Mtoto Kalebu Simwelu(6) enzi za uhai wake, mtoto huyu alichinjwa na kaka yake kwa madai kuwa baba yake alimrithisha mali zote. |
Mwili wa marehemu Kalebu ukiingizwa katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia. |
Ibada ya mazishi ikiendelea katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia |
Umati wa waombolezaji uliohudhuria maziko ya mtoto Kalebu ambaye aliuawa kwa kuchinjwa na kaka yake aliyedai kuwa baba yao amemuandikisha mali zote. |
Jamaa na ndugu wakiendelea na mazishi katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia ambako mtoto Kalebu alizikwa. |
KATIKA
hali isiyo ya kawaida mmoja wa watoto wa Diwani wa Kata ya Nkangamo
Weston Simwelu(55) ambaye watoto wake waliuawa kwa kuchinjwa na
kunyongwa,Enock Simwelu(23) amekiri kufanya mauaji hayo kwa madai kuwa
yametokana na baba yao kumrithisha mali zote marehemu mdogo wao.
Mauaji
hayo yalitokea Disemba 19 eneo la TAZARA katika mji mdogo wa Tunduma
ambapo wauaji walivamia nyumbani kwa Diwani huyo na kufanya mauaji
ambapo walimchinja kwa kisu mtoto Kalebu Simwelu(6) na mfanyakazi wa
ndani Sista Nyirenge(17) na miili yao kuficha sebuleni nyuma ya kochi.
Imeelezwa
kuwa Enock pamoja na nduguye wa mama mmoja Gabriel walishirikiana kwa
pamoja kufanya mauaji hayo kwa madai ya baba yao kufanya upendeleo kwa
mdogo wao Kalebu(6) ambaye ni mtoto wa mke mdogo wa baba yao.
‘’Chanzo
cha mauaji hayo kimebainika, mtoto wa mke mkubwa wa Diwani, Enock
amekiri kuhusika na mauaji hayo ameshirikiana na nduguye Gabriel
Simwelu, madai yao, baba yao amemwandikisha mali zote marehemu Kalebu,
mtoto wa mke mdogo wa Diwani,’’amesema Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa
Mbeya Barakael Masaki katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa
na Kamanda Masaki ni kwamba mmoja wa watuhumiwa walioshikiliwa kwa ajili
ya mahojiano ambaye ni kaka wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Enock
Simwelu(23) amedai kukiri kufanya mauaji hayo akishirikiana na mdogo
wake aliyemtambulisha kwa jina la Gabriel Simwelu(19).
Kulingana
na taarifa hiyo ni kwamba mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye amehusika
moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na tatizo la baba yake kuandikisha
mali zote kwa mdogo wao ambaye ni mtoto wa mke mdogo Kalebu Simwelu.
Kamanda
Masaki alisema kuwa mauaji hayo pia yalifanywa kwa kushirikiana na
jirani na rafiki yao aliyefahamika kwa jina la Patrick Msigwa(18) mkazi
wa eneo la Majengo katika mji mdogo wa Tunduma.
Mara
baada ya kutokea kwa mauaji hayo Jeshi la Polisi liliwanasa watu watano
wakiwemo watoto wa mke mkubwa wa Diwani Simwelu ambapo kulingana na
madai ya awali ni kwamba chanzo kilitokana na mgogoro wa kifamilia.
Wakati
tukio hilo la mauaji linatokea Baba wa marehemu Simwelu alikuwa
shambani katika kijiji cha Kipaka ilhali mama mzazi wa mtoto Tumaini
Yohana(29) alikuwa kazini katika Ofisi ya Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Aidha
mazishi ya mtoto Kalebu yalifanyika Disemba 21 kwenye makaburi ya
Nakonde katika mji mdogo uliopo nchini Zambia na kuhudhuria na umati wa
wakazi wa mpakani mwa Tanzania na Zambia ambapo mwili wa mfanyakazi wa
ndani Sista Nyirenge yalifanyika katika kijiji cha Isansa wilayani
Mbozi.
(PICHA KWA HISANI YA SHOMI MTAKI-TUNDUMA)
No comments:
Post a Comment