpiga mgongoni huku wakitishia kumuua
na kwamba wakati huo mkewe alikuwa amejificha katika mvungu wa kitanda.
‘’Wale
wavamizi walianza kupekuwa vitu mbalimbali, wakachukua simu yangu ya
mkononi ambayo mtu wa mwisho kuwasiliana naye alikuwa ni shemeji yangu
ambaye ni Mwanajeshi,’’alisema na kuongeza.
‘’Wavamizi
wale walichukua simu tatu, simu moja ikajipiga kwa bahati shemeji yangu
aliipokea, akasikia vurumai iliyokuwa ikiendelea nyumbani na namna
ambavyo tulivyokuwa tukijitetea ili tusiuawe, muda huo huo akaenda kutoa
taarifa polisi,’’alisema.
Alisema
kuwa wavamizi hao waliingia katika mji wake majira ya saa 8:45 na
kuendelea kuwepo pale hadi majira ya saa 9;00 usiku ambapo walichukua
simu tatu, tv seat ya nchi 22, ving’amuzi viwili kimoja cha Startimes na
kingine cha Zuku vyote vikiwa na thamani ya sh. Milioni 2.
Alisema
kuwa mara baada ya wavamizi hao kumaliza kukusanya vitu walivyoona
vinafaa waliwaamrisha kuingia chumbani na wao wakatokomea upande wa
mashariki na muda mfupi baadaye polisi walifika eneo la tukio wakatukuta
mien a mke wangu tukiwa tumekumbatiana huku tukilia na kumuomba Mungu.
..........................................
TUNAKUOMBEA UPONE HARAKA MPIGANAJI UFO SARO
Kingo tanzania tunakutakia matibabu mema na yenye
kuleta afya jema tunaomba mungu akuponye haraka ili siku moja urejee
katika kazi yako ya kuwatumikia watanzania Mungu akujalie afya njema na kukupa nafuu
haraka .kutoka kulia ni Abdull Saiboko Habari Leo, Ufo Saro mwenyewe
ITV, Said Makala Chanel Ten na John Bukuku
....................................................
No comments:
Post a Comment