Sunday, November 10, 2013

UMISAVUTA KANDA YA KUSINI YAANZA TENA TANGU KUSITISHWA MWAKA 1995

KATIKATI NI MKUU WA CHUO CHA UALIMU TUKUYU MATHIAS MVULA  AKIWA NA PHILIP KHAMIS MAKAMU MKUU WA CHUO CHA TANDALA NA KULIA NI JOHN V. WAKIWA WANASHUHUDIA MPAMBANO WA MPIRA WA MIGUU MECHI YA PILI KUNDI B KATI YA TUKUYU TC & TANDALA TC NA MATOKEO TUKUYU TC 3 & TANDALA TC 2

VIJANA WA TUKUYU TC WAKIWA MAPUMZIKO HUKU WAKIONGOZA KWA 2 NA TANDALA 1

KIKUNDI CHA HAMASA CHA TUKUYU TC WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA TIMU YAO INAIBUKA NA USHINDI KIVUTIO KUKUBWA KATIKA KUNDI HILI NI KUMUONA MSICHANA MMOJA TU AKISHANGILIA TIMU YAO YA TUKUYU TC

TIMU YA TANDALA TC WAKIWA MAPUMZIKO HUKU WAKIWA NA GOLI MOJA NA TUKUYU TC 2
HAMASA NI MUHIMU KATIKA KUSAKA USHINDI


TUKUYU TC WAKIPATA GOLI LA TATU THIDI YA TANDALA TC


BAADHI YA WALIMU WA TUKUYU TC WAKIWA MAKINI KUANGALIA MECHI AMBAPO VIJANA WAO WAMEIBUKA NA USHINDI WA MAGOLI 3 KWA 2

KAULI MBIU YA MASHINDANO HAYA YA UMISAVUTA NYANDA YA KUSINI NI KUIOMBEA AMANI TANZANIA
UMISAVUTA NI MICHEZO INAYOWAKUTANISHA WANAMICHEZO WA VYUO VYA UALIMU NA TANGU MWAKA 1995 MICHEZO HII ILIFUTWA VYUONI ILA KWA KUONA UMUHIMU WA MICHEZO MASHULENI NA VYUONI SERIKALI IMELEJESHA TENA MICHEZO HII HIVYO MWAKA HUU NDIO MWAKA WA KWANZA KUANZA MICHEZO TENA VYUONI NA KWA KUANZIA MICHEZO MITATU INACHEZWA NA JUMLA YA VYUO 8 KATI YA 17 NYANDA YA KUSINI

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA NDIYE KAFUNGUA MICHEZO KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA UALIMU TUKUYU NA KUSISITIZA AMANI NA UPENDO KATIKA MICHEZO ZAIDI AMESEMA BILA AMANI TANZANIA HAKUNA MICHEZO NA SHUGHURI ZA KIUCHUMI ZITAZILOTA HIVYO AMEWATAKA WANAVYUO NA JAMII KUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU NA HII NDIO KAULI MBIU YA MICHEZO YA UMISAVUTA MWAKA HUU MICHEZO INAYOTARAJIWA KUFUNGWA TAREHE 13.11.2013 AMBAPO WASHIDI WATAPATIKANA NA KUTANGAZWA PAMOJA NA KUPEWA ZAWADI ZAO.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
Post a Comment