Saturday, November 16, 2013

Nida: Watendaji wanaodai fedha za vitambulisho kukiona

NIDA1 a9f58
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imewaonya baadhi ya watendaji wanaodaiwa kuwatoza fedha wananchi kwa ajili ya kuwapatia vitambulisho hivyo na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua za sheria.
SOMA ZAIDI...


Aidha, imesema zoezi la utaoji wa vitambulisho limefikia katika hatua ya kuchukua ala
ma za vidole na picha kwa watu waliojaza fomu za kuviomba.

Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu, akizungumza katika mahojiano na Radio One, alisema zoezi la vitambulisho linagharamiwa na serikali kwa asilimia 100, hivyo hairuhusiwi mtendaji yeyote kumtoza fedha mwananchi.

Alisema zoezi linaendelea katika wilaya za Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar na kuwa wanaopuuza kupata vitambulisho vya taifa watapata athari ikiwamo kushindwa kupata huduma mbalimbali kama kufungua akaunti au kupata ajira.

Kuna madai kuwa baadhi ya watendaji wa mitaa wamekuwa wakiwatoza Sh. 2,000 watu wanaokwenda katika ofisi zao ili kugongewa mihuli.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment