Saturday, October 12, 2013

Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo asaini mkataba wa utafutaji wa mafuta

  
Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo akisaini mkataba wa utafutaji wa mafuta unaomilikishwa kwa kampuni ya Afrem Tanzania toka shirika mama la Afrem Gabon mara baada ya campuni hiyo kufungua ofisi zake nchini Tanzania na kusajili kampuni hiyo hivyo kazi zilizokuwa zikifanywa na Afrem Gabon zitafanywa na Afrem Tanzania kwa ushirika na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania wa pili toka kulia kwa Profesa Sospeter Muhongo ni Meneja wa kampuni ya Afrem Tanzania Jeremy Martin.

waziri wa Nishati na madini Akisikiliza hoja toka kwa wawekezaji wa mradi wa Kigosi Tanzania American International development corporation 2000 Ltd baada ya kuhoji mambo mbalimbali ikiwemo la endapo wanafahamu tozo mbalimbali mara baada ya kuanza uzalishaji wa madini husika.

Waziri akisaini leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya mradi wa Kigosi uliopo chini ya kampuni ya Tanzania American International development corporation 2000 Ltd

waziri wa Nishati na madini Akisikiliza hoja toka kwa wawekezaji wa mradi wa Kigosi Tanzania American International development corporation 2000 Ltd baada ya kuhoji mambo mbalimbali ikiwemo la endapo wanafahamu tozo mbalimbali mara baada ya kuanza uzalishaji wa madini husika.

Nuru I. Mwasampeta
---------------------------------
 
Ministry of Energy and Minerals

........................

HABARI YA KUSIKITISHA: KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi mitano bila huduma za msingi. jijini Mbeya

 Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake

 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha 


 Mwenyekiti wa  Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

 Agustino Steven (8) akipika mchicha

 Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula 


 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe


 Unga pamoja na maharage
 Hili ndilo sanduku lao Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi matano bila huduma za msingi.

Watoto hao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza  shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine.

Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa  Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.

Aidha watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500  ambazo huzitumia kununua mahitaji ya nyumbani pamoja na kujipikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Amesema majirani pia waendelee kuwa karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao watakapopatikana kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida.

Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo pia alitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili.
 
Wazazi hao wanatabia kama hiyo kutokana na kuwahi kumtelekeza binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Salome Steven ambaye hakuwahi kupelekwa shule hivyo kuachiwa jukumu la kuwalea wadogo zake.

Kutokana na ugumu wa maisha binti huyo katika harakati za kutafuta chochote kwa ajili ya wadogo zake ameishia kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake nay eye kukimbilia kwa rafiki yake.

Pia Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia limeamua kulifuatilia suala hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti ).

Na mbeya yetu
Post a Comment