Thursday, November 28, 2013

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AICHANA CHADEMA TUNDUMA-MOMBA

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana jioni ya leo, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma, ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi. Katika mkutano huo uliofabnyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, Kinana aliambatana na majenbe ya Chama cha Mapinduzi  , Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro, Katika mkutano huo Kinana amesema wananchi kuikosoa CCM sio kosa kwani Chama hicho kimeingia mkataba na wananchi pale kilipopewa ridhaa ya kuongoza nchi ili kutekeleza ilani yake ya uchaguzi na ni haki ya mtu yeyote wakiwemo wapinzani ili kujua maendeleo yao, Amesema CCM haitakubali kuona ukiritimba na umangimeza wa baadhi ya watendaji  Serikalini  unakwamisha maendeleo ya wananchi, ameongeza kuwa kazi ya CCM ni kutenda tu. na kazi ya wapinzani ni kusema maneno matupu.
SOMA ZAIDI..
  2 
Wananchi wakisakata muziki kabla ya kuanza kwa mkutano.
7 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiskata muziki na wananchi 9 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake akilekea katika eneo la  10a 
Msafara ukiwasili mjini Tunduma ukitokea wilayani Ileje 11 
Maelefu ya wananchi wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana hayupo pichani alipokuwa akiwahutubia.12 
Hapa akisisitiza jambo kwa wananchi hao wakati akitoa hutuba yake 13 
Mzee wa kimila wa kabila la wanamwanga wilayani Momba Jubeki Chipansia akimpa silaha za kijadi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumsimika kuwa miongoni mwa wazee wa kabila hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduma leo jioni.

No comments: