UMOJA
wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeanza utaratibu
wa kutoa vyeti maalum kwa wanachama wa klabu za waandishi wa
habari nchini ambao wanapatiwa mafunzo mbali mbali.
Mkurugenzi
mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan alisema kuwa vyeti hivyo
vimeanza kutolewa baada ya maadhimio ya wajumbe wa mkutano mkuu .
Hivyo alisema kuanzia sasa wanachama wa vilabu ambao watapewa mafunzo wanachama wake watapewa vye vyeti maalum .
Pia alisema vyeti hivyo vitakuwa vya viwango vya juu na vinaanza kutolewa sasa kwa vilabu hivyo.
Wakati
huo huo umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC)
umewataka viongozi wa vilabu hivyo mikoani kutumia changamoto
zinazojitokeza katika maeneo yao kujipanga badala ya kuzichukia
changamoto hizo.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Mwanza na Rais wa UTPC Kenneth Simbaya
wakati akifungua mkutano mkuu wa wanachama wa klabu za waandishi wa
habari .
Simbaya
alisema kuwa mbali ya kuwepo kwa mafanikio makubwa katika klabu
vya waandishi wa habari nchini ila bado wapo baadhi ya viongozi ambao
wameendelea kukwepa changamoto mbali mbali badala ya kuzifanyia
kazi.
No comments:
Post a Comment